Kosa la Magufuli-Pombe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kosa la Magufuli-Pombe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lole Gwakisa, Mar 20, 2011.

 1. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Masikini Pombe Magufuli, amejicharacterise kama mtu maarufu na anayeweza kuwa mtendaji mzuri tu wa serikali.
  Katika kufikiri hivyo Pombe Magufuli alifanya makosa makubwa ya kujikweza katika medani za kisiasa na kujiona ana uwezo wa utekelezaji mradi amepewa wadhifa wa kufanya hivyo.
  Kwanza kabisa inabibid tumuelewe Dr Pombe Magufuli kuwa ni mtu gani.
  This guy is a bull dozer who operates on matters of principles.Kitu ambacho ni muhumu sana kwa mtu wa maadili.
  Pili huyu Dr Magufuli haogopi kutekeleza yale yaliyo andikiwa (kisomi) akiwa kama mtekelezaji wa ilani ya chama chake.
  Tatu Dr Magufuli bado hajaingia katika zile duru za magwiji ya kisiasa hapa nchini, licha ya umaarufu wake.
  Nne, nafasi ya Dr Pombe katika Serikali hii ya awamu ya nne ni kama nani haswa?ikizingatiwa kuwa katika awamu ya tatu Dr Magufuli alikuwa karibu sana na Ben Mkapa.
  Dondoo hizi ndio zitatupa ukweli wa kisiasa katika utekelezaji wa majukumu ya Dr Magufuli ikizingatiwa kuwa yeye ni mwanasiasa tu katika Wizara ya Ujenzi.
  Ikumbukwe kuwa mtekelezaji mkuu wa sera za serikali katika wizara ni katibu mkuu.

  Hivyo basi, amri ya utekelezaji wa bomoa bomoa ya Dr Magufuli, pamoja na kuwa na nguvu ya kisheria haikuwa na mguvu ya kisiasa kulingana na uwezo wa kisiasa wa Dr Magufuli.
  Na ndio maana imekuwa rahisi sana kumdhibiti Dr Magufuli kuendesha zoezi la bomoa bomoa nchi nzima, zoezi ambalo wengi wanaona lingempa umaarufu kiutendaji na kisiasa.
  Waziri Mkuu Pinda hakukurupuka kumdhibiti Dr Magufuli na inaelekea kuwa si ajabu Mzee Pinda hakuchukua hatua hiyo kama yeye binafsi.
  Hivi karibuni zoezi la Dr Magufuli , ambali lingekuwa pan -territorial, lingekuwa na matokeo ya kisiasa mbayo Dr Magufuli peke yake asigeweza kuyadhibiti, hivyo kuhitaji Wizara na Idara nyingine za serikali kuingilia kati.
  Pamoja na uwezo mzuri tu wa kiutekelezaji wa Dr Magufuli, ni vyema angewasiliana na mkuu wake wa kazi pamoja na wizara nyingine kuliko kuwa na a "one man show" katika maendeleo ya nchi.
  Kwa kulinganisha tu, wale mwaziri wenye ushawishi mkubwa wa kisiasa eg Mh Sitta,Mwakyembe na hata wasio mawaziri eg Lowassa, wana uzito wa kisiasa na wa kiutekelezaji , lakini wao vile vile wamepata misuko suko.
  Nia ya Magufuli ni njema , lakini inabidi ajenge political base ili awe na nguvu ya kiutekelezaji
   
 2. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijakuelewa!!unataka mapadlock awaonge wajumbe wa vikao muhimu ccm ili awe na political base kama mzee wa mvi?
   
 3. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  mheshimiwa John Magufuli na Mpendwa wa WaTz wote, nakushauri ondoka kwenywe hiyo merikebu inayoitwa CCM maana utatoswa muda si mrefu kama Yona vinginevyo Mungu kama anakuhitaji kukomboa WaTanzania atakutosa na utaifanya kazi kwa kiboko, kumbuka Malkia Ester alivyotakiwa kuwakomboa Israel, aliambiwa kuwa akikaa kimya ukombozi utapotikana kwa njia nyingine na yeye hatasalimmika kwakuwa yuko ndani. Uko katikati ya mafisadi wakiamua watakutosa any time na anguko litakuwa la kutisha, ccm ina baadhi ya watu wazuri lakini wasipojipambanua watangukia ktk anguko moja na hawataweza kujisafisha tena.
   
 4. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hapo nilipokoleza inawezekana pana ukweli hapo,ukichukulia na mahali lilipotolewa katazo.Pinda inawezekana ametumika kumdhibiti Magufuli.Na yote hii ni vita kuelekea 2015
   
 5. m

  mwanza_kwetu JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 684
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Magufuli ni mtendaji mzuri ila ni mtu asiyejiamini na ni mwepesi kudhibitiwa maana hataki kusikiliza mawazo ya wengi. 2005 alitakiwa aingie ktk kinyang'anyiro cha urahisi hata kama angeshindwa, ila ingeonyesha ana vision. Otherwise Pinda kafanya alichoagizwa na mafisadi ya kumfunga miguu magufuli maana hafunganani na kundi lolote kwa usafi wake walau huo wa kiutendaji. Ila hilo ni goli kwa ccm maana huyo ndiye pekee alikuwa turufu. Naamini baada ya magufuli kufungwa kamba sasa Chadema wana nguvu na wanapumua kwa uhakika maana ccm haina mahala pa kukimbilia 2015 wanaondoka
   
 6. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tatizo ni kwamba Pinda anajaribu ku-win a double trust. Meaning anataka awe mnafiki wa hali ya juu. Anataka aonekane anawatetea wanaovunjiwa nyumba (makazi na biashara), huku akitaka wananchi waamini kwamba serikali inawatetea?!!!!!!!!!!!!
   
 7. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mtemiwao , siasa za ushawishi haziendani kwa kuhonga , na kwa vyovyote vile hayo ni mawazo finyu.
  Ushawishi wa kisiasa ni pamoja na kukubalika katika kile chama kinacho-msponsor mwanasiasa wake.Pamoja na utendaji wake wa kasi Dr Magufuli bado hajaweza kujipenyeza na kukubalika vyema katika chama.
   
 8. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2011
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Sijui mutoa mada alikuwa na lengo gani maana kama ni insha yaonekana haina maudhui.

  Haya ndo mambo yanayotufanya tuwe watumwa wa CCM. Yaonekana hata wewe bado unaamini mafanikio ni kusifiwa na chama. Chama kwanza nchi nyuma, Kingunge style. Ni mtindo kwa utawala ambao hata siku moja hautaleta yaliyomema.

  Hebu angalia ni akina nani wana hiyo inayoitwa base ktk chama. Tuambie ni nani mtu mwenye substance. Lowasa? Makamba? Rostam? au nani?

  Ni aibu kumukosoa Magufuli kwa kutumia mazingira dhaifu yaliyopo badala ya kuangalia muelekeo wetu ni upi.

  Huyo Pinda! Mungu apishe mbali maana nasikia naye kisha anza kuuona urais unakuja kwake. Sifa kuu aliyo nayo ni upole. UPOLE!

  Sijawahi hata kumusikia akitoa hotuba ya kukumbukwa. Utawala huu sasa hivi ni gari bovu lenye dereva asiye na leseni.

   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Umefanya uchambuzi makini sana. Huo ni ukweli kabisa. Hivi manajua zaidi ya kuwa mbunge, Dr. Pombe hana cheo kingine huko CCM? He has no political base at all even though he is a good political performer in the Government!!
   
 10. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hivi ilishindikana nini kwa WAziri mkuu Pinda kumwita katika kikao na kumwagiza Magufuli astop na zoezi lake la bomoa bomoa badala yake anamzalilisha mbele ya hadira?
   
 11. m

  matawi JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  100% lazima michezo ya kisiasa aanze kuzoea kuicheza
   
Loading...