Ku Jail-break iPhone 6 Plus

Ku Jail-break iPhone 6 Plus

captain dunga

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2014
Posts
282
Reaction score
636
habarini wadau..

Wiki mbili zimepita niliomba msaada wa ushauri ninunuie simu gani kati ya GalaxyNote4 na iphone 6 plus...

Wengi mkaniambia iphone6 plus,alafu Chief-Mkwawa akanambia kama nataka simu ambayo badae nitaiuza nichukue 6plus coz haishuki thamani,hvo mwisho wa siku nikachukua 6plus..

Nimeipenda muonekano wake na smoothness yake,tatzo ni limitation za ajabu ajabu ambazo haizna maana..

Hivyo nimeomba nielezwe namna ya kui jail break bila kusababisha matatizo ili niondoe hizi limits za kishamba...

Natanguliza shukrani..

Note::Wapenzi wa Android msijaribu kununua apple devices mtajuta..
 
Last edited by a moderator:
Usijaribu ata kidogo....jailbreak ya iPhone 6 bado haiko stable .u will most likely end up in bootloops.
 
Ndo maana mimi siikubali iphone sababu ya vikwazo vyao vya kijinga. Unakuwa na simu harafu hufurahii. Hata 3G only haikai inahama hama tu
 
hizo limitations unazoongelea wewe hasa ni zipi??

Umejibu kwa kujiamini mkuu,inaonesha unatumia iphone..
Kama hujaona limitations anza kuwa na wasiwasi na akili zako we mwenyewe..
 
Umejibu kwa kujiamini mkuu,inaonesha unatumia iphone..
Kama hujaona limitations anza kuwa na wasiwasi na akili zako we mwenyewe..

Acha kujudge mapema, nimeuliza swali jepesi tu, limitations ni zipi? zitaje labda kuna alternative tunaweza kupa, wewe usharukia kutoa majibu yasiyo na msingi... Akili zangu we unazijua?
 
Wewe jamaa inaelekea bado hujaielewa vizuri iPhone. Mimi nimetumia aina tofauti za iPhone kwa mwaka wa 3 sasa na sijaona tatizo lake. Ili upate service nyingi za iPhone lazima uwe umejisajili kwanza. Ili upate Apple ID. Then utapata apps nyingi bure. Na ni rahisi sana kumkamata mwizi wa simu yako kama ikiibwa maana huwezi ku temper nayo kirais.
 
Umejibu kwa kujiamini mkuu,inaonesha unatumia iphone..
Kama hujaona limitations anza kuwa na wasiwasi na akili zako we mwenyewe..

Mkuu umeulizwa swali la msingi sana
Nakumbuka post yako ya juzi kati kuomba ushauri ununue ipi, binafsi nilikushauri iphone lakini ujiandae na ukiritimba kidogo ambo ahuwezi kuathiri sana matumizi ya simu yako

Nadhani ni mapema mno kuanza kujailbrake simu yako, vuta subira uijue vizuri iphone yako,
Labda ungetaja ni jambo gani linakukera sana ambalo wadau wanaweza kukupa mbadala wakati unaendelea kuisoma iphone yako
 
Ndo maana mimi siikubali iphone sababu ya vikwazo vyao vya kijinga. Unakuwa na simu harafu hufurahii. Hata 3G only haikai inahama hama tu

Furahia ni neno subjective sana. Kuna wanaoipenda iphone kuliko unavyoipenda android device.
Binafsi, hakuna simu kama iphone.
Nimewashawishi home kila mmoja anatumia iphone and they can tell a difference with their andoid devices.

Galaxy Note series au Google Nexus series ndo simu pekee ninaweza kuziangalia mara mbilimbili zaidi ya hapo hizo nyingine ni takataka.
Jailbreaking ni curiocity na sio standard formula ya kutumia simu.
 
Apple: Has majority of priced apps,closed operating system(programu zake huandikwa na wahandisi wa kampuni yao tu),less customizable,less user friendly OS(Ni rahisi kwa waliowahi kutumia tu),Less product substitutes(zipo chache km iphone 3,4,5,6 na zote znatumia programu sawa),high cost of their products due to high quality hardware and overall perfomance...

Google Android: Majority of free apps, Open operating system(kila mwenye uwezo wa kuandika programu anaweza kutengeneza hivyo wahandisi ni watu binafsi na wenye kampuni za simu), Very user friendly OS,Majority of substitutes products(zipo za kimaskini km itel,tecno,huawei na za kitajiri kama Samsung,Sony,Htc), Less cost of their products(low end products) due to majority of substitutes.

Pimeni then mtajua product ipi ni bora kwa matumizi.
 
Acha kujudge mapema, nimeuliza swali jepesi tu, limitations ni zipi? zitaje labda kuna alternative tunaweza kupa, wewe usharukia kutoa majibu yasiyo na msingi... Akili zangu we unazijua?

Umeandika. 'hizo limitations unazoongelea wewe hasa ni zipi??'

Unless sijui vizuri kiswahili..
 
Watu hutofautiana, mimi nimetumia nokia symbian, android phones, windows phone na iphones. Nimerud tu kwenye iphones... Inategemea na mtu anapenda nini. Ila mm napenda iphones.
 
Limitations zipo na nazielewa kwa mfano kutokudownload nyimbo na videos straight from safari. Nyimbo za whatsapp huzioni kwenye my music kama ilivyo kwa simu nyingne pamoja na kutumiana files kwa bluetooth.
Ila kama ni applications zile basic ambazo wengi huzitumia mfano whatsapp, twitter, livescore, jf, insta, news apps unapata tu bila shida ni free kama kwa simu nyingne. Inategemea na mtu anachokitaka na matumizi yake.
 
Apple: Has majority of priced apps,closed operating system(programu zake huandikwa na wahandisi wa kampuni yao tu),less customizable,less user friendly OS(Ni rahisi kwa waliowahi kutumia tu),Less product substitutes(zipo chache km iphone 3,4,5,6 na zote znatumia programu sawa),high cost of their products due to high quality hardware and overall perfomance...

Google Android: Majority of free apps, Open operating system(kila mwenye uwezo wa kuandika programu anaweza kutengeneza hivyo wahandisi ni watu binafsi na wenye kampuni za simu), Very user friendly OS,Majority of substitutes products(zipo za kimaskini km itel,tecno,huawei na za kitajiri kama Samsung,Sony,Htc), Less cost of their products(low end products) due to majority of substitutes.

Pimeni then mtajua product ipi ni bora kwa matumizi.

Sikubaliani na wewe kwamba Apps za Apple zinaandikwa na Apple wenyewe tu, hata wewe unaweza kuandika na ukazipeleka, tatizo ni viwango
Apple hawapokei tu li App lolote utakalo wapelekea ilimradi linaweza kuwa installed kwenye ios kama wanavyopokea Android,,,,,,, its standard and classic that is matter

Sio kweli kwamba ios sio user friendly, kama umezoea android ukihamia ios lazima utaiona sio user friendly wakati hujaizoea kama ilivyo kwa mtumiaji wa ios atakavyoiona android sio user friendly kwakuwa hajaizoea

Karibu Apps nyingi zile must have zinapatikana bure pia ios, sema watu wamekariri apps za apple nyingi za kununua kitu ambacho sio kweli

Mengine naweza kukubaliana na wewe lakini kaa utambue hizo sijui iphone za chini sio substitutes kama ulivyoziita, hizo ndio zilikua simu za juu wakati wake na hazikutolewa kama sub
Apple wanatengeneza only High-end phones
 
Nimetumia Symbian OS under Nokia, Android under HTC na sasa iOS under iPhone 5s, hakika sijutii kutumia iPhone hata kidogo, na sina hata mpango wa kujailbreak iPhone 5S yangu kwa sababu inanitosheleza mahitaji yangu. Kwa ushauri tu kama umezoea kutumia Android ni vyema kabla hujahamia iOS ni bora ukajua ni kwa nini unataka kuhamia. Kwangu mimi najali sana security kuliko kitu kingine
 
Apple: Has majority of priced apps,closed operating system(programu zake huandikwa na wahandisi wa kampuni yao tu),less customizable,less user friendly OS(Ni rahisi kwa waliowahi kutumia tu),Less product substitutes(zipo chache km iphone 3,4,5,6 na zote znatumia programu sawa),high cost of their products due to high quality hardware and overall perfomance...

iOS ni closed OS, lakini hiyo haimaanishi software zake huandikwa na apple wenyewe, only the Operating System part inaandikwa na wao, apps nyingine zote huandikwa na mtu yeyote yule, wapo very selective kwenye apps na ndo kitu kinawafanya wana high quality apps ukicompare na android, Apple wanaweza chukua wiki 2~4 kuiweka app yako kwenye app store sababu ya ukaguzi mwingi japo android ni masaa mawili tu.
 
Mkuu umeulizwa swali la msingi sana
Nakumbuka post yako ya juzi kati kuomba ushauri ununue ipi, binafsi nilikushauri iphone lakini ujiandae na ukiritimba kidogo ambo ahuwezi kuathiri sana matumizi ya simu yako

Nadhani ni mapema mno kuanza kujailbrake simu yako, vuta subira uijue vizuri iphone yako,
Labda ungetaja ni jambo gani linakukera sana ambalo wadau wanaweza kukupa mbadala wakati unaendelea kuisoma iphone yako

Kudownload miziki au chochote kupitia safari au any browser..

Kutuma files kupitia email..

Ku download video za youtube..

Bluetooth sharing..

Niki download miziki through i downloader iende kwenye music moja kwa moja,na pia idownloader hai pakui miziki from mkito..

Kutumia simu yangu kama kifaa cha kuhamishia files..

Kuingiza files kutoka kwenye pc bila kutumia itunes(huu ni upuuzi ambao sijaona 7bu ya aple kuuweka)...

Kubadili fonts..

Kufunga app flani kwa password..

Haikubali ku download vitu zaid ya mb100 kwa mobile data..(kituko hiki,au na hii wanaifanya kwasababu za kibiashara na kama ndio,biashara gani hiyo.?)

Delivery report,video call bila wifi..
 
Back
Top Bottom