Kongamano la Siku Ya Uhuru UDSM Dec 9

matasha

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
378
0
UNIVERSITY OF DAR ES SALAAMAcademic Staff Assembly


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tunapenda kuwajulisha kuwa Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) kwa ushirikiano na IPP Media wameandaa Kongamano tarehe 9 Desemba 2012 ndani ya Ukumbi wa Nkrumah kuanzia saa 8 mchana hadi saa 12 jioni. Mada kuu ya Kongamano ni, “Uhuru wetu na Mustakabali wa Taifa kwa Miaka 50 Ijayo”. Vipengele vya mjadala ni: a) Amani na Utulivu wa Taifa letu kwa Miaka 50 Ijayo;b) Elimu na Maendeleo ya Taifa kwa Miaka 50 Ijayo; c) Rasilimali zetu kwa Maendeleo ya Kiuchumi ya Taifa. Kongamano hilo litarushwa moja kwa moja na ITV, Radio One na Capital Radio. Wote mnakaribishwa kufuatilia mjadala huo. Wazungumzaji watakaongoza mjadala ni Bw. Maggid Mjengwa, Prof. Gaudence Mpangala, Dkt Martha Qorro, Dkt Kitila Mkumbo, Dkt Haji Semboja, na Mhandisi Joshwa Raya. Watakuwepo pia wazungumzaji waalikwa kama vile: Joseph Butiku, Dkt Aldin Mutembei, Julius Mtatiro, January Makamba, Usu Mallya na Esther Wassira. Wote mnakaribishwa Limetolewa na Uongozi wa UDASA
 

Wa kusoma

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
3,456
2,000
Safu iko powa nitakuwa live Luningani. Mbona Ulimwengu na Kubenea siku hizi kimya?
 

Az 89

JF-Expert Member
Nov 20, 2011
1,661
2,000
Hahaa imekaa njema sana nasubiria hu mtanange jumapili kwa hamu sana
 

Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,050
2,000
Ahsante kwa kutujuza, nitaungana na wafuatiliaji wengine kujua kitakachoendelea.
 

kijereshi

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
379
500
Dah hii safi sana maana mijadala kama hii ya fikra huru ilikuwa ishapotea kitambo pale mlimani.
 

Root

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
43,553
2,000
Sisi wengine tulio mbali na TV zetu tunaomba tupewe updates za kinachoendelea siku hiyo
 

cabhatica

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
1,078
1,500
Asante kwa taarifa. Ombi langu journalists watakaohudhuria wawe objective kuripoti yatakayojiri kwa mustakabali wa taifa, waweke ushabiki na itikadi pembeni. Editors nao wazipe habari hizo uzito unaostahili. Tanzania Kwanza.
 

Bishweko

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
3,024
2,000
Uhuru wa Nchi gani hiyo? ebu nyie wasomi mtwambie ukweli bwana hhhaa!
[FONT=Times
New Roman] [/FONT]
[FONT=Times
New Roman]UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM[/FONT]
[FONT=Times New
Roman]Academic Staff
Assembly
[/FONT]​
[FONT=Times
New Roman][/FONT]


[FONT=Times New
Roman]TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
[/FONT]
[FONT=Times New
Roman] [/FONT][FONT=Times New
Roman] [/FONT][FONT=Times
New Roman]Tunapenda kuwajulisha kuwa Jumuiya ya
Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) kwa ushirikiano na
IPP Media wameandaa Kongamano tarehe 9 Desemba 2012 ndani ya Ukumbi wa
Nkrumah kuanzia saa 8 mchana hadi saa 12 jioni. Mada kuu ya Kongamano
ni, “Uhuru wetu na Mustakabali wa Taifa kwa Miaka 50 Ijayo”.
Vipengele vya mjadala ni:
[/FONT]
[FONT=Times New
Roman]a) Amani na Utulivu wa
Taifa letu kwa Miaka 50 Ijayo;
[/FONT][FONT=Times New
Roman]b) Elimu na Maendeleo
ya Taifa kwa Miaka 50 Ijayo;
[/FONT][FONT=Times New
Roman]c) Rasilimali zetu kwa Maendeleo ya
Kiuchumi ya Taifa.
[/FONT]
[FONT=Times New
Roman]
[/FONT][FONT=Times New
Roman]Kongamano hilo litarushwa moja kwa moja na ITV, Radio One na
Capital Radio. Wote mnakaribishwa kufuatilia mjadala huo. Wazungumzaji
watakaongoza mjadala ni Bw. Maggid Mjengwa, Prof. Gaudence Mpangala, Dkt
Martha Qorro, Dkt Kitila Mkumbo, Dkt Haji Semboja, na Mhandisi Joshwa
Raya. Watakuwepo pia wazungumzaji waalikwa kama vile: Joseph Butiku, Dkt
Aldin Mutembei, Julius Mtatiro, January Makamba, Usu Mallya na Esther
Wassira. [/FONT]
[FONT=Times New
Roman]
[/FONT]Wote
mnakaribishwa
[FONT=Times New
Roman] [/FONT][FONT=Times New
Roman]
[/FONT][FONT=Times New
Roman]Limetolewa na Uongozi wa UDASA[/FONT]
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom