Kosa lipo wapi ukitamka Unguja na Tanganyika?

kazikubwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
597
143
Ukweli inatia uchungu sana ninaposikia kwa makusudi viongozi wetu wanapoona dhambi kutamka hadharani jina la nchi iliyohusika katika muungano, TANGANYIKA. Utawasikia Muungano wa kati ya Zanzibar na Tanzania Bara, tangu lini Tanzania bara ilifanya muungano? Hatuoni kama historia ya nchi hii inaharibiwa? Kipi kizito kwao kutamka jina la Tanganyika?

Kwa upande wa pili, utawasikia hao hao wanasema, tutakwenda Zanzibar hadi pemba na wengine hadi wanafanya makosa hadi kwenye mikutano ya kimataifa. Nenda pale bandarini, utaona wameandika boti itaondoka Dar kwenda Zanzibar na baadaye Pemba. Pemba ni sehemu ya Zanzibar, ingekuwa vema tukatamka au kuandika kuwa boti itaondoka Dar kwenda Unguja saa...na baadaye kwenda Pemba saa...Tunafahamu fika Unguja na Pemba ndiyo inatengeneza Zanzibar. Nahofia atazuka mwehu huko baadaye na kusema nakwenda Dar na baadaye Tanzania.

Nasema tena nasema mkome kutuharibia jiographia yetu pamoja na historia. Naleta hii mada hapa kwa uchungu baada ya kushuhudia ubishi wa watoto wetu wa shule za msingi, wengine wanadiriki kuwacheka wenzao kuwa hakuna sehemu inayoitwa Unguja huko Zanzibar. Kwa kujiamini wanadai kuna Zanzibar na Pemba na mmoja akaenda mbali kusema ameshafika Zanzibar lakini hakwenda Pemba.

Tunakwenda wapi? Tunawarithisha historia gani vijana wetu? Narudia tena, mkome tena mkome kutuharibia vijana wetu.

Wadau wa JF nisaidieni kuwalazimisha hawa watu wanaojitia ndimi zao haziwezi kutamka majina haya ya Tanganyika na Unguja hadharani na kuwarejesha kwenye mstari.
 
Ni sawa na kusema na kwenda musoma na baada ya hapo nitakwenda Mara. Naunga mkono hoja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom