Korea Kusini wamefanya, je nasi hatuwezi Fanya uchaguzi October?

Ramark

JF-Expert Member
May 19, 2015
1,989
1,441
Wana jukwaa,

Nchi ya Korea Kusini kama ilivyo kawaida baada ya miaka 4 hufanya uchaguzi wa Wabunge kila tarehe 15 April, Leo wamefanya uchaguzi.

Uchaguzi umepata wapiga kura 17.2 waliofika vituoni licha ya kuwepo maambuzi ya corona tukijua kuwa, ndiyo nchi iliyokumbwa na maambukizi makubwa kama China kwa mashariki ya mbali; kwani walipaswa kuvaa barakoa, na wasimamizi waliwasanitazer, kuwapima joto KISHA kuwapa gloves zinazotupwa lkn pia walikuwa wanasanitazer vituo kila baada ya mtumiaji mmoja hivyo kuimarisha usalama wa wapiga kura. Lakini usimamaji nao ulizingatia umbali wa mita 1 kila baada ya mtu.

Walioko karantini pia walipewa nafasi ya kupiga kura kwa muda baada ya upigaji kura kukamilika kama ingekuwa kwetu ni kuanzia SAA 10-12 ila kwao imeanza SAA 11:30 jioni hadi 1:00 usiku. Pia walipimwa joto kabla ya kutoka karantini na waliendelea kufuatiliwa kwa app ili wasikimbie. Vilevile walipaswa kusimama mita mbili kila baada ya msimamaji mmoja.

Wagonjwa
Walipewa nafasi ya kushiriki kwa kupiga kura kwa posta kama wamejiandikisha kabla ya march 30.
Hata hivyo waliopiga kura kwa posta ni zaidi ya 11m hivyo kutengeneza zaidi ya 66% ya wapiga kura, yaani wapiga kura w amekuwa wengi tofauti na kipindi cha karibuni kwani wakorea zaidi ya 70% walipga kura 1992 hivyo hii ni idadi kubwa ikiifuata ya mwaka 1992 kwenye uchaguzi Mkuu.

Corona imekuwepo na waliambukizwa wengi pia kufa tofauti na Tz je, haiwezi kuwa mfano nasi tukabaki na wazo letu LA uchaguzi?

Wengine wanaweza kupinga kuwa S.korea in nchi angalau IPO juu kiteknolojia na kwa kipato cha MTU mmoja mmoja lkn bila kusahau mfumo wao WA elimu umeruhusu wananchi wengi kupata elimu nzuri tofauti na hapa.

Lkn pia wapo wanaoweza kubaki na wazo la Rais LA kuendelea na uchaguzi licha ya changamoto ya Corona kwani ni kuheshimu mfumo wetu WA siasa pia si janga kubwa na Tz haijatangaza hali ya hatari hivyo uchaguzi haupingiki. Endapo ikitokea maambukizi kuongezeja mifumo yetu ya afya inaweza kuendelea kuwatibu wagonjwa.

Kinachoonekana kwa uhalisia

Tz kufanya uchaguzi katika attention hii ni changamoto kwa wapiga kura kwani mifumo yetu ya siasa haiaminiki hasa Tume ya uchaguzi, vyombo vya ulinzi na media ikiwemo TCRA. Watz wanaonekana bado hawawezi kuiamini mifumo hiyo ya siasa kwani katika nyakati zisizo na attention havikufanya vizuri je wakati huu watafanya vizuri?

Kwa kutofunga ofisi kupokea fomu za ugombea, viapo vya mawakala, kurushwa hewani kwa hotuba za wapinzani, kutowafuatilia whistle blowers, watoa maoni na watengenezaji katuni piakutokutengeneza jam wakati WA ufuatiliaj kampen.

Lkn kama mikutano au kampeni ikiendelea kuanzia sasa je, umuhimu WA siasa kwa maisha ya watu utamaanisha? Je taratibu za primary zinaweza fanyika kwa usalama wakati vyana havina fedha hata za kujilinda?

Sijui ni swali lililopo kichwani mwangu na kwenu pia
Kama kuna MTU ana majibu au maswali ya kuongeza, karibu ili tufanye Tafakuri ya kina.
 
Tume huru kwanza Tanzania then hayo maswala ya kampeni na uchaguzi ndyo yafuate kujadiliwa na hayawez yakashindikana kamwe
 
Tume huru ya uchaguzi kwanza, hizo taratibu za ugonjwa elimu itaendelea kutolewa na hata kwenye mikutano ya kampeni.
 
kwanza kampeni zao zilikuaje? za kwetu tunajua zinavyorundika watu, hapa bongo bado hatuwezi kuwaiga, maana tutazidi kuambukizana!
 
Kwanza pambana na Covid-19, kwani Uchaguzi tunachaguwa watu walio hai.Uzima kwanza.
Korea wameudhibiti kisayansi,ndio maana wameshinda kuendelea na uchaguzi wa wabunge.
 
Uchaguzi unaandaliwa mapema, kama maandalizi ynachelewa nini kinamaanisha?
Mwezi may primary zinaanza je,kwa mazingira haya?
 
Back
Top Bottom