Kimaumbile huna tatizo lolote ila hiyo ni dalili kwamba hujafanya ngono kwa muda mrefu, hiyo ni hali inayoweza kumtokea mwanaume yeyote ambaye hajafanya ngono kwa muda mrefu.
Kwa kawaida mwanaume yeyote aliye na afya njema, anakula vizuri, asiyeumwa na ni mkamilifu, huwa anatengeneza/anazalisha shahawa kila siku na shahawa kwa kuwa zinazaliswha lazima zitoke. Kuna njia mbalimbali za shahawa kutoka mwilini, kuna zile njia za asili kimaumbile (natural) nazo ni 1) kufanya ngono, 2) kuota ndotoni na hiyo ya 3) shahawa kutoka zenyewe wakati unajisaidia haja kubwa. Ile isiyo ya asili kimaumbile ni ya kujichua au wengine wanaiita kupiga punyeto.