Lakini wakati ukifika..... NITAICHOMA DUNIA YOTE.
Jana ilikua siku takatifu ya muhimu sana kwa wakristo wote Duniani. Tulikua tunaadhimisha kuzaliwa kwa bwana wetu YESU KRISTO. Masia wetu. Ilikua Krismas.
Ukitaja krismas hakuna asieijua siku hii. Nakumbuka kijijini kwetu Shilabela ni siku ambayo bila kujali dini ndugu wote huchinja na ni siku ya kula vinono.
Duniani kote ni siku ya kufanya Ibada na kutafakari zawadi hii kubwa kutoka kwa Mungu wetu. Kwamba alimleta mwanae wa pekee ili tupate KUPONA.
Imekua ikihubiriwa na watumishi wa Mungu mara nyingi kwamba krismas sio siku ya kutenda dhambi au kufanya mambo ya ajabu kwa kisingizio eti tunasheherekea. Neno moja wapo ni ule msitari maarufu kwenye kitabu cha Mhubiri. "Ana faida gani mtu na lile ajishughulishalo nalo?"
Nikiwa na familia yangu jana tulikua tunaelekea mahali kupumzika nilishuhudia mambo ambayo mpaka sasa nawaza Dunia inaelekea wapi?
Niliona makundi ya vijana wanaojiita kempu wamekodi magari yanaendeshwa kwa fujo kuelekea beach. Kilichoendelea huko sijui lakini naamini si mambo mema maana ndani ya magari tu penyewe hali haikua shwari.
Kibaya kuliko vyote ni kwamba kulikua na magari yamejaa vijana wa jinsia zote. Walikua wanapiga ngoma na wengine wakicheza "matusi". Kama hiyo haitoshi watoto wa kike walikua uchi wa mnyama. NA wengine walikua wanabinua viuno vyao nje ya dirisha la gari. Imagine uko na mwanao na mtu anaanika vitu vyake hadharani. Eti anasheherekea kuzaliwa kwa bwana. This is tooo much.! Mtu anakata kiuno uchi kwenye dirisha la gari ili watu waone uchi wake. Lol sielewielewi! 😬😬😬Nikasikia watu wanasifia "chezea wazaramo wewe"
Achilia mbali waliofanya uzinzi, ulevi, ufuska na madhambi mengine! Hii haivumiliki. Hili ni jipu ambalo yapaswa litumbuliwe katika level zote. Kuanzia individually, kifamilia, kijamii na hata kitaifa.
Mungu anaona yote yanayotendeka. Sijui anawaza nini juu ya hayo. Tunapaswa kutubu na kubadilika ili kuepuka hasira za Mungu. Kuna wimbo maarufu wa AIC SHINYANGA unaitwa AIBU. Unatoa picha ya haya nisemayo.
Tubadilike jamani. Ni heri ukaacha kufanya chochote kuliko kusheherekea kwa namna dhalimu inayoharibu maana ya Krismas. Mungu akituchoka tutalipwa sawasawa na matendo yetu.