Sijui una maana gani unapotumia neno "udhu" ila kama una maana ya "usafi" basi nadhani humfahamu vizuri huyu jamaa. Frederick Sumaye ninayemjua mimi ni mmoja wa waasisi wa ufisadi ndani ya CCM. Kwa kumbukumbu zangu huyu jamaa wakati akiwa waziri mkuu aliwaambia wafanyabiashara kuwa yeyote anayetaka mambo yake yamnyookee lazima ajiunge na CCM. Matokeo yake ni wimbi la wafanyabiashara kuingia ndani ya CCM na kuzigeuza siasa za ndani ya chama kuwa biashara ya kuuza na kununua kura. Kama sikosei hajawahi kujibu kashfa ya kutumia vibaya madaraka pale alipojibinasfishia mashamba ya ushirika ya kijiji akiwa waziri mkuu .
Sijarlewa mashamba ya ushirika yepi,mbona km alishakanusha hiyo issue,inshort binafsi siwezi kumlinganisha sumae na genge la mtandao linalotaka kukamata nchi 2015 ni balaa tupu ni bora hata na la sasa,yatu watu wanaopita kwa rushwa ni hatari ni lazima fedha zao zirudi