Kontena la futi 40 lililosheheni meno ya tembo lakamatwa Unguja!

Adrian Stepp

JF-Expert Member
Jul 1, 2011
2,764
2,582
Kontena lenye urefu wa futi 40 lililojaa pembe za ndovu limekamatwa kisiwani Unguja mchana huu likitokea bandari ya Dar es Salaam.

Mpaka sasa haijajulikana mzigo huo una thamani ya kiasi gani na raia wawili wa Tanzania wamekamatwa kuisaidia polisi .

Kwa mujibu wa Waziri Kagasheki, kontena hilo pia linahisiwa kumilikiwa na raia wa China.

Tukio hilo limeshudiwa na Waziri wa nchi tawala za mikoa Zanzibar pamoja na Waziri wa maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki.

Source: Eatv/ Radio

==================
Picha
==================

 
Adrian Stepp embu chunguza kwanza mmiliki wa meli iliyobeba kontena ni nani? Taharifa yako nzuri inaitaji nyama nyama tuone kama kaa mbali na tembo anahusika kivipi.
 
Last edited by a moderator:

Hadi pale ccm itakapoondoka madarakani, na hasa pale katibu mkuu wake Kinana atakapotiwa ndani ndipo tutakuwa na uhakika kuwa tembo wetu watanusurika.

Vinginevyo hadi kufikia mwaka 2015 tutakuwa hatuna tembo hata mmoja kwa spidi hii wanayoendelea nayo ya kuwaua tembo wetu.

Huu ushirika wa ccm na wachina ndio umezidi kutumalizia tembo wetu kwahiyo tunatakiwa tuwatimue nchini wachina kama hatua ya kwanza ya kuwanusuru tembo wetu kabla ya kuwatimua madarakani ccm 2015.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…