Kuanza kwa Vita Baridi kuna athari gani kwa Demokrasia ya Afrika

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,372
6,078
Kuanza kwa vita baridi kati ya Urusi na Marekani kutaathiri na kurudisha nyuma sehemu kubwa ya Demokrasia iliyokuwepo Africa kwa miongo miwili. Baada ya vita vikuu vya pili ya dunia mataifa haya makubwa yalipambana sana kupata ushawishi kwenye nchi nyingi za kiafrika bila kujali utawala bora, demokrasia na haki za binadamu, kwa kifupi watawala wengi wa africa walikuwa madikteta kwa kusaidiwa na Marekani ama Russia kwa mfano huu:

1969 mapinduzi yalifanyika nchini Somalia baada ya kuuawa kwa Rais Sharrmake aliyekuwa amechaguliwa ki Demokrasia na Meja Jeneral Siaad Barre akachukua madaraka kwa kutanganza Somalia ni nchi ya kijamaa na nchi ya USSR ambayo kwa sasa ni Russia ilitambua utawala huo wa kijeshi, ikapeleka silaha nyingi na wataalam wa kijeshi Somalia ikawa nchi ya kidikiteta mfumo wa vyama vingi ukafutwa.

Mwaka 1974 Ethiopia napo palitokea mapinduzi utawala wa kifalme wa Mfalme Haile Selassa uliangushwa na Kanali Mengistu alichukua madaraka na kutanganza kuwa taifa hilo litakuwa la kijamaa, Urussi ikapeleka silaha nyingi na wataalam wa kijeshi nchi hiyo pia ikawa ya kidikiteta.

Somaliia na Ethiopia zilipigania vita mwaka 1977 baada ya Somalia kuivamia Ethiopia kudai jimbo la Ogaden, hapo ndipo Urusi na washirika wake Cuba waliisaidia Ethiopia kwenye uvamizi huo kutoka Somalia, ndipo Rais wa Somalia akaamua kuiacha sera za kijamaa na kukimbilia kutafuta msaada Marekani nao walimpaa silaha nyingi sana na wataalam wa kijeshi.

Rais Siad Barre alipinduliwa mwaka 1991 ndo vita vya wenyewe kwa wenyewe vikaanza, silaha walizotoa Urusi na Marekani zilikuwa nyingi mno kiasi ambacho nchi hiyo kwa muda wa miaka mitano hawakuhitaji kuaagiza silaha kwenye vita vyao wenyewe kwa wenyewe.

Baada ya Zaire kupata uhuru Patrice Lumumba alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa nchi hio alionekana ana mwelekeo wa sera za kijamaa ya Urusi, Marekani kwa kutumia mbinu wakapindua utawala wa ki demokrasia na kumuua Waziri Mkuu huyo na kumweka General Mobutu Sese Seko kuwa kiongozi wa nchi hiyo kwa miongo mitatu. Wakati wa vita baridi kati ya Urusi na Marekani kulikuwa na madikteta wengi duniani waliokuwa wanaunguwa mkono na Urusi ama Marekani, baada ya kuangukaa kwa dola ya USSR miaka 90 na Marekani kuacha kuunga mkono hao madikteta, wengi walitoweka kutoka kwenye madaraka na nchi nyingi ziliamua kuanzisha utawala wa ki demokrrasia.

Je, kwa kuanza kwa vita baridi kati ya Marekani na Urussi demokrasia ilioanzishwa na kudumu kwa miongo miwili hapa Afrika itaendelea kuwepo?
 
History ni mwalimu mzuri saana...ngoja tusubili tuone mwisho wake.
Kwa kifupi tutarud kuwa makoroni yao tena!.
Labda ule upande usiofungamana na upande wowote upate nguvu ..Ila Marekan Wana sera zao Kama haupo Pamoja na sisi Basi we ni adui yetu...hapo ndo anapowavuruga.
 
Back
Top Bottom