jf user
JF-Expert Member
- Aug 22, 2018
- 777
- 625
Kijana mwenzangu ulieko chuo chochote Tanzania hii kuanzia certificate, diploma, degree hata masters kama uliunga hebu leo tuzungumze kwa kina.
Ewe kijana mwenye level yeyote hapo juu unakuta umepanga room nje, Room yako umeijaza sofa, TV, kitanda cha 6 kwa 6 na godoro kali sana la QFL pembeni lipo upo mtungi wa gesi, rice cooker, Subwoofer au Home Theatre kwa wale wenzangu wapenda mziki. Zipo furniture za kisasa kama meza, meza za viio, kabati, kabati la nguo, viti, vipo vyombo vya chakula, ndoo n.k
Chumba walipia maybe 50,000-100,000 kwa mwezi, eneo ulipo waweza jichanganganya na raia wa hilo eneo ukapiga kazi ya maana na ikakupa pesa ndefu ya kukusomesha hata mpaka master. Kama ulibahatika una mkopo wa HESLB Mungu akupe nini tena?
Kwa shuhuli unazoweza kuzifanya ni biashara ya duka ukamuacha mtu aua hata wewe uwe una shift kulingana na vipindi vya darasani, Umelima mashamba ya mpunga, bodaboda, mahindi, maharagwe, alizeti, umefuga kuku as unaweza tengeneza banda mobile la kutunza kuku kama 50 ndugu yangu kwanini usitoboe? Kwanini usinunue kiwanja ujenge nyumba yako? ndugu na wazazi wako kwa nini usiwatumie hela ya sukari na ada hasa wadogo zako?
Ukiutumia muda wa chuo vizuri utatoboa pia kumkabidhi MUNGU maisha yako kwa maana yeye ndie mwenye maisha yetu.
Ukinunua mifuko ya mchele, maharagwe, choroko, dagaa, mahindi na mavitu mengine ya kula tofauti na ile ya kula Canteen na mboga wanunua sokoni si utakua ume save pesa nyingi sana?
Imagine sio mnywaji sana wa pombe au hutumii kabisa pia sigara, huendi club kila weekend na una demu mmoja au huna kabisa japo naamini hii ni applicable kwa watumishi wa MUNGU kwanini usifike mbali? Ukiilinda afya yako dhidi ya magonjwa ya ukimwi n.k kwanini usifike mbali?
Kama biashara itaweza kwenda vizuri unaweza ahirisha mwaka mzima wa masomo upige kazi kwani ndio utu uzima huo kwanini usifike mbali?
Mnapokosea wanachuo
1/Mnapomaliza chuo mnauza kila mlicho nacho kwa bei ya hasara hapa mnafanya makosa makubwa sana ni bora musafirishekwenu hata gaharama zikiwa kubwa vipi kwani gharama itakua ni ndogo au basi hata ikiwa kubwa kiasi still itakusaidia kwa sababu vitu vyako vitaenda kukusaidia baadae. Ukipiga hesabu eti utakuja kununua baadae we tambua gharama zinapanda huku mtu mzima dada au kaka wahitaji kuwa na familia yako na mambo mengine kwa hiyo unafanya blunders! So iwapo utauza hakikisha asilimia 85% uliyotumia kununulia inarudi hii ni kutokana na kwamba vitu ni used na vingine vimepoteza quality so used item bei yake ni chee.
2/Kurudi kwa wazazi wenu
Hapa naomba niwaambie ukweli tuu ndugu zangu mnakosea sana yani ni sawa na kuruka mkojo halafu ukanyege mavi! Huko nyumbani wafata nini? kama eneo la kuishi unalo na ni kwa bei nafuu as I know mageto wanayopanga wanafunzi ni bei chee tofauti na vyumba vya kawaida kwa nini usitulize kichwa na kuwaza utatokaje hapo geto?
Unaporudi nyumbana ukagombanie mandazi na wadogo zako na kuwasumbua wazazi wako waona hilo ni sawa? Kidume mzima huna aibu? bora hata mdada anajua ataolewa vipi wewe dume mwenzangu mkeo utamleta mje mbanane nyumba za wazazi?
Its shocking but niwaambie tuu huo muda mtakao kuwa mnasubira ajira kaeni kwenye hayo mageto mkisumbua akili mpate namna ya kujitaftia kipato na kwa Tanzania hii asilimia 100%fikiria kuhusu kujiajiri, tumia ujuzi wako kufungua huduma yako mambo ya kuwaza kuajiriwa niwapo pole. Hilo toeni akilini mwenu.
Mwisho
"The most beautiful part of human body is brain" hii quote aliyotoa marehemu Steve Jobs wa Apple.
Mimi naitumia hiyo kukushauri ndugu mwanachuo tumia akili yako, kikune kichwa chako kutatua matatizo yako! Tabia ya kurudi kwa wazazi na kujipanga eti utoke kiamaisha imepitwa...
Guys you must think wise and different acheni kuishi kwa mazoea. Get up, prays to GOD kijana kachakarike maisha ni popote sio kuajiriwa tuu. Tumia nguvu zako sasa kijana wangu kabla hazijaisha huko mbeleni ni taabu kama hukujiandaa ujanani mwako.
Wenzio tungepata fursa kama hii ungekuta tuko mbali sana kimaisha ila tumshukuru MUNGU kwa yote...
Kijana mwenzangu unapopata fursa itumie vizuri kwani hujue kesho itakuaje.
MUNGU awe nanyi ndugu.

...mkuu umenipa akili hata mimi kwasababu mi pia ni miongoni mwa wanachuo hapa mwanza chuo cha mipango. Nahisi imefika kwa walengwa mahususi!