Ndugu Makorogosi,
Watanzania hatulazimiki kuishi ili tukalitumikie KATIBA, ila KATIBA ni orodha ya ndoto zetu, matumaini na matamani yetu katika maisha ya kila siku ambayo imepata baraka za wengi na kurasmiswa katika ki-jijalada ili ITUTUMIKIE ipasavyo!!
Pindi katiba inapoanza kuonekana kubaki nyuma ya wakati, na kuanza kukidhi maslahi ya kipindi cha nyuma tu na tena kwa maslahi ya wachache, hapo ndipo raia sote tunalazimika KUFANYA HARAKATI za Makusudi kabisa na BILA UNAFIKI kukibadilisha ili iweze KUKIDHI MAHITAJI YETU HALISI YA SASA na ya KIPINDI Kijacho!!
Hapo ndipo watu tunapoanza kukosea kuhusu mambo mazito na ya msingi kama ambavyo VIJANA tumeanza kulizungumzia sauala la KATIBA MPYA humu. Katiba sio mali ya Viongozi, ni mali yetu sisi VIJANA na ni sisi tunaovaa viatu ndio tunajua fika ni wapi hasa tunapominya pumsi tubadilishe haraka. Upatikanaji wa katiba mpya sio suala la AKINA WALE (wakiwemo Waheshimiwa wabunge wa Chama Changu cha CHADEMA). Katiba inatuhusu sote; wewe, mimi na yule kwa pamoja.
Isitoshe, katiba ni MKATABA kati ya Watawala na Watawaliwa. Mle ndani, Watawaliwa (Mie, wewe na yule) tunatoa mwelekeo kwa Watawala jinsi gani tungependa watutawale KWA MASLAHI NA MAENDELEO YETU kwa sehemu kubwa sana Kitaifa. Ukifanikiwa kuelewa hili basi na ukawaeleweshe na wengine 10 zaidi toka sasa, na elimu juu ya katiba na haki yetu juu yake itaenea kila kona ya nchi yetu hii.