Kuanzia jana nimemuelewa Freeman Mbowe

Kuanzia jana nimemuelewa Freeman Mbowe

Mubby777

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2018
Posts
1,627
Reaction score
5,714
Nilikuwa disapointed sana tangu mikutano iliporuhusiwa jinsi Chadema walivyokuwa wanampamba Mama Samia ndipo nikaamini wamelamba asali. Ila baada ya jana nimepata picha.

Tuendelee na siasa za kupiga makelele jukwaani tukitukana CCM na kupambana nayo kibabaae huku tume ikiwa sio huru na katiba hiihii inayokipa chama tawala mamlaka juu ya polisi/ mahakama/ bunge nk. Je, hii siasa itatatufikisha wapi? Chama gani kilifanikiwa kwa style hii wakat katiba ikiwa mbovu? Hakuna

Kuendelea kupambana na serikali tutaishia kuwekwa ndani huku amna anayehangaika kusaidia na kwa bahati mbaya hawa watanzania ni waoga kuliko kinyonga, kama huamini waambie waandamane kama utakuta mtu barabarani [emoji23][emoji23]

So kama mama anakubali kukaa na kuongea na kuahidi ataleta katiba mpya na tume ya uchaguzi huru na tuko nae kwa maridhiano na anaonesha kabisa ana hiyo nia, Je twende mikutanoni kumtukana tena? Ili abadili mawazo? Hapana acha tuwe wajinga tumsifie na kumjaza ili avimbe kichwa but tunachokitaka kifanikiwe.

Hiyo kenya mnayoona inabadili vyama tawala kila siku ni kwa sababu tume ni huru na mahakama ni huru.

Bila kuwa na tume huru na mahamaka huru na katiba mpya ndg zangu hakuna siku tutaishinda CCM.

Love long Mbowe mimi nimekuelewa na nakuunga mkono endelea kujifanya bwege lengo lako likitimia utakuwa shujaa ambaye utakumbukwa milele.
 
Wafahidhina na mataga watamwaga sana povu hapa, wanakuja.
Wapo kila upande
FqsVdVaWIAAapSB.jpg
 
Unadhani kwanini Dkt. Samia kaamua kufanya maridhiano na Chadema pekee bila vyama vingine vya upinzani?
 
Upinzan kuna chama kimoja ndg hivyo vingine utaita vyama?
Upande wa Zanzibar CCM inaunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUKI) na Chama Cha ACT-Wazalendo ambacho ni chama cha upinzani huku BARA.

Unatumia hoja ipi kudai kwamba ACT-Wazalendo sio chama makini Cha upinzani nchini?
 
Ukijua vya hivi🤛👈
Wengine wanajua vya hivi🤜👉
 
Nilikuwa disapointed sana tangu mikutano iliporuhusiwa jinsi Chadema walivyokuwa wanampamba Mama Samia ndipo nikaamini wamelamba asali. Ila baada ya jana nimepata picha...
Sana tu.
 
Back
Top Bottom