Ktiba mpya ya jamuhuri ya muungano tza


M

makongorosi

Member
Joined
Apr 24, 2009
Messages
49
Likes
0
Points
0
M

makongorosi

Member
Joined Apr 24, 2009
49 0 0
Nikiwa mfuasi wa chama cha upinzani, nimefurahi kupata viti vingi vya ubunge uchaguzi wa mwaka huu. Pamoja na uwingi huo wa wabunge wa upinzani ukiringanisha na ccm bado wanatuzidi sana, maana nimeshuudia wapenzi wengi wa mageuzi wakisema bunge la mwaka huu litachimbika sasa kwa maandalizi ya kushinda 2015 lazima tuwe na katiba mpya itakayoleta tume huru, sasa hawa wabunge wetu wa upinzani ambao ni vijana watahimili vipi ktk kupatikana katiba mpya maana ccm wanatuzidi kwa mbali, hata ikitolewa hoja ya katiba mpya bado tutapwaya, sasa swali kwa wana jamii nini kifanyike ili kuweza kufanikisha hiyo ndoto ya katiba mpya? je hakuna njia nyingine ya kudai katiba mpya nje ya bunge kama vile mahakamani? maana kwa kupigiwa kura ndani ya bunge ili kupata katiba mpya ndiyo yatakuja yaleyale ya Mabere marando na Anna Makinda.
 
U

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2010
Messages
6,947
Likes
13
Points
0
U

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2010
6,947 13 0
Ndugu Makorogosi,

Watanzania hatulazimiki kuishi ili tukalitumikie KATIBA, ila KATIBA ni orodha ya ndoto zetu, matumaini na matamani yetu katika maisha ya kila siku ambayo imepata baraka za wengi na kurasmiswa katika ki-jijalada ili ITUTUMIKIE ipasavyo!!

Pindi katiba inapoanza kuonekana kubaki nyuma ya wakati, na kuanza kukidhi maslahi ya kipindi cha nyuma tu na tena kwa maslahi ya wachache, hapo ndipo raia sote tunalazimika KUFANYA HARAKATI za Makusudi kabisa na BILA UNAFIKI kukibadilisha ili iweze KUKIDHI MAHITAJI YETU HALISI YA SASA na ya KIPINDI Kijacho!!

Hapo ndipo watu tunapoanza kukosea kuhusu mambo mazito na ya msingi kama ambavyo VIJANA tumeanza kulizungumzia sauala la KATIBA MPYA humu. Katiba sio mali ya Viongozi, ni mali yetu sisi VIJANA na ni sisi tunaovaa viatu ndio tunajua fika ni wapi hasa tunapominya pumsi tubadilishe haraka. Upatikanaji wa katiba mpya sio suala la AKINA WALE (wakiwemo Waheshimiwa wabunge wa Chama Changu cha CHADEMA). Katiba inatuhusu sote; wewe, mimi na yule kwa pamoja.

Isitoshe, katiba ni MKATABA kati ya Watawala na Watawaliwa. Mle ndani, Watawaliwa (Mie, wewe na yule) tunatoa mwelekeo kwa Watawala jinsi gani tungependa watutawale KWA MASLAHI NA MAENDELEO YETU kwa sehemu kubwa sana Kitaifa. Ukifanikiwa kuelewa hili basi na ukawaeleweshe na wengine 10 zaidi toka sasa, na elimu juu ya katiba na haki yetu juu yake itaenea kila kona ya nchi yetu hii.
 
L

Lorah

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2008
Messages
1,193
Likes
5
Points
0
L

Lorah

JF-Expert Member
Joined Aug 22, 2008
1,193 5 0
waambieni tuanze tupitishe kura ya Maoni bwana Tunaotaka Katiba Dafu na wasiotaka Pera tuone mambo yatakuwaje Kama kweli CCM inakubalika, hawajaiba kura, hawakucheza rafu watuonyeshe kwa Kuthubutu basi....:bowl:
 
M

matarimo

Member
Joined
Nov 2, 2010
Messages
5
Likes
0
Points
0
M

matarimo

Member
Joined Nov 2, 2010
5 0 0
nI KWELI MIMI BINAFSI NAKUBAILIANA NA WEWE, WANANCHI TUKIWA NA MWAAMKO WA KUDAI KATIBA MPYA, HILO LITAWEZEKANA. BILA KATIBA MPYA , ITAKUWA VIGUMU KUIBADILISHA NCHI YETU.
 
C.K

C.K

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2010
Messages
389
Likes
37
Points
45
C.K

C.K

JF-Expert Member
Joined Nov 5, 2010
389 37 45
Asante sana my people wenye mawazo ya kutaka katiba mpya. Kwa sasa hili ndilo suala muhimu zaidi ya kitu kingine . Tunahitaji mabadiliko ya katiba yetu ili kutoa mwanya kwa umma kuchagua kile wanachokitaka kwa wakati husika. Kwa katiba ya sasa hilo haliwezekani kwani NEC inaundwa na utawala wa CCM, unategemea nini hapo!

Let's demand for new const........ keep pressing till hapen!
 

Forum statistics

Threads 1,235,920
Members 474,863
Posts 29,240,583