"Kuagana"

Sooth

JF-Expert Member
Apr 27, 2009
3,928
5,615
Baada ya kuongea na rafiki zangu kadhaa, nimegundua kwamba ''Kuagana" imekuwa fasheni siku hizi.....Labda nawahukumu bure....

Ndoa ni kitu tukufu, misahafu ni shahidi,
Yataka moyo mkunjufu, hakuna mlio wa bundi,
Zawadi kama mikufu, tuzo njema kwa ushindi,
Kuagana na wa zamani, siku hizi imeshakuwa fasheni?

Zamani likuwa sifa, heshima liwekwa mbele,
Binti alifundwa vyema, katu sipige kelele,
Uwanja safi daima, watoto sipate upele,
Kuagana na wa zamani, siku hizi imeshakuwa fasheni?

Ndoa meingia doa, leo kuna kuagana,
Siku muhimu ya ndoa, wa zamani anapewa,
Penzi kama kukohoa, ni tabu kwa waungwana,
Kuagana na wa zamani, siku hizi imeshakuwa fasheni?

Kama wa zamani mzuri, kwanini hakukuoa,
Ka anukia uturi, nenda kapeleke posa,
Kwao huyu umekiri, kwa yule nataka poza,
Kuagana na wa zamani, siku hizi imeshakuwa fasheni?

Fungate haina mvuto, viungo vimelegea,
Ndoa sasa ni kipato, na bado utamegewa,
Ni moto pia fukuto, la upate ngekewa,

mmmh, kweli...Gang-mentality kills common sense.
 
Mimi nilisema hakuna haja ya ndoa siku hizi, mkanishambulia haya sasa yaoneni haya ya mshairi wetu leo!
 
Mimi nilisema hakuna haja ya ndoa siku hizi, mkanishambulia haya sasa yaoneni haya ya mshairi wetu leo!

mmh! Kama ni kweli, kwa nini watu wanalalamika ndoa zao zina kero lakini hawathubutu kutengana? Ni kwa nini mume/mke anapofiwa na mwenza wake anaoa/anaolewa tena?
 
Ninakupa 5, mashairi yametulia, vina umepangilia, na ujumbe swaaa...........fiii
wewe ni mwana malenga. .... !
 
majuti ni mjukuu, babu yangu aliniasa
nenda wangu mjukuu, uachane na anasa
ukaweke lango kuu, ukafunge na vitasa
kama imekuwa fasheni, nani wa kulaumiwa?

vionjo unavitaka, ndoa unaitaka
wafanana na maji taka, yangu ndio mashaka
hata utoe zaka, milele una mashaka
kama hukuwa tayari, uliharakia nini?
 
Huyu nae ni malenga mwingine nimependa mistari yako

majuti ni mjukuu, babu yangu aliniasa
nenda wangu mjukuu, uachane na anasa
ukaweke lango kuu, ukafunge na vitasa
kama imekuwa fasheni, nani wa kulaumiwa?

vionjo unavitaka, ndoa unaitaka
wafanana na maji taka, yangu ndio mashaka
hata utoe zaka, milele una mashaka
kama hukuwa tayari, uliharakia nini?
 
mabadiliko ya kweli, daima huanza nasi
tusikimbilie mseli, na kubambikiana kesi
tuwe na mapenzi ya kweli, ndio twende kwa kasisi
kuagana ni batili, kamwe sifagilii
 
mabadiliko ya kweli, daima huanza nasi
tusikimbilie mseli, na kubambikiana kesi
tuwe na mapenzi ya kweli, ndio twende kwa kasisi
kuagana ni batili, kamwe sifagilii

Hata mimi sifagilii, na wala situngii shairi
na wala haistaili, milele huleta shari
usiagane na mgili, chagua wako mahiri
Dunia imeharibika, tufateni maadili
 
duuh..nikiwaza hii kitu pozi zinaniisha kbc

Yaani haya mambo hayana kanuni, unaweza ukafikiri kwamba kwakuwa wewe ndiye uliyezindua mgodi, basi atakuwa na wewe tu, kumbe mwenzio anawaza na kutamani aonje njegere maana toka azaliwe anakula maharage tu. Yaani unakuta anatamani aonje nyama kutoka bucha lingine na sio lile lile kila siku..
 
majuti ni mjukuu, babu yangu aliniasa
nenda wangu mjukuu, uachane na anasa
ukaweke lango kuu, ukafunge na vitasa
kama imekuwa fasheni, nani wa kulaumiwa?

vionjo unavitaka, ndoa unaitaka
wafanana na maji taka, yangu ndio mashaka
hata utoe zaka, milele una mashaka
kama hukuwa tayari, uliharakia nini?

Give me more Shantel,
U have more 2 tell,
I will buy ur idea, just waiting 4 u 2 sell
!
 
mabadiliko ya kweli, daima huanza nasi
tusikimbilie mseli, na kubambikiana kesi
tuwe na mapenzi ya kweli, ndio twende kwa kasisi
kuagana ni batili, kamwe sifagilii

Gaga karibu jamvini, tuwakemee majizi,
Hima malenga njooni, tuwafunde wavamizi,
Afrodenzi leta kuni, tuwamulike bazazi,
Kuagana kabla ya ndoa iwe mwiko!
 
Magu panda jukwaani, nahitaji wako mzani,
Klorokwini sikuoni, una busara pomoni,
Okoa ndoa kinani, watupishe hayawani,
Kuagana unapotaka kufunga ndoa iwe mwiko.

Lizzy mbona sikuoni, nani kakuficha ndani,
Yakuonea makini, mchango wako ni thamani,
Hata kama we mpagani, ndoa iwe jukwaani,
Kuagana unapotaka kufunga ndoa iwe mwiko.
 
Huu sasa ushetani, kweli kuna ulakini
Ndoa tunazitamani, tuache wetu uhuni
Mola akitulaani, tutamlilia nani
Tusikimbilie ndoa, kama hatujatulia

Ndoa jambo la heri, vitabu vyatuambia
Iweje tufanye shari, tena kwa kudhamiria
Hapa twacheza kamari, mbeleni tutajutia
Tusikimbilie ndoa, kama hatuja tulia

sindano mwana wa ganzi

Tuko pamoja ni shughuli tu za w'end zimebana

Magu panda jukwaani, nahitaji wako mzani,
Klorokwini sikuoni, una busara pomoni,
Okoa ndoa kinani, watupishe hayawani,
Kuagana unapotaka kufunga ndoa iwe mwiko.

Lizzy mbona sikuoni, nani kakuficha ndani,
Yakuonea makini, mchango wako ni thamani,
Hata kama we mpagani, ndoa iwe jukwaani,
Kuagana unapotaka kufunga ndoa iwe mwiko.
 
Give me more Shantel,
U have more 2 tell,
I will buy ur idea, just waiting 4 u 2 sell
!
uliharakia nini, bazazi nakuambia
wakati wajuani, uroho hujakimbia
tembea mabuchani, ni ileile nakwambia
tuache tafrani , hakuna cha tofauti
 
Back
Top Bottom