Korti yakubali ombi la Mpendazoe, Lissu kidedea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Korti yakubali ombi la Mpendazoe, Lissu kidedea

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 9, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,874
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imekubali ombi la aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Segerea, Fred Mpendazoe (CHADEMA), la kutaka mahakama imruhusu aweke sh milioni 15 mahakamani kama dhamana.
  Dhamana hiyo ni kwa kila mdaiwa ambapo wadaiwa katika kesi hiyo ni mbunge wa Segerea na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (CCM), Mwanasheria Mkuu wa Serikali na aliyekuwa Msimamizi wa Uchaguzi anazotakiwa kuzitoa kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2010.
  Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Profesa Ibrahimu Juma ambapo alisema anakubaliana na ombi lilowasilishwa na wakili wa Mpendazoe, Peter Kibatala, lililoiomba mahakama hiyo iwaruhusu kuweka kiasi hicho cha fedha kwa sababu ombi hilo limekidhi matakwa ya kisheria.
  “Mahakama inakubaliana na ombi la mlalamikaji (Mpendazoe) na linalitupilia mbali pingamizi la mdaiwa (Dk. Mahanga) na wenzake kwa sababu kifungu cha sheria walichokitumia kuwasilisha pingamizi hilo si sahihi na hakiendani na ombi la mlalamikaji.
  “… kwa maana hiyo mahakama imemruhusu mlalamikaji kuwasilisha kiasi hicho cha fedha na ndipo kesi ipangwe tarehe ya kuanza kusikilizwa,” alisema Jaji Juma.
  Februari 28 mwaka huu, wakili wa Mpendazoe, Peter Kibatala aliwasilisha ombi jipya la kuomba mteja wake aruhusiwe kuweka kiasi hicho cha fedha kwani tayari mteja amepata kiasi hicho cha fedha.
  Katika kesi ya msingi Mpendazoe anapinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 katika jimbo la Segerea yaliyomtangaza Dk. Mahanga kuwa mbunge wa jimbo hilo.
  Katika katua nyingine, Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma imetupilia mbali maombi ya kuondoa ama kusamehewa dhamana za gharama za uendeshaji kesi za uchaguzi, yaliyofunguliwa na wanachama wawili wa CCM dhidi ya mbunge wa Singida Mashariki, Tindu Lissu (CHADEMA).
  Hukumu hiyo ilitolewa jana na Jaji Silivangira Mwangesi na kuongeza kuwa Lissu ameshinda kesi hiyo kutokana na kutofuatwa kwa utaratibu wakati wa kufungua kesi hiyo.
  Hata hivyo, hukumu hiyo ilitolewa wakati Lissu hakuwepo mahakamani. Mlalamikiwa huyo aliwakilishwa na ndugu yake aliyejitambulisha kwa jina la Samson Mkotya ambaye alidai alifanya hivyo kwa kuwa Lissu aliharibikiwa na gari mkoani Morogoro.
  Maombi hayo yaliwasilishwa na wanachama wawili wa CCM, Shaban Itambu na Pascal Hallu ambao wamewafungulia kesi ya kupinga matokeo ya ubunge jimbo la Singida Mashariki, Tindu Lissu, Msimamizi wa Uchaguzi na Mwanasheria wa Serikali.
  Hata hivyo, Lissu alipinga maombi hayo kwa sababu waombaji hawakuwasilisha maombi ya kutaka kupangiwa dhamana ya gharama za uendeshaji kesi za uchaguzi.
  Lissu aliwasilisha hukumu za kesi tatu ambazo mahakama kuu iliwahi kuzitupa baada ya walalamikaji kutowasilisha kwanza maombi ya kupangiwa dhamana hiyo. Hukumu zilizowasiliswa na Lissu ni ya John Mnyika na Charles Keenja, Joyce Chitende na Zainabu Gama, John Jomba Koyo na Christopher Ole Sendeka. Akipinga pingamizi hilo, wakili wa walalamikiwa hao ni Abdallah Possi, alisema si lazima Jaji akubaliane na hukumu hizo ambazo zimetolewa na majaji wenzake wa mahakama hiyo.
   
Loading...