Kova,Anadanganya wakati MUAFAKA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kova,Anadanganya wakati MUAFAKA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bajabiri, Jul 16, 2012.

 1. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Al-Haji sipendi kuichanganya kazi yako na imani yako ya kidini,ila licha ya kuwa wewe ni kamanda,pia vilevile wewe ni al-haji,mtu ambaye ulifanya ibada ya kwenda kuhiji mahala patakatifu(kwa imani ya kiisalm)kwenye mji wa Makkah,,,kwa imani ya kiislam mtu akienda makkah anaenda kutubu kwa Mola(ALLAH) JUU ya DHAMBI alizofanya,anaomba Allah amsamehe,na mtu yule hufutiwa madhambi huwa msafi kama mtoto mchanga,,,,pia hata mchakato wa safari unahusisha pesa safi(zisizopatikana kwa njia ya haramu),ukitoka makkah maaswi yote uloyafanya kabla ya kwenda hupaswi kuyarudia,mfano ni KUDANGANYA,KUSENGENYA,KUNYWA POMBE,KUZINI na mengineyo yasiyompendeza ALLAH,
  Al-Haji Kova kutokana na haya yanayoendelea sasa kuna dalili kuwa una muasi Allah kwa kusema uwongo,hasa majibu yako ya leo,hivyo basi unamuasi ALLAH,nimesema umedanganya wakati muafaka kwa sababu kuna siku chache sana waislam wataingia tena kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa RAMADHAN nakushauri uutumie kutubu kwa muumba wako,kwani hiyo ni fursa pekee kwako kumuomba msamaha muumba wako,,,,hasa wakati wa kumi la MAGH****(KUMI LA KUOMBA MSAMAHA),ndo maana nikasema UMEDANGANYA WAKATI MUAFAKA,KWANI UNA NAFASI YA KUTUBU,NA NAMUOMBA ALLAH AKUPE AFYA ILI MWEZI WA RAMADHAN UWEPO NAWE UKIWEPO,,,,,,najua kazi yako ina maadili na miongoni mwa hayo KUTODANGANYA
  WASALAAM.
   
 2. E

  Etairo JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 244
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mhh. Bajabiri-we kiboko, sina hakika kama atakuwa amesoma na kuelewa ujumbe wako, lkn pia sishangai kwani kusoma na kuelewa kisha ukajidau umesahau ni kawaida kwa kova (alhaji).
  Hata mtoto mdongo hawezi kudanganyika kwa maneno na porojo za alhaj. Siku ya kwanza ulikuwa na 'confidence" mia kwa mia, lkn wenye akili waliona ulivyokuwa unababaika kusema kuwa yule mkenya ndiye mtekaji wa Dk. Ulimboka (sina hakika kama ulipima madhara yake kwa upande wa majirani zetu)
  mchungaji kachomoa, unakemea "eti suala hili liko mahakamani" mahakama ni nini? kuzuia watu kuzungumza kwa kufungwa 'suala liko mahakamani' au ndo kimekuwa kivuli cha kuwalinda walafi/wauaji/mafisadi nk.
  Mbona EPA bado inajadiliwa, chavda, Richmond IPTL, ATCL. Reli na uchavu/madudu mengine yanajadiliwa ilihali yako mahakamani? Kuna nini bwana Alhaji katika hili? Maslahi binafsi? Mbona hukugusia kuhusu kauli ya mchungaji kuwa 'ashikwe na kuhojiwa kwanza Bw. Msangi aliyetajwa awali kumteka na kujeruhi Dk? Lkn kwa huyu mkenya mara moja -mahakanai. POOOLE SAAAAAANA, wakati huo umepitwa na wakati (soma nyakati bwana eehh.)
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  mwezi unaanza kova unapaswa kuomba sana msamaha kwa maaulana
   
Loading...