huyo ni mkweli ila kuna mwingine juzi (ila yeye dreva wa dalala) alinifurahisha sana maana alikuwa anaendesha gari bovu huku analalamika kuwa tajiri yake hamsikiii akimwambia mafundi wanamzinguwa kwani hawatengenezi kari viruzi na tajiri anamwambia wewe (yaani suka) aongee vizuri na mafundi. Abiria mmoja mama akamwambia kwanini sasa usimwachie huyo tajiri gari kama hakusikilizi? Yule dreva alimwambia "nikililiacha tu hili gari hata kama ni bovu wewe jioni giza likishaingia hukatizi uchochoroni, hivyo bora nibangaize na hili gari bovu kuliko kwenda kupiga watu roba mtaani"