Kosa liko upande upi?

Kosa liko upande upi?

Salum Sanane

Member
Joined
Apr 14, 2013
Posts
30
Reaction score
4
Mke akiwa safarini kwao aliandika ujumbe redioni, 'NAMRUSHA ROHO FULANI(JINA KA MUME WAKE). UJUMBE ASITEME BIGIJII KWA KARANGA ZA KUONJESHWA'.
Baada ya mume kuusikia majibizano yalianza kwa meseji.
Mume: Ujumbe wako unamaanisha nini?
Mke: Fikiria mwenyewe.
Mume: Nimeshafikiria,nimeshindwa.
Mke: Filkiria tu.
Mume: Mimi ni nani kwako?
Mke: Tusivuruge ndoa yetu bure kwa mambo ya kupita. Wewe mume wangu.
Mume: Ikiwa hivyo ndivyo nitake radhi kisha unijulishe maana yako. Ujumbe sikuupenda.
Mke: Hata mimi najua sina la kukufurahisha. Nisamee.
Haya toeni ushauri juu ya wawili hawa nani yuko sawa na nani kajichanganya.
 
Bibi na bwana wakigombana nyumbani waache wenyewe mpaka wataelewana,lakini ukiwaingilia wakipatana utabaki na .......!
 
Mke akiwa safarini kwao aliandika ujumbe redioni, 'NAMRUSHA ROHO FULANI(JINA KA MUME WAKE). UJUMBE ASITEME BIGIJII KWA KARANGA ZA KUONJESHWA'.
Baada ya mume kuusikia majibizano yalianza kwa meseji.
Mume: Ujumbe wako unamaanisha nini?
Mke: Fikiria mwenyewe.
Mume: Nimeshafikiria,nimeshindwa.
Mke: Filkiria tu.
Mume: Mimi ni nani kwako?
Mke: Tusivuruge ndoa yetu bure kwa mambo ya kupita. Wewe mume wangu.
Mume: Ikiwa hivyo ndivyo nitake radhi kisha unijulishe maana yako. Ujumbe sikuupenda.
Mke: Hata mimi najua sina la kukufurahisha. Nisamee.
Haya toeni ushauri juu ya wawili hawa nani yuko sawa na nani kajichanganya.

Big G umeinunua kisha muuza karanga anakuja kukuonjesha karanga kwa kuwa huwezi tafuna karanga zile wakati una Big G mdomoni unatema ukisha meza karanga zako kwa sekunde tu unaanza kukumbuka Big G ambayo umeshatema.

Kindoa maana yake usimwache mkeo kwa malaya wa kupita. Hapo Karanga zimekuwa kama malaya wa kupita. Big G inachukua muda mrefu kuisha utamu ambaye ndiye mke katika fumbo hilo.
 
Yote hayo ni kweli. Tatizo ni juu ya majibizano yaliyofuata.
 
Back
Top Bottom