JAMII-ASM
JF-Expert Member
- Jul 30, 2015
- 1,305
- 524
Wabunge kutoka kambi ya upinzani wakiwa wamevaa vifaa vya kujikinga na athari za gesi wakiingia bungeni.
Hili ni bunge la Kosovo,nchi iliyojipatia uhuru mwaka 2008 baada ya Yugoslavia kusambaratika. Bunge la Kosovo ni bunge linaloongoza kwa vituko barani Ulaya.
Kwa muda mrefu kumekuwa na mvutano mkali bungeni kati ya serikali na wabunge wa upinzani. Hoja kuu ya upinzani ni serikali itoe ufafanuzi kwanini nchi yao ya Kosovo imekithiri kwa rushwa ,ubadhilifu ,ukosefu wa ajira na umasikini.
Tarehe 19 Februari mwaka huu bila kutarajiwa wabunge wa upinzani waliamua kuingia bungeni huku wakiwa wamejihami kwa kuvaa vifaa vya kuzuia gesi (gas mask) ..... na kuanza kuwarushia wabunge wa chama tawala mabomu ya machozi
Kutokana na hali kuwa mbaya spika aliamua kusitisha shughuli za bunge na kuomba msaada wa polisi kunusuru maisha ya wabunge waliokuwa ndani ya ukumbi.
Polisi waliingia bungeni na kuwatoa wabunge waliozidiwa .
Hata hivyo wabunge wa upinzani wameapa kufanya tena walichokifanya kama hawatapata majibu sahihi kwa hoja zao wanazowasilisha bungeni. Hii ni mara ya saba wabunge wa upinzani kurusha mabomu ya machozi bungeni.