Korea Kaskazini ndiyo nchi yenye sheria za ajabu zaidi kwa raia wake

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
15,267
29,906
#JE WAJUA........?

KOREA KASKAZINI NDIYO NCHI YENYE SHERIA ZA AJABU ZAIDI KWA RAIA WAKE.
________________________________________________Hebu chukua muda wako kusoma hizi baadhi ya Sheria za huko Korea Kaskazini, Na ukitaka kuuliwa kirahisi, basi we nenda kinyume na hizi - hawana muda wa kukubembeleza!
.
1. ITERNATIONAL CALLS/Kuwasiliana na Watu wa nje ya Nchi - Ni marufuku kupiga simu kuwasiliana na Mtu alieko nje ya Nchi.
.
2. KUFANYA KAZI - Swala la Free time kule hakuna. Kila mtu atafanya kazi kwa Masaa angalau 17 kilasiku, hio ni lazima sio hiari.
.
3. KUNYOA - Hakuna uhuru wa kunyoa unavotaka wewe. Serikali imetoa staili 28 tu za kunyoa (Kwa jinsia zote mbili) - kwahio mtafuata hizo na si vinginevyo.
.
4. KUKAA MJINI - Serikali ndiyo itachagua nani akae mjini. Wanaoruhusiwa na Kim Jong-Un kukaa Mjini ni Wafanya Biashara maarufu wenye pesa zao na Watu wenye nguvu flani kwenye Jamii.
.
5. KUANGALIA TV - Sahau kuusu Movies. Utaangalia Channels 2 tu, Na kila kinachoendelea kwenye Channels hizo kinaendeshwa na Serikali. Ukikamatwa unaangalia kitu tofauti kwenye TV imekula kwako.

6. BIBLIA - Ni kosa la jinai kumiliki Biblia. Wao wanaamini hizo ni Tamaduni wa Kizungu kwahio utasababisha Watu wazifuate (Sijajua kuusu QURAN)
.
7. Bidhaa za Apple, Sony na Microsoft haziruhusiwi.
.
8. KWENDA/KULIA MSIBANI - Akifa Raisi Wananchi wote lazima kuhudhuria Msiba na lazima wote mlie. Alipokufa Baba yake Kim Jong Wananchi wote walilia. Korea kaskazini Raisi ni kama mungu.
.
9. KUMILIKI GARI - Hairuhusiwi kumiliki Gari, labda uwe Mfanya kazi wa Serikali au Mfanya Biashara mkubwa myenye Pesa. Magari ni Machache Barabarani kiasi kwamba ni ngumu kuskia eti kuna Ajali labda mtu Kagongwa.
.
10. KUPIGA PICHA - Ni marufuku kupiga Picha, uwe Mwananchi au Mtalii - ni marufuku. Anaeruhusiwa kumiliki Kamera labda Mpiga picha wa Kim Jong Un.
.
11. MAKOSA NA ADHABU - Akifanya kosa mtu mmoja kwenye Familia yenu mnaadhibiwa Familia nzima (Uwe mtoto au Mtu mzima) wote mtawajibika.
.
12. KUPIGA KURA - Mfumo wao ni kwamba Jina la mgombea ni Moja tu na lazima mumchague huyo. Ndio Majina ya Wagombea wengine yapo pale, lakini ni kama kivuli ili Nchi ionekane iko Fair.

SOURCE:

9 Strange Laws In North Korea That'll Make You Glad You're Living In India
 
Namba 10 sina hakika kama ni kweli maana nimeona kijana flani wa U.K alienda soma K.K amemaliza na sasa hivi anasaidia watu wanaotaka kwenda tembea K.K au kusoma na ametupia mipicha kibao akiwa K.K
 
Hiyo Nchi Ni Utopia. Yabi Mpakani Na South Korea Ukinyoosha Kidole Kumuonyesha Mwenzako Kuwa Kule Ndo Notth Korea Inaweza Kula Kwako,Eti Kwa Kutishia Usalama. Ndipo Ilipokua Goguryeo Huko.
 
Mengi uongo kama hilonla picha mbona watalii wengi tu wanapiga hata ukiingia mitandaoni utaziona picha zilizopigwa na watu wa kawaida tu mitaani.
 
Kama hiyo no. 6 ni kweli basi naweza kuuona utawala wao kifalme ukienda nchi za mbali na kupotelea huko.
 
hilo LA kunyoa na LA kumiliki usafiri ndio ya kweli lakini yaliyobaki ni real lies
 
Akifa rais wananchi wote wanahudhuria mazishi kivipi sasa? Nafasi inatoshaje?
 
Back
Top Bottom