Kontena laanguka barabarani Taa za TAZARA

Kontena laanguka barabarani Taa za TAZARA

trachomatis

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2011
Posts
3,758
Reaction score
746
Kuna foleni ndefu. Angalia njia nyingine ya kupita,maana hata zinazotokea Buguruni haziendi na zinazotokea Temeke pia haziendi. Labda za Airport na za City Center.
 
Duh,,..mkiambiwa dar imejaa mnabisha, na gesi mnataka ije hukohuko...mtajibeba!!
 
Duh,,..mkiambiwa dar imejaa mnabisha, na gesi mnataka ije hukohuko...mtajibeba!!
Waambine hao, tena wakazane kupiga kelele gesi ije Dar, watahamishwa mpaka basi.. Airport walihamishwa kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege, Kigamboni (...), Kinyerezi........... inaonekana jinsi gani hamstahili kuishi mjini.
 
Kuna foleni ndefu. Angalia njia nyingine ya kupita,maana hata zinazotokea Buguruni haziendi na zinazotokea Temeke pia haziendi. Labda za Airport na za City Center.

Acha uongo bana, foleni kwa uzoefu wangu katika njia hii ni kitu ya kawaida kwa siku ya Jumamosi hususani kuanzia mida ya saa nne (4) asubuhi, hata hivyo lori lenyewe halikukaa zaidi ya saa moja. Magari yote yalikuwa yanapita vizuri tu kasoro yale yatokayo Gongolamboto kuelekea Buguruni. Trafiki wamefanya kazi nzuri kuongoza magari.
 
Edmund. Tazama na muda nilioripoti tukio.. Usipende tu kuwa negative.
Mi nilikuwa njiani napita ila kama wewe ni makazi yako hapo Tazara basi ni suala lingine.
 
Last edited by a moderator:
Chum Chang. Nimepiga ila haikutoka vizuri.nilikuwa kwenye daladala.
 
Last edited by a moderator:
Wakilinyanyua lori lililoanguka likiwa na kontena mataa ya Tazara

KONTENA TAZARA.jpg
 
halafu hata mwaka jana lilianguka hapo hapo!
Eeee, yeye hana mpango wa kuangamiza maalbino bali ni budi aangushe kontena lake tu hapohapo kila mwaka. Ndo ushauri wa Dr Manyaunyau huo!
 
Acha uongo bana, foleni kwa uzoefu wangu katika njia hii ni kitu ya kawaida kwa siku ya Jumamosi hususani kuanzia mida ya saa nne (4) asubuhi, hata hivyo lori lenyewe halikukaa zaidi ya saa moja. Magari yote yalikuwa yanapita vizuri tu kasoro yale yatokayo Gongolamboto kuelekea Buguruni. Trafiki wamefanya kazi nzuri kuongoza magari.
Hapo uongo wake ni nini? Kwamba kontena halijaanguka? Au foleni hakuna?
 
Moderators you may now close the thread. Thanks in advance.
 
haya makontena ukipishana nayo moyo huwa unadunda...
 
Mungu mkubwa hapakuwepo gari pembeni ama bodaboda na ni vile muda wenyewe SAA 6 .15 hivi usiku. Yaonyesha hilo semi wakati anazunguka 'keepleft' alikua speed kubwa ikasababisha Container lote 40ft na body kuanguka barabarani na kuiacha cabin ikiwa stable, yaonyesha pia hakukua na madhara kwa Dereva na utingo.

Tutegemee foleni kubwa asubuhi kesho hasa kwa waendao Mbagala.
 
Back
Top Bottom