Kondomu kujaa na kuziba mitaroni!

Kaka Pekee

JF-Expert Member
Apr 3, 2018
336
559
Nimepita baadhi ya Vichochoro hapa Mitaa ya Manzese Mitaro Inaonekana Imeshiba hadi kurudisha Chenji huku asilimia kubwa ya Unavyoweza kuviona pembezoni au ndani ya Maji hayo vikielea ni Mipira ya Kiume (Kondomu). Hii ikanikumbusha siku niliyomuona mtoto mmoja akipuliza Kondomu kama Puto...Nilikuwa kwenye Daladala vinginevyo hakyanani ningemuuliza amepata wapi kisha ningewalamba vibao wahusika wa eneo hilo!

Aneweiii...To cut the Story Short!

1.) Nimefurahishwa na Hamasa ya WANAUME Wenzangu kujitambua na kupiga Soksi kabla ya Mechi Ila tujitahidi basi kufunga vizuri kwenye Karatasi / Toilet Paper kabla ya Kutupa.

2.) Kuna Umuhimu wa Jamii kupelewa Darasa Elekezi la namna bora ya Kutupa (Waste Disposal)ya Kondomu ili kuepusha utupaji hovyo...au ikibidi Kuweka Mapipa ya Taka Hatarishi Mtaani kwenye Viunga ili Iturahishie au Iwarahishie wenye Magesti kutupa humo kwa usalama wa watoto na Afya Zetu!
1565941824383.png
1565941683389.png
1565941769241.png
 
Saikolojia ya macho kuprosesi kile unachoona inasema, mara nyingi mtu huona kile anachopendelea zaidi kuona. Kwa mfano, unaweza kupita sehemu, usione mambo mengi zaidi ya nyumba nzuri na wanawake wanarembo. Ukiambiwa kulikuwa na nyumba mbovu na wanaume unakataa kwasababu haukuwaona/haukuviona
 
Hujakosea Nafurahishwa sana na Kuona Zana zikitumika ila pia macho huzunguka kuangalia Wadada Warembo kisha huwa nawapa rates kichwani. Ila nikiona mrebo zaidi najaribu kete yangu. ;)
 
Wataalam wa mazingaombwez hebu Mshana Jr tupe ujuzi, mtaalamu akichukua hizo manii anaweza kufanyia nini?
 
Back
Top Bottom