Korea Kaskazini yakata mawasiliano na Marekani.

Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Messages
17,650
Likes
51,691
Points
280
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2015
17,650 51,691 280
8a3733bedccdb165f3284dabc2e31182.jpg

Maafisa wa runinga inayothibitiwa na serikali ya Korea Kaskazini wamesema kuwa serikali ya nchi hiyo itakata mawasiliano na Marekani.

Korea Kaskazini inasema kuwa utawala wa Washington tayari umefahamishwa sababu ya hatua hiyo.

Aidha Korea imesema kuwa maswala ambayo bado yabajadiliwa ikiwa pamoja na kukamatwa kwa wamarekani wawili sasa yatajadiliwa chini ya sheria kali za kivita.

Korea Kaskazini inasema hatua hiyo imefikiwa katika kile kinachotajwa sheria za kivita

Shirika hilo la serikali aidha linasema kuwa imeafikia hatua hiyo baada ya marekani kumuorodhesha rais wa nchi hiyo Kim Jong-un katika orodha ya wale waliopigwa marufuku kutokana na rekodi mbaya ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Wakati huo huo Korea imeapa kudungua manuari yeyote ya kivita itakayolenga roketi zake za masafa marefu.

Marekani na Korea kusini zimetangaza mipango ya kuweka mfumo wa ulinzi wa Terminal High Altitude Area Defense (THAAD) unaolenga kudungua makombora ya masafa marefu ya Korea Kaskazini.

Korea Kaskazini imeonya kuwa hilo ni dhihirisho la mataifa hayo kuichokoza na hivyo kutangaza vita dhidi yao.

Hata hivyo haijajulikana marekani na Korea Kaskazini zitaweka wapi mtambo huo wa ulinzi wa kisasa na yupi kati ya washirika hao wawili watauendesha mtambo huo wenye uwezo mkubwa wa ulinzi dhidi ya makombora.

Chanzo : BBC
 
mchome jr

mchome jr

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2015
Messages
600
Likes
730
Points
180
mchome jr

mchome jr

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2015
600 730 180
USA wameingia choo cha kike sahivi...!hawa jamaa wanajiamini vibaya mno.
 
Fundi chupi

Fundi chupi

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Messages
344
Likes
240
Points
60
Age
25
Fundi chupi

Fundi chupi

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2016
344 240 60
Tumechoka kusikia maneno bila vitendo
 
painscott

painscott

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2015
Messages
233
Likes
119
Points
60
painscott

painscott

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2015
233 119 60
Hata hivyo haijulikaniki marekani na Korea ya kaskazini zitaweka wapi mtambo huo.............. Sijaelewa, how come wsshirikiane wakati ni maadai# kabaash
 
Cendy

Cendy

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2015
Messages
1,148
Likes
2,184
Points
280
Age
25
Cendy

Cendy

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2015
1,148 2,184 280
8a3733bedccdb165f3284dabc2e31182.jpg

Maafisa wa runinga inayothibitiwa na serikali ya Korea Kaskazini wamesema kuwa serikali ya nchi hiyo itakata mawasiliano na Marekani.

Korea Kaskazini inasema kuwa utawala wa Washington tayari umefahamishwa sababu ya hatua hiyo.

Aidha Korea imesema kuwa maswala ambayo bado yabajadiliwa ikiwa pamoja na kukamatwa kwa wamarekani wawili sasa yatajadiliwa chini ya sheria kali za kivita.

Korea Kaskazini inasema hatua hiyo imefikiwa katika kile kinachotajwa sheria za kivita

Shirika hilo la serikali aidha linasema kuwa imeafikia hatua hiyo baada ya marekani kumuorodhesha rais wa nchi hiyo Kim Jong-un katika orodha ya wale waliopigwa marufuku kutokana na rekodi mbaya ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Wakati huo huo Korea imeapa kudungua manuari yeyote ya kivita itakayolenga roketi zake za masafa marefu.

Marekani na Korea kusini zimetangaza mipango ya kuweka mfumo wa ulinzi wa Terminal High Altitude Area Defense (THAAD) unaolenga kudungua makombora ya masafa marefu ya Korea Kaskazini.

Korea Kaskazini imeonya kuwa hilo ni dhihirisho la mataifa hayo kuichokoza na hivyo kutangaza vita dhidi yao.

Hata hivyo haijajulikana marekani na Korea Kaskazini zitaweka wapi mtambo huo wa ulinzi wa kisasa na yupi kati ya washirika hao wawili watauendesha mtambo huo wenye uwezo mkubwa wa ulinzi dhidi ya makombora.

Chanzo : BBC
Kwanini ni hawa jamaa wana nini
 
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Messages
17,650
Likes
51,691
Points
280
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2015
17,650 51,691 280
Hata hivyo haijulikaniki marekani na Korea ya kaskazini zitaweka wapi mtambo huo.............. Sijaelewa, how come wsshirikiane wakati ni maadai# kabaash
Ushirikiano hapo ni marekani na Korea kusini dhidi ya Korea Kaskazini mkuu
 
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Messages
80,779
Likes
46,178
Points
280
Age
28
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined May 15, 2006
80,779 46,178 280
No one really cares.

They could go jump in the river and the good 'ol USA couldn't care less!
 
Forum statistics

Threads 1,235,727
Members 474,712
Posts 29,232,567