Korea Kaskazini: CIA wanapanga kumuua Kim Jong-un

Jambazi

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
16,644
18,707
Maajenti wa Marekani na Korea Kusini wanapanga njama ya
kumuua kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, vyombo
vya habari nchini humo
vimesema. Taarifa kutoka wizara ya usalama nchini Korea Kusini imesema
mawakala wa kundi la kigaidi linaloungwa mkono na Shirika la
Ujasusi la Marekani (CIA) na shirika
la ujasusi la Korea Kusini wameingia nchini Korea Kusini wakiwa na silaha
hatari ya bio-kemikali. Taarifa hiyo imesema Korea Kaskazini itawasaka mawakala hao na kuwaangamiza bila huruma Korea Kaskazini imesema hayo huku wasiwasi ukiendelea kuongezeka katika rasi ya Korea. Taarifa hiyo, ambayo imechapishwa na shirika la habari la Korea Kaskazini inasema njama hiyo
inahusisha kutumiwa kwa "silaha ya
bio-kemikali pamoja na kemikali yenye miali nururishi na sumu". Matokeo ya shambulio kama hilo
yataanza kubainika baada ya miezi
sita hadi 12..

Source:bbc
 
85b84a50fc7d7820c6b4f8a5988299c3.jpg
711dfd67ee7fdbb3d6fc8b6fccf66cd6.jpg
 
Hii yote aibu anashindwa tu namna ya kurudisha majeshi maana dunia nzima inatupia macho huko akirudisha majeshi tu mataifa mengi yatafanya kama North Korea
Hawahawa North Korea walifanya hacking ya mtandao wa kampuni ya Sony na kuharibu mifumo yao ya kompyuta, kwa kilichodaiwa kwamba Sony walitengeneza game ya PC ya kumdhihaki Kim. Ukifanya ujinga wao wanafnya upumbavu. Habari iko HAPA.
 
Marekani Ana tapa tapa walifikiri kiduku mwaarabu sasa wanaona aibu kurudisha majeshi nyumbani
 
Bush alipotwaa ofisi iliitaja NK kama rogue state[taifa korofi?]
Wakati huo kulikuwa na RSs nyingine kama vile Libya, Afghan, Cuba, Iraq Yugoslavia, Sudan, Syria, Iran na NK iliyoongezwa.

US akaanza kuwashughulikia Afghan, Iraq, Yugoslavia, Libya na Cuba aliyemalizana naye kwa mazungumzo.
Then baada ya kumalizana na Libya [pamoja na Cuba] hivi majuzi akageukia Syria na NK. Syria kakingiwa kifua na Russia hadi leo mfupa umekuwa mgumu kwa fisi.

NK baada ya kuona mwisho wenye machungu kwa Iraq, alijitengenezea silaha za Nuke ili US atakapomgeukia naye aweze kujibu.
Leo hii US hawezi kuigusa NK maana anajua kitakachompata........Inanishangaza kuona US anaomba support ya jumuhia ya kimataifa ili amkabili Kim, mbona hakuomba support alipokabilina na Saddam au Gaddafi?
Bado kuna wanaosema Kim ni mtoto mdogo kwa US?

Maajabu ni kwamba pro-US wanajihamini zaidi dhidi ya NK kuliko US yenyewe.
 
Hawahawa North Korea walifanya hacking ya mtandao wa kampuni ya Sony na kuharibu mifumo yao ya kompyuta, kwa kilichodaiwa kwamba Sony walitengeneza game ya PC ya kumdhihaki Kim. Ukifanya ujinga wao wanafnya upumbavu. Habari iko HAPA.
Khaa
 
Back
Top Bottom