Kozi gani umesoma ambayo huwezi kumshauri mtu mwingine aisome?

Nimesomea Masters in Atomic Engineering nje ya nchi kule Pakistani.
Binafsi nina ujuzi wa kutengeneza mpaka mabomu ya atomic na nishati ya atomic ila nipo kitaa nimetulia napiga udalali ,kupata kazi labda niende Marekani au Iran.

Nangoja siku Tanzania tutakapoanza tengeneza umeme wa uranium hapo ndio utaona Magufuli au rais ajaye ananipigia sim moja kwa moja nakula kitengo cha mabomu na umeme.

Wenye ujuzi huu kwa Tanzania tupo wawili tu mm na jamaa yangu na wote tupo kitaa hatuna habari .
Acha kujidanganya yakuwa mpo Wawili, unajua Makamu wa rais Hatibu Bilali Yule Mzanzibar, Nae anataaluma kama yako,
 
Unaandika "mtaara" halafu unajimwambafy una masters?
Kuna nchi niliishi hapa Africa nikakuta wana mtaara unaotoa "Bachelor of Science in Witchcraft "yaani mambo ya uganga na uchawi na ukienda hospital zao kuna hicho kitengo kama ugonjwa umeshindkana hospital kuna wodi ya waliorogwa .

Ushawai kuwaza kitu kama hicho kipo duniani??
Serikali ingebidi iongeze huu mtaara kama vp wafute baadhi ya kozi waongeze hii itakuwa na soko sana mtu anaweza hata kujiajiri kirahisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Medicine doctor. Kozi gumu miaka Sita shule halafu mshahara mdogo kuliko hata aliesoma kozi ya miaka mitatu huku akila bata chuoni.

Sishauri Kabisa mtu asome kozi hii
Unategemea na lengo lako kama ni kufungua pharmacy ni sawa kazi inakuwa ni pa kusakia mtaji
 
Ukishasoma kozi yoyote ya Environmental ..
Ili watu wakuogope inabdi usome short kozi kama NOSCH hii kozi inatolewa na serikali kila mwaka kupitia OSHA kupata ratiba nenda kwny website zao ,ukimaliza hiyo soma IOSH Managing Safely hii ni Online kozi unalipa kama 400,000/=
Ukimaliza soma NEBOSH (igc) international General Certificate
hii nayo ni online kozi .Hapo unakuwa umetimia sasa hakuna wa kukunyima kazi.

Hata kama hauna Degree hizo short kozi unaweza ukasoma ,hiyo NEBOSH (igc) ukiwa na cheti chake mwenye degree akukamati maana hiyo ni kozi ya kimataifa,kama mpenda sifa kasome na SAMTRAC inatolewa South Africa na NOSA hizo zote ni kozi zinazotambulika kimataifa .Kitaifa ni NOSCH .
Kwa mimi niliyesoma kozi tofauti na environment ..tano sina degree ya mazingira, Nina degree engine kabisa..naweza somea izo short kozi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ukiona kazi zinatangazwa nne usifikiri kwamba hilo eneo halilipi hapana linalipa sana sema watu hawajajua hizo kazi zinapatikana wapi.Ukiwa na utaalam kama huo unaweza kufanya kazi kwenye hata makampuni local yanayohusika na mafuta na gas,unachotakiwa tu na kujiongezea ujuzi wa ziada.

Sio lazima ukisoma GEOLOGY uwe mchimba madini.Unaweza kuwa mtafiti(Free lance)Unaweza kuwa Broker,unaweza kuwa mshauri(consultant) unaweza kuwa anything kwenye sekta ya madini mradi uwe na utayari na uelewa.Iwapo unahitaji ushauri wa namna ya kubadili eneo lako la usomi kuwa fursa basi tuwasiliane kwa email au pm.Maisha ni kupambana
Dah bro naku pm apo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basi nenda hizo nchi za wenzetu ukafanye kazi ulipwe mshahara mnoni..sisi huku kwetu ni wito..hutaki kalime bangi..

#MaendeleoHayanaChama
Nani kakwambia.

Wito utapeleka watoto shule, au kulipia matumizi ya nyumbani au kunijengea nyumba ya kuishi.

Eti wito. Hamna kitu kama hicho. Msijidanganye.

Nchi za wenzetu madaktari wanalipwa vizuri kichizi, thamani ya kazi yao inatambuliwa.
Nyie huku mmekalia wito wito.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna masters ya finance or accounting in criminology
Sijaona chuo cha tanzania kinachotoa,hii masters ina soko sana ila watu wengi hawajaijua.
Kwa mtu akiyemaliza bachelor ya uhasibu akapiga hii masters ana opportunity kubwa sana kupata kazi sehem tofauti bila shida..
Kwa aliyepiga kozi tofauti na uhasibu hawezi piga hii masters?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom