Korea Kaskazini: Ripoti mpya yafichua mamia ya maeneo ya kuua Watu hadharani

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Shirika moja lisilo la kiserikali nchini Korea Kusini linasema kuwa limegundua maeno 318 nchini Korea Kaskazini ambayo yanatumia na serikali kuua watu hadharani.

Shirika hilo limewahoji watu 610 waliotoroka Korea Kaskazini zaidi ya miaka minne iliyopita ili kuandaa ripoti yake.

Limeorodhesha mauaji yaliyotekelezwa miongo kadhaa iliyopita, ambayo yalijumuisha makosa kama ya uwizi wa ng'ombe na kutizama televisheni ya Korea Kusini.

Mauaji ya hadharani yalifanywa karibu na maeneo ya mtoni, viwanjani, sokoni, shuleni, na viwanja vya michezo, lilisema shirika hilo la kutetea haki.

Kundi la watu 1,000 au zaidi walikua wakijitokeza kushuhudia mauaji hayo, lilisema shirika hilo katika ripoti yake inayofahamika kama ''Ramani ya hatma ya waliofariki'', iliyotolewa siku ya Jumanne.

Ripoti hiyo inadai kuwa familia za wale waliohukumiwa kifo, wakiwemo watoto wakati mwingine zililazimishwa kushuhudia mauaji hayo.
Miili ya waliouawa haikuwahi kupewa familia zao wala kuoneshwa mahali ilipozikwa.

Kwa mujibu wa ushahidi, mtu mdogo zaidi kushuhudia mauaji hayo alikuwa na miaka saba.
Mauaji mengine yalikuwa yakitekelezwa katika vituo vya kuzuilia watu kama vile jela na kambi za kufanya kazi- ambapo watu walioshitakiwa kwa uhalifu wa kisiasa wanalazimishwa kufanya kazi ya ngumu kama vile ya uchumbaji madini na kukata miti.

Mmoja wa watu waliohamia kusini ambaye alizuiliwa katika kambi ya kazi miaka ya 2000 alielezea jinsi wafungwa 80 walivyolazimishwa kushuhudia mauaji ya wanawake watatu walioshitakiwa kwa jaribio la kutorokea China.

Walisema kuwa afisa wa wizara ya usalama aliwaambia watu: "Hili linaweza kuwakuta."
Ripoti hiyo inasema mauaji ni "mbinu kuu inayotumiwa na utawala kuwatia hofu wanainchi wanaojihusishana vitendo vinavyodhaniwa kuhujumu serikali".

Kuuawa na kuigwa risasi na kunyongwa
Mauaji mara nyingi yalikua yakitekelezwa kupitia kikoso maalu cha kuwamiminia watu risasi, waliotoroka wanasema .

Mauaji kama hayo mara nyingi yalihusisha maafisa watatu wanaomiminia risasi za rashasha mtu aliyehukumiwa kifo.

Baadhi ya watu waliohojiwa walisema kuwa baadhi ya watu waliopewa jukumu la mauaji walionekana kuwa walevi.

Mmoja alisema "hii ni kwasababu kazi ya kuua ni ngumu sana na huathiri hisia ya mtekelezaji wa kitendo hicho".

Ni idadi ndogo ya visa vya maauaji ya kunyongwa hadharani viliripotiwa, japo shirika hilo linasema huenda mauaji ya hayo yalipunguzwa au yalisitishwa tangu mwaka 2005.

Ethan Shin, mmoja wa waandalizi wa ripoti hiyo ameliambia shirika la habari la AFP kwamba "huenda idadi ya mauaji ya watu hadharani imeanza kupungua", lakini Pyongyang huenda pia inafanya hivyo kisiri "inapojaribu kujionesha kama taifa la kawaida".

Maafisa wa ngazi ya juu wa Korea Kaskazini pia hakuponea mauaji kama hayo. Mwaka 2013, mjomba wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un aliuawa kwa kufanya kosa la uhaini.

Lakini ripoti ya mauaji ni vigumu sana kuthibitisha, na kwasababu visa vya watu kusemekana wameuawa na baadae kubainika kuwa uwongo vimewahi kutokea .

Kwa mfano mwaka 2013, Mwimbaji maarufu wa Korea Kaskazini Hyon Song-wol alidaiwa kuuawa hadharani, na hata Gazeti moja la Korea Kusini likaripoti kuwa aliuawa kwa kupigwa risasi na kunukuu kwamba "alimiminiwa risasi huku waimbaji wa bendi yake wakishuhudia".

Lakini mwimbaji huyo alionekana mwaka 2018 akiwa miongoni mwa wajumbe wa Korea Kaskazini waliozuru Seoul kabla ya mashindano ya Olimpiki ya msimu wa baridi.

BBC
 
11 Juni 2019.

Western propaganda kuichafua n Korea..kumbe sometimes Ni hisia tu zisizo na ukweli..
 
AFADHALI WAO WANAOUWA KWA KUJIFICHA ILA WESTERN KILA SEC WANAWA MAELFU YA WATU DUNIANI, AU NDIO NYANI HAONI MK...... WAKE
 
Korea Kaskazini: Ripoti Mpya Yafichua Mamia Ya Maeneo Ya Kuua Watu Hadharani

1124659

Shirika moja lisilo la kiserikali nchini Korea Kusini linasema kuwa limegundua maeno 318 nchini Korea Kaskazini ambayo yanatumia na serikali kuua watu hadharani.

Shirika hilo limewahoji watu 610 waliotoroka Korea Kaskazini zaidi ya miaka minne iliyopita ili kuandaa ripoti yake. Limeorodhesha mauaji yaliyotekelezwa miongo kadhaa iliyopita, ambayo yalijumuisha makosa kama ya wizi wa ng'ombe na kutizama televisheni ya Korea Kusini.

Mauaji ya hadharani yalifanywa karibu na maeneo ya mtoni, viwanjani, sokoni, shuleni, na viwanja vya michezo, lilisema shirika hilo la kutetea haki.

Kundi la watu 1,000 au zaidi walikua wakijitokeza kushuhudia mauaji hayo, lilisema shirika hilo katika ripoti yake inayofahamika kama ''Ramani ya hatma ya waliofariki'', iliyotolewa siku ya Jumanne.

Ripoti hiyo inadai kuwa familia za wale waliohukumiwa kifo, wakiwemo watoto wakati mwingine zililazimishwa kushuhudia mauaji hayo. Miili ya waliouawa haikuwahi kupewa familia zao wala kuoneshwa mahali ilipozikwa. Kwa mujibu wa ushahidi, mtu mdogo zaidi kushuhudia mauaji hayo alikuwa na miaka saba.

Mauaji mengine yalikuwa yakitekelezwa katika vituo vya kuzuilia watu kama vile jela na kambi za kufanya kazi ambapo watu walioshitakiwa kwa uhalifu wa kisiasa wanalazimishwa kufanya kazi ngumu kama vile ya uchumbaji madini na kukata miti.

Mmoja wa watu waliohamia kusini ambaye alizuiliwa katika kambi ya kazi miaka ya 2000 alielezea jinsi wafungwa 80 walivyolazimishwa kushuhudia mauaji ya wanawake watatu walioshitakiwa kwa jaribio la kutorokea China.

Walisema kuwa afisa wa wizara ya usalama aliwaambia watu: "Hili linaweza kuwakuta."

Ripoti hiyo inasema mauaji ni "mbinu kuu inayotumiwa na utawala kuwatia hofu wananchi wanaojihusisha na vitendo vinavyodhaniwa kuhujumu serikali".

Kuuawa kwa kupigwa risasi na kunyongwa

Mauaji mara nyingi yalikua yakitekelezwa kupitia kikosi maalum cha kuwamiminia watu risasi, waliotoroka wanasema. Mauaji kama hayo mara nyingi yalihusisha maafisa watatu wanaommiminia risasi za rasharasha mtu aliyehukumiwa kifo.

1124662

Kim Yong-chol (Kulia) anatajwa kuwa mshirika wa karibu wa Rais Kim Jong-un

Baadhi ya watu waliohojiwa walisema kuwa baadhi ya watu waliopewa jukumu la mauaji walionekana kuwa walevi.

Mmoja alisema "hii ni kwasababu kazi ya kuua ni ngumu sana na huathiri hisia ya mtekelezaji wa kitendo hicho".

Ni idadi ndogo ya visa vya maauaji ya kunyongwa hadharani viliripotiwa, japo shirika hilo linasema huenda mauaji ya hayo yalipunguzwa au yalisitishwa tangu mwaka 2005.

Ethan Shin, mmoja wa waandalizi wa ripoti hiyo ameliambia shirika la habari la AFP kwamba "huenda idadi ya mauaji ya watu hadharani imeanza kupungua", lakini Pyongyang huenda pia inafanya hivyo kisiri "inapojaribu kujionesha kama taifa la kawaida".

Maafisa wa ngazi ya juu wa Korea Kaskazini pia hakuponea mauaji kama hayo. Mwaka 2013, mjomba wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un aliuawa kwa kufanya kosa la uhaini.

Lakini ripoti ya mauaji ni vigumu sana kuthibitisha, na kwasababu visa vya watu kusemekana wameuawa na baadae kubainika kuwa uwongo vimewahi kutokea.

Kwa mfano mwaka 2013, Mwimbaji maarufu wa Korea Kaskazini Hyon Song-wol alidaiwa kuuawa hadharani, na hata Gazeti moja la Korea Kusini likaripoti kuwa aliuawa kwa kupigwa risasi na kunukuu kwamba "alimiminiwa risasi huku waimbaji wa bendi yake wakishuhudia".Lakini mwimbaji huyo alionekana mwaka 2018 akiwa miongoni mwa wajumbe wa Korea Kaskazini waliozuru Seoul kabla ya mashindano ya Olimpiki ya msimu wa baridi.

Chanzo: BBC
 
Back
Top Bottom