Kuachana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuachana

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Felixonfellix, Oct 29, 2011.

 1. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  [FONT=&amp]Luka 16:1 8 "Kila amwachaye mkewe na kumuoa mke mwingine azini naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe azini." [/FONT] [FONT=&amp]Wapendwa katika Bwana, nawasalimu wote katika Jina la Yesu Kristo Mwokozi wetu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa. Nimesukumwa leo kulizungumzia suala hili zito: Suala la kuachana watu wawili waliokwisha kuoana, waliokwisha kukubaliana kuwa MKE na MUME. Maandiko yamesema hapo juu kuwa kila amwachaye na kuoa mwingine AZINI, na yule amwoaye yule aliyeachwa AZINI. Nimekuwa nikisuluhisha ndoa za watu wengi zenye machafuko, zenye shida, na baada ya hayo yote, nikasukumwa kuwa niandike ujumbe huu, ili uwasaidie wale ambao tayari wamekwisha kuoana, na wale ambao wataoana.[/FONT]

  [FONT=&amp]Efeso 5:33 "Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe, na mke asikose kumstahi mumewe"[/FONT] [FONT=&amp]Mpendwa, hebu tuendelee kujifunza kutoka kwenye Neno la Mungu. Wajibu wa MUME ni kumpenda mke wake kama nafsi yake. Suala hili ni gumu; ni agizo gumu, lakini aliyetuagiza anajua kuwa wanaume wataweza kumpenda mke KAMA mtu apendavyo nafsi yake. Mtu anapojikwaa mguu, kwa kuwa anaupenda mguu wake, haupigi, wala haukati, anaupuliza, anaushughulikia kama umeumia, hawezi kuuliza kuwa ‘ulikuwa unatembeaje mpaka ukajikwaa?'. Na MKE ameambiwa asikose KUMSTAHI mumewe. KUMSTAHI ni KUMHESHIMU MUMEWE. Kumheshimu kwa njia gani?[/FONT]

  [FONT=&amp]Efeso 5:22 "Enyi wake watiini waume zenu, kama kumtii Bwana wetu, kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha kanisa, naye ni mwokozi wa mwili. Lakini kama vile kanisa limtiivyo Kristo, viyo hivyuo nao wawatii waume zao katika kila jambo"[/FONT]

  [FONT=&amp]Naomba twende pole pole tukijifunza, ili ndoa zipone maana nyingi zimeoza, hazifai. Wamama wameambiwa wawatii waume kama kumtii Kristo. Hapo napo huwa kuna matatizo, maadam wote wameokoka, basi wanajihesabu kuwa wako sawa. Hapana! Soma vizuri: MUME NI KICHWA. Sasa kama mume ni kichwa, ndiye anatakiwa kuongoza nyumba, kwa kuwa kichwani kuna- MACHO, MASIKIO, UBONGO, MDOMO, n.k[/FONT]

  [FONT=&amp]Nazungumzia mambo ya rohoni: wamama wengi wamebomoa nyumba zao kwa mikono yao, pale walipojaribu kuongoza, wakidhani wanaweza. Kumbuka neno hili kuwa Adamu aliishi bila Hawa lakini Hawa hakuwahi kuishi bila Adamu. Hawa alipoishi bila Adamu kwa dakika chache tu aliondoka akakutana na nyoka, wakati Adam hayupo pamoja naye, akajitahidi kuzungumza na nyoka akijibu maswali aliyokuwa anaulizwa, lakini hakufua dafu![/FONT]

  [FONT=&amp]1Tim 2:13-14 "Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye. Wala Adamu hakudangaywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa, akaingia katika hali ya kukosa"[/FONT] [FONT=&amp]Biblia inaeleza wazi wazi kuwa Adam hakudanganywa. Aliyedanganywa ni Hawa. Sasa tuendelee kujiuliza: kama Adam hakudanganywa, ilikuwaje Ale tunda? Je, Alilazimishwa?; Kwa nini alikula?[/FONT] [FONT=&amp]

  Nilipokuwa natafakari mambo haya niliyaona kwa ndani zaidi. Utakumbuka wakati Bwana alipokuja ili akutane nao Bustanini, hakuwakuta, akamwita Adam na kumuuliza alikokuwa! Adamu akasema "nimejificha, kwa kuwa niko uchi"; akamuuliza "nani amekwambia kuwa uko uchi?" [au umekula tunda nililokukataza?] Adamu akasema "Mwanamke uliyenipa ndiye amenipa tunda nikala".[/FONT]
  [FONT=&amp]

  Sasa ona hapa, Je, Hawa alimlazimisha? Kwa nini alikula? Watu wengi wanasema kuwa Adam aliposema kuwa ni huyo mwanamke uliyenipa, alikuwa anamlaumu Mungu kwa kumpatia mwanamke. Hapana! Hebu leo nikuonyeshe kitu hapo: Biblia inasema "Apataye mke apata kitu chema, tena hujipatia kibali kwa Bwana"[/FONT]
  [FONT=&amp]

  Sasa Adam alipojibu kuwa "ni huyo mwanamke uliyenipa" alikuwa akisema hivi: "Huyu mwanamke uliyenipa, najua hukunipa kitu kibaya, ulinipa kitu chema kabisa, na mimi kama mimi hajanikosema, amekukosea wewe. Na kawa kuwa wewe Mungu wangu ulinipa kitu chema basi sitakiacha, nitaongozana nacho kokote kitakakokwenda, sitakiacha. Wewe Mungu una uwezo, kwanza unajua kuwa ni chombo dhaifu, wewe ungeweza kukizuia kabisa kisile tunda lakini ukakiacha kikala, basi nakufa nacho!".[/FONT]
  [FONT=&amp]

  Alipomaliza kusema hayo akalipokea tunda kwa hiari yake, akala na akajua sasa hawawezi kumuona Mungu wakiwa na hali hiyo; wakakubaliana waondoke shambani.[/FONT]
  [FONT=&amp]Sababu nyingine iliyofanya ale ni kuwa alijua kuwa yeye Adam aliishi bila Hawa na wala hakuomba Mungu ampe mke, ni Mungu tu alisema "si vema sasa uwe peke yako nitakufanyia msaidizi", na akamfanyia wa kufanana naye, yaani alimfanyia mwili wake, sasa mwili wako utaukataje uutupe? Akajua kuwa UBAVU wenyewe hauwezi kuishi bila kichwa, ndio maana alisema basi nitaendelea kuwa na ubavu huu.[/FONT]

  [FONT=&amp]Ruth 1:16-17 "Naye Ruth akasema, usinisihi nikuache, nirejee nawe, maana wewe uendako nitakwenda, nawe ukaapo nitakaam watu wako watakuwa watu wangu, pale utakapokufa nitakufa nami, na papo hapo nitazikwa. Bwana anitende hivyo na kuzidi, ila kufa kutatutenga wewe na mimi"[/FONT]

  [FONT=&amp]Huyo ni Ruth alipokuwa anamwambia mama mkwe wake, wakati amemsihi aondoke kama Olpa alivyofanya. Ndugu zangu nazungumza habari za KUACHANA, siku tulizonazo, limekuwa ni tatizo kubwa katika maisha ya wana ndoa wengi, wengine maombi yao yamekwama hayajibiwi kwa sababu ya ndoa zao.[/FONT]

  [FONT=&amp]1Pt 3:7 "Kadhalika nanyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili, na kumpa mke heshima, kama chombo ksicho na nguvu, na kama warithi pamoja na neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe"[/FONT]

  [FONT=&amp]Neno linasema wazi wazi kuwa mume ukae na mke wako kwa akili. Unaona hiyo? Kukaa na mke inatakiwa akili itumike. Je, Ni akili ya namna gani? : Kuwa ni chombo kisicho na nguvu, japo wakati mwingine wanajitutumua kana kwamba wana nguvu, lakini Biblia inabaki pale pale kuwa ni chombo kisicho na nguvu, ya kwamba mume umpe mke Heshima. Kumpa heshima ni kufanyaje?[/FONT]

  [FONT=&amp]Hayo yote tuyaangalie vizuri maana ndiyo yanayoleta matatizo iwapo mmoja atashindwa kutimiza wajibu wake. Unajua kama madereva wote wangefuata sheria za barabarani, nakwambia hakungekuwa kunatokea ajali barabarani, pale pa "keep left", mwendo gani unatakiwa hapo, wakati gani umpite mwezako aliye mbele, wakati gani usimame n.k![/FONT]

  [FONT=&amp]1 Pt 3:1-6 "Kadhalika nanyi wake watiini waume zenu, kusudi, ikiwa wako wasioliamini Nneo, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile neno. Wakiutazama mwenendo wenu safi na wa hofu. Kujipamba kwenu kusiwe kujipamba kwa nje, yaani kusuka nywele, na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi, bali uwe utu wamoyoni, usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika, yaani roho ya upole, na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumikia Mungu, na kuwatii waume zao,kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana. Nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yoyote"[/FONT]

  [FONT=&amp]Soma kwa makini hayo yote hapo juu, utaelewa. Je, wewe mama unamwitaje mumeo?[/FONT]

  [FONT=&amp]Unajipambaje? Wengi wamesoma wakaelewa vibaya kuwa Biblia imetukataza kujipamba, hapana. Inakueleza jinsi unatakiwa kujipamba, usidhani ukiisha vaa nguo nzuri, ukasuka nywele zako, ufikiri kuwa hapo umemaliza; hapana. Kumbuka Bwana anaangalia MOYO, na jambo hili Yesu aliliweka hivi:[/FONT]

  [FONT=&amp]Math 23:27-28 "Ole wenu waandishi na mafarisayo wanafiki, kwa kuwa mmefanana na makaburi, yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote. Vivyo hivi ninyi kwa nje mwaonekana na watukuwa wenbye haki bali ndani mmejaa unafiki na maasi."

  [/FONT]
  [FONT=&amp]Unaona alichosema Bwana Yesu hapa? Wala hakusema makaburi yasipakwe chokaa, hapana! Kama ambavyo hakusema watu wasivae mavazi mazuri, ila pamoja na kuvaa, tuelewe kuwa kuna cha zaidi ya kuvaa: mioyo ni muhimu kuliko kuvaa! Hapo inabidi tuelewe vizuri, maana wapo watu wanasema kuwa Biblia inasema haturuhusiwi kuvaa mavazi ya thamani. Hapana hiyo siyo maana yake!Mtu akikwambia kuwa uanajeshi wako usiwe wa kuvaa buti, hapo hajasema usivae buti, ila anasema ukiisha vaa buti, usije ukadhani umemaliza, kuna zaidi ya hapo![/FONT]

  [FONT=&amp]Biblia inasema kuwa katika siku za mwisho watu watakuwa na tabia fulani, ambapo mimi nimechagua mambo matatu ambayo hayo ni mabaya mno! Hebu jipime:[/FONT]
  [FONT=&amp]1.Wenye kuvunja maagano.[/FONT]

  [FONT=&amp]2.Wasiotaka kufanya suluhu.[/FONT]

  [FONT=&amp]3.Wasio na shukurani.[/FONT]

  [FONT=&amp]Tafakari hayo mambo hapo juu. Mtume Paulo aliona siku za mwisho kuwa watu watakuwa wanavunja maagano. Katika kuoana huwa kuna maagano, wengine wanavalishana pete, wanasema maneno mbele za Mungu na mbele za watu, vigelegele vinapigwa, Neno linasomwa na watumishi wa Mungu.! Lakini baada ya siku si nyingi, hayo maagano yanavunjika; unasikia ndoa hiyo imekwisha wala haipo tena! Ni wengi wamevunja, na tayari wameshaoa tena. Lakini wanasema bado wanasonga kuelekea Mbinguni! Hivi ni kweli kuna kuelekea mbinguni hapo? Endelea kutafakari![/FONT] [FONT=&amp]

  Wengine hawataki kabisa kufanya suluhu. Biblia imesema kuwa "Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu." Wapo wana wa Mungu, wazuri kabisa katika kuwapatanisha wapendwa wanapokoseana. Lakini kwa sababu siku za mwisho watu hawatakubali kufanya suluhu, basi hakuna kinachofanyika isipokuwa kuachana tu. Endelea kutafakari![/FONT]


  [FONT=&amp]Watakuwepo watu watakaovaliwa na roho ya kukosa shukurani. Hivi kweli, mkeo/mumeo ambaye mmekaa naye miaka kadhaa unayoijua wewe; Hakuna hata jambo moja tu ambalo aliwahi kukufanyia zuri? Ukilikumbuka hilo, naamini kuwa litageuza hasira yako na utaumba roho ya kushukuru, na mwisho msamaha utaumbika na utamsamehe, na utajikuta mnasameheana.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kol 3:12 "Bsi kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana na kusahemeana; mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake, kama Bwana alivyowasamehe ninyi; vivyo nanyi"[/FONT] [FONT=&amp]

  Napenda nimalizie kwa kusema kuwa Mungu atusaidie: ndoa ziponywe; talaka zisitajwe kwetu kamwe; vinginevyo tunaelekea kwa wenzetu wan chi zilizoendelea hasa za Ulaya na Marekani ambao wanaoana kwa mkataba, ukiisha wanaongeza. Hiyo siyo Biblia.[/FONT]
  [FONT=&amp]Nawatakia kila la kheri katika ndoa zenu. Amina![/FONT]

  [FONT=&amp]Mchungaji Samnuel Imori.[/FONT]
  Source: Strictly gospel
   
 2. s

  shalis JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni ushari mzuri na maneno ya ki mungu, ni vizuri kukaa mikononi mwa bwana.
   
 3. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Hapo sitii neno mwenye masikio na asikin, mwenye macho na ameona
   
 4. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #4
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Nimejifunza kitu hapa
   
 5. m

  msafi Senior Member

  #5
  Oct 29, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  thanks a lot, wanandoa wakiwa na Mungu katika maisha yao, hakutakuwa na talaka maana wote watakuwa na hofu ya Mungu, na kila mwenza atachukuliana na mwenzake. Binafsi tunapishanaga sana tu na mke wangu lakini tunasameana na kuendelea mbele, na tunauona utukufu wa Mungu katika maisha yetu. Wanandoa kutalakiana ni kwa sababu Mungu hayupo ndani yao na hivyo kuvumiliana na kuchukuliana inakuwa ngumu. Mume akimpenda mke wake kama nafsi yake, automatically mke atamheshimu na kumtii mume wake kwa kila jambo, lakini inakuwa ngumu mwanamke kumtii mume katika upendo kama mume hampendi. Wanaume tunasehemu kubwa sana ya kuwafanya hawa viumbe watutii katika upendo.
   
 6. M

  Mangolo Member

  #6
  Oct 30, 2011
  Joined: Oct 30, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  baba mchungaji nimefarijika mno,tatizo kubwa kwa ndoa siku hizi ni ule msingi.
  hazina msingi imara hivyo tetemeko kidogo tu inabomoka moja kwa moja
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Oct 30, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Ndiyo maana siachani na mwenzi wangu, lakini kuzini na zini kweli, hilo hata Mungu anajua kuwa mie mdhaifu hapo!
   
Loading...