makongorosi
Member
- Apr 24, 2009
- 49
- 3
Nikiwa mfuasi wa chama cha upinzani, nimefurahi kupata viti vingi vya ubunge uchaguzi wa mwaka huu. Pamoja na uwingi huo wa wabunge wa upinzani ukiringanisha na ccm bado wanatuzidi sana, maana nimeshuudia wapenzi wengi wa mageuzi wakisema bunge la mwaka huu litachimbika sasa kwa maandalizi ya kushinda 2015 lazima tuwe na katiba mpya itakayoleta tume huru, sasa hawa wabunge wetu wa upinzani ambao ni vijana watahimili vipi ktk kupatikana katiba mpya maana ccm wanatuzidi kwa mbali, hata ikitolewa hoja ya katiba mpya bado tutapwaya, sasa swali kwa wana jamii nini kifanyike ili kuweza kufanikisha hiyo ndoto ya katiba mpya? je hakuna njia nyingine ya kudai katiba mpya nje ya bunge kama vile mahakamani? maana kwa kupigiwa kura ndani ya bunge ili kupata katiba mpya ndiyo yatakuja yaleyale ya Mabere marando na Anna Makinda.