GAGL
JF-Expert Member
- Aug 5, 2010
- 390
- 392
Napenda kulishukuru Jeshi la polisi kwa huduma za afya mnazotoa hapa baracks kurasini. Lakini kuna mambo ya ajabu hapa. Raia wa kawaida wanapoenda kutibiwa hapa kwa huduma ambayo wanailipia, wanatozwa gharama kubwa kinyume na gharama halisi kwa kuambiwa wakanunue dawa kwenye famasia iliyokaribu na kilwa pub. Mfano, shangazi yangu alienda kutibiwa malaria na presha pale, akaambiwa atoe sh 3000 kwa ajili ya dawa mseto ya malaria ambayo kihalisia inauzwa sh 600. Na kwa maelezo ya wizara ya afya, dawa hii inatakiwa kuuzwa vituo vya afya vya serikali tu au na vile vilivyothibitishwa. Kwa hapa dawa hii utaambiwa imeisha ila inapatikana famasia iliyopo hapa kilwa pub ambayo naamini ni mradi wa baadhi ya madaktari. This is against the law and it is pure corruption.