Korea Kaskazini 'kulipua bomu la nyuklia tena

Morocco forever

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2016
Posts
7,121
Reaction score
6,879
_91161737_mediaitem91161735.jpg

Korea Kaskazini 'kulipua bomu la nyuklia tena'
12 Septemba 2016

Maafisa wa korea kusini wametahadharisha kwamba huenda Korea Kaskazini ikafanya jaribio jingine la bomu la nyuklia wakati wowote, baada ya kutekeleza jaribio jingine la bomu la nyuklia Ijumaa.
Jaribio hilo la Ijumaa lilikuwa kubwa zaidi kuwahi kufanywa na Korea Kaskazini.
Msemaji wa jeshi la Korea Kusini amesema bado kuna shimo la kulipua bomu ambalo halijatumiwa katika eneo la kufanyia majaribio Punggye-ri ambalo linaweza kutumiwa kulipua bomu la sita wakati wowote.
_91077693_mediaitem91077690.jpg

Korea Kaskazini ilishutumiwa vikali na jamii ya kimataifa baada ya jaribio hilo la Ijumaa na hali ya wasiwasi na uhasama imeongezeka.
Marekani yatishia kuiadhibu Korea Kaskazini
Mwanamke maarufu zaidi Korea Kaskazini
Jumapili, mmoja wa maafisa wa jeshi la Korea Kusini alinukuliwa na shirika la habari la taifa hilo Yonhap akisema kwamba nchi hiyo ina mpango wa kuuangamiza kabisa Pyongyang, mji mkuu wa Korea Kaskazini, iwapo kutaonekana dalili kwamba nchi hiyo inajiandaa kutekeleza shambulio la kinyuklia.
Bado kuna shaka kuhusu uwezo wa Korea Kusini kuweka mabomu ya nyuklia kwenye makombora ya masafa marefu, kuiwezesha kutekeleza shambulio, lakini wataalamu wanasema hatua zilizopigwa na taifa hilo zinazua wasiwasi.
Jumatatu, shirika la Yonhap lilimnukuu afisa mmoja wa serikali akisema dalili zinaonesha Korea Kaskazini imekamilisha maandalizi ya kutekeleza shambulio jingine milimani kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Jaribio lililotekelezwa Ijumaa linaaminika kuwa kubwa zaidi kuwahi kutekelezwa na Korea Kaskazini
 
Safi lazima siku moja niende Korea Kaskazini

Naskia wamewekewa vikwazo hadi waweka vikwazo wenyewe wamechoka maana vimeisha vyote na watu hawajali, na Kim Jong Un an onekana ndiye ata kuwa katili kuliko hata baba na babu yake
 
Safi sana kijana wazo zuri,ila jitahidi uende haraka iwezekanavyo...maana Kim Jong anatafuta mchapakazi haswaa wa kureplace ile nafasi ya waziri aliyemdedisha....
 
View attachment 399022

Korea Kaskazini 'kulipua bomu la nyuklia tena'
12 Septemba 2016

Maafisa wa korea kusini wametahadharisha kwamba huenda Korea Kaskazini ikafanya jaribio jingine la bomu la nyuklia wakati wowote, baada ya kutekeleza jaribio jingine la bomu la nyuklia Ijumaa.
Jaribio hilo la Ijumaa lilikuwa kubwa zaidi kuwahi kufanywa na Korea Kaskazini.
Msemaji wa jeshi la Korea Kusini amesema bado kuna shimo la kulipua bomu ambalo halijatumiwa katika eneo la kufanyia majaribio Punggye-ri ambalo linaweza kutumiwa kulipua bomu la sita wakati wowote.
Korea Kaskazini ilishutumiwa vikali na jamii ya kimataifa baada ya jaribio hilo la Ijumaa na hali ya wasiwasi na uhasama imeongezeka.
Marekani yatishia kuiadhibu Korea Kaskazini
Mwanamke maarufu zaidi Korea Kaskazini
Jumapili, mmoja wa maafisa wa jeshi la Korea Kusini alinukuliwa na shirika la habari la taifa hilo Yonhap akisema kwamba nchi hiyo ina mpango wa kuuangamiza kabisa Pyongyang, mji mkuu wa Korea Kaskazini, iwapo kutaonekana dalili kwamba nchi hiyo inajiandaa kutekeleza shambulio la kinyuklia.
Bado kuna shaka kuhusu uwezo wa Korea Kusini kuweka mabomu ya nyuklia kwenye makombora ya masafa marefu, kuiwezesha kutekeleza shambulio, lakini wataalamu wanasema hatua zilizopigwa na taifa hilo zinazua wasiwasi.
Jumatatu, shirika la Yonhap lilimnukuu afisa mmoja wa serikali akisema dalili zinaonesha Korea Kaskazini imekamilisha maandalizi ya kutekeleza shambulio jingine milimani kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Jaribio lililotekelezwa Ijumaa linaaminika kuwa kubwa zaidi kuwahi kutekelezwa na Korea Kaskazini
Me nimefail kuwaelewa hawa jamaa wa NORTH kila siku ni mikwara ya mbu nje ya neti...
 
Hivi ubalozi wao bado upo Tz?, miaka ya Nyerere na wakti huo Babu yake huyu Rais w wa sasa (Kim ill Sung) akiwa raisi wa Korea, walikuwa karibu sana na Wabongo, maana walikuwa na ubalozi na pia walikuwa na kituo cha utamaduni cha watu wa Korea, pale katibu na umoja wa Vijana, walikuwa na masomo ya Muziki na pia walikuwa na senema za vita ya Korea,

Jamaa walikuwa wajamaa Hasa,
 
We
Me nimefail kuwaelewa hawa jamaa wa NORTH kila siku ni mikwara ya mbu nje ya neti...
we uko Bongo umeshashiba wali Maharage unaona jamaa wanapiga Mkwara mbuzi, wenzio wenye kula vizuri na kulala vizuri, sasa hivi hawapati usingizi,
Kile kitu kilichopigwa last week sio mchezo, kikitua sehemu kama Dar, kunabaki history tu, so Wajapan, South Korea, Amerika na wengine sasa hivi wanamwamkia dogo kila asubuhi
 
Mwanaume ndio unatakiwa kuwa hivyo sio vikangaroo vya kiafrika
 
Sio viongozi wetu wana tutisha sisi tuu kwa marekani wana ufyata

Ha ha ha haa na ile issue ya kusitisha msaada kwa serikali yetu ilifikia wapi,baada ya jecha kufanya mambo kule zenji? Naona kama walianza kulialia vile ha ha ha ha
 
Back
Top Bottom