Kuacha kazi kwa notice ya siku 28

Posho City

JF-Expert Member
Mar 15, 2012
648
418
Wakuu za leo,

Katika utumishi kuna utaratibu wa kuacha kazi kwa kumpa mwajiri taarifa ya siku 28 au mwezi mmoja.

Swali langu je katika huo mwezi wa notice mwajiri anakulipa mshahara au unafanya kazi bila malipo?

Ahsanteni.
 
Ukitoa notisi ya 28 unapokea mshahara kama kawaida mpaka siku yako ya mwisho kufanya kazi.

Unaweza pia kutoa notisi ya masaa 24 ambapo wewe unayeacha kazi utatakiwa kumlipa mwajir mshahara wako wa mwezi mmoja.
Na kuna athari gani kuacha kazi bila kutoa notisi
 
Ukitoa notisi ya 28 unapokea mshahara kama kawaida mpaka siku yako ya mwisho kufanya kazi.

Unaweza pia kutoa notisi ya masaa 24 ambapo wewe unayeacha kazi utatakiwa kumlipa mwajir mshahara wako wa mwezi mmoja.
Na huo mshahara wa kumlipa mwajiri wako unaulipa mapema na risiti ya kulipa mshahara huo lazima uiambatanishe kwenye barua yako unayoomba kuacha kazi/notisi ya masaa 24. Vinginevyo hilo ombi lako la kuacha kazi halitakubaliwa kwa sababu litakuwa halijakidhi vigezo.

Kwa maana nyingine ni kwamba wewe unaeacha kazi unatakiwa kumlipa mwajiri wako huo mshahara wa mwezi mmoja ambao unatakiwa uwe ni basic salary (usidhani ni ile net salary!) na kuambatanisha kwenye notisi yako bila kujali kwamba mshahara wako wa mwezi huo umeshalipwa kwako au la.

Kama wakati unapeleka notisi yako ya kuacha kazi wewe ulikuwa haujalipwa basi huo mshahara wako utafuatia baadae katika tarehe za kawaida za ulipaji wa mishahara.
 
Athari za kuacha kazi bila notisi ni zipi.
 
Mwajiri hatokupa barua ya kukubali wewe kuacha kazi. Utakwama kwenye kudai mafao kwenye mifuko ya hifadhi mf. Ppf, nssf, pspf nk
Ni kweli mkuu. Mbali na financial benefits kama hizo kuna mengine ambayo ni ya kimahusiano zaidi 1.Ukiomba kazi sehemu nyingine na huko wakahitaji reference kutoka kwao kuhusu utendaji wako wa kazi itakuletea shida kwa sababu hautapata recommendation nzuri. 2. Siku moja huko mbeleni unaweza kuhitaji kurudi kufanya nao kazi tena. Hapo utakwama kwa sababu haukuondoka kwa ustaarabu 3. Kuna uwezekano mtu wa HR uliyemwacha pale bila kumuaga ukamkuta katika taasisi nyingine ambako umeomba kazi na kuitwa kwenye interview. Sasa kutokana na tabia yako uliyoonyesha ya kuacha kazi bila kuaga, kuna uwezekano mkubwa nae akachangia kukuangusha kwenye interview hiyo.

Kwa ujumla ni jambo la kistaarabu kuondoka kistaarabu kwa kuaga. Pia uepuke maneno ya dharau kuhusu mahali hapo ulipokuwa na pia kujivuna au kujivunia waziwazi kazi yako mpya na taasisi nyingine unakoenda. Kuna methali isemayo usiwatukane wakunga na uzazi ungalipo.
 
Ufafanuzi mzuri, naona hapa kama ume-base kwenye private sectors mkuu, vipi kuhusu serikalini.?
 
Kwa kadri ninavyoelewa hata serikalini hali ni hiyo hiyo. Jaribu kuangalia pointi moja moja hapo juu na utaona kuwa hata serikalini athari za kutoaga ni hizo hizo.
 
Nitachukulia kama mtoro kazini, nitakutafuta popote ulipo!
Hivi nimeacha kazi yangu kwa hiari yangu utanilazimisha vip kufanya kazi yako.Sidhani kama sheria ipo hivyo,ila ukinitafuta utakuwa umetumia gharama kubwa.
 
Kwa kawaida mikataba mingi ya kazi ina kipengere cha KUKABIDHI (HANDOVER)! makabidhiano muhimu kaka!
 
Mwajiri hatokupa barua ya kukubali wewe kuacha kazi. Utakwama kwenye kudai mafao kwenye mifuko ya hifadhi mf. Ppf, nssf, pspf nk

ukiwa na laki mbili au tatu mkononi njoo nkupeleke upewe mafao yako bila kua na fomu za mwajiri wala nini
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom