Kombinesheni ya mhe. Freeman mbowe na dr.slaa ni tishio | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kombinesheni ya mhe. Freeman mbowe na dr.slaa ni tishio

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbelwa Germano, Oct 7, 2012.

 1. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Katika mpira wa miguu kombinesheni ya wachezaji ni muhimu sana katika kuleta ushindi. Fomesheni, nidhamu na uwezo wa wachezaji ni baadhi ya mambo ya ziada.

  Kwa washabiki wa mpira wa miguu wanakumbuka washambuliaji mahiri kama Dwight Yorke na Andy Cole ambapo kombinesheni yao ilikuwa tishio kwa timu pinzani, ndivyo ilivyo kwa Mh.Freeeman Mbowe na Dr. Willbroad Slaa katika uwanja wa siasa kama viongozi wa juu kabisa wa chama kikuu cha upinzani nchini. Ushirikiano wao ni ishara ya ushindi.

  Tunakumbuka wakati Ronadihno yupo Barcelona alikuwa anatumika kama mchezaji huru kutokana na staili yake ya uchezaji na kipaji kikubwa cha kupenya ngome ya timu pinzani. Hapa ndipo Mh. Zuberi Zitto Kabwe anapojitambulisha kama mwanasiasa mwenye kipaji (talented politician) akitumia ujuzi na akili kupenya ngome ya mpinzani. Kwa kizungu naweza kusema, a talented politician with agility. Japokuwa zipo hisia kwamba utambulisho huu unaweza kudhoofisha nguvu ya ushindi bado mchango wake ni wa muhimu sana katika chama.

  Aidha viungo washambuliaji ni muhimu sana katika kuunganisha timu na kupeleka mashambulizi. Umahiri wao unafanya wapinzani wao kupandwa na jazba na kuzungumza maneno ya ovyo. Umahiri wa Tundu Lissu, John Mnyika na Halima Mdee ni changamoto kwa timu pinzani na ishara ya ushindi. Ukiwa na viungo washambuliaji wa ziada kama Godbless Lema, Joseph Mbilinyi na Vicent Nyerere huwezi kuwa na wasiwasi na majeruhi katika timu ya ushindi.

  Kama kuna changamoto kubwa ya kuimarisha kikosi cha ushindi basi ipo haja ya kuangalia mabeki au ngome ya timu. Hapa ndipo naikumbuka timu ya Taifa ya Djibuti. Hapa ndipo wanasiamama Bavicha na Bawacha. Ukitafakari vizuri na kuweka ushabiki pembeni utagundua ni kwa jinsi gani ngome (defence) ya timu bado haijakaa vizuri na kusababisha washambuliaji kurudi nyuma na kufanya kazi ya kulinda (defensive role). Umakini na ufanisi wa ulinzi bado ni changamoto.

  Benchi la ufundi (technical bench) yaani kurugenzi za chama bado ni changamoto. Ipo haja ya kujitathmini upya na kujiongezea uwezo ubunifu (creativity) ili kujenga mbinu imara za ushindi na kutambulisha CDM kuwa chama imara zaidi.

  Wapo ma-nahodha(Captain) wa timu ambao wanapaswa kutumia uwezo na uzoefu wao kujenga timu imara. Hawa katika siasa naweza nikawaita viongozi mikoani ambapo kwa nafasi zao wanapaswa kuhakikisha kwamba sauti ya mabadiliko inafika hadi vijiji vya kule Ngwelo, Malibwi na Makanya walayani Lushoto.
   
Loading...