Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC): Simba SC 2-3 Mashujaa FC | Uwanja wa Taifa, Dar es salaam | 26/12/2018

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Mabingwa wa Nchi, Simba SC, baada ya kuwafurusha vilivyo Nkana FC kutoka nchni Zambia kwa mabao (4-3 ) kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, leo inaingia kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kupepetana na Klabu ya Mashujaa FC kutoka mkoani Kigoma, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC).

Kupitia kwa Mkuu wa kitengo cha Habari wa klabu ya Simba SC , Haji Manara amesema hawataidharau timu ya Mashujaa FC, kwani Viongozi pamoja na Wachezaji wanalitambua hilo kwa vile yasije yakawakuta kama ya Green Worriors, kwahivyo wamejiandaa kuhakikisha wanaibuka na ushindi maridhawa.

Je Mashujaa FC wanaweza kumzuia Mnyama Mkali, Lunyasi, asiweze kuibuka na ushindi? Usibonye kitufe..Kumbuka mchezo ni saa 10: 00. Usikose Ukaambiwa.

IMG_20181226_153107_123.jpeg


Mshindi katika michuano hii ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports ASFC, anaungana na bingwa wa TPL kuiwakilisha nchi katika michuano ya Kimataifa.

Kuanzia sasa mpira utaanza uwanja wa Taifa, Kombe Shirikisho la Azam Sports ASFC

00' Naaaaaaaam mpira unaanza uwanja wa Taifa, dakika 90' za mchezo.

Simba SC 0-0 Mashujaa FC

3' Simba wanalifikia lango la wapinzani kwa mchezaji Zana kupiga Krosi ambayo golikipa anadaka

5' Mashujaa FC wanajibu shambulizi kwa mchezaji Mohamed kupiga shuti upande wa kulia. Lakini mpira unatoka nje na kuwa goal kick

10' ASFC, uwanja wa Taifa hakuna timu imepata bao pamoja Simba kufika mara kwa mara lango la Mashujaa FC

Simba SC 0-0 Mashujaa FC

15' Huku kila timu ikijaribu kutafuta ushindi, Simba wanatawala nafasi ya katikati ya uwanja.

18' Gooooooooooaaal Gooooooaaal

Mlinzi Paul Bukaba anaipatia Simba bao la kwanza

Simba SC 1-0 Mashujaa FC

20' Simba wanakwenda katika lango la Mashujaa, lakini washambuliaji Salamba, Abdul Suleiman wanashindwa kutumia nafasi wanazopata

Mashujaa wajibu kwa uchache sana mashambulizi

30' ASFC, uwanja wa Taifa Simba bado wako mbele ya goli moja dhidi ya Mashujaa.

Simba SC 1-0 Mashujaa FC

40' Mchezaji jezi namba 10 wa Mashujaa anashindwa kutumia vema nafasi ya wazi kuandika bao..Hivyo mpira kutoka nje na kuwa goal kick

Kuelekea mapumziko Kombe la Shirikisho la Azam Sports

45+2' Wakati wowote mpira utakuwa mapumziko

Naaaaaaaam mpira ni mapumziko kipindi cha kwanza Simba wanatoka wakiwa mbele ya goli moja dhidi ya Mashujaa FC.

Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Taifa

47' Gooooooooooaaal Mashujaa FC wanasawazisha bao

Simba SC 1-1 Mashujaa FC

Washambulizi lango la Simba, yanazidi lolote linaweza kutokea

Gooooooooooaaal Mashujaa FC wanapata goli la pili

Simba SC 1-2 Mashujaa FC

68' Ametoka Abdul, ameingia Cleoutus Chama

Ametoka Juma ameingia Mohamed Ibrahim Mo, upande wa Simba SC

Mashambulizi wanapanga upande wa Simba lakini mpira unaokolewa na mabeki wa Mashujaa FC

Yassin anakwenda kwenye benchi anaingia Kotei

80' Gooooooooooaaal..Free kick ya Chama inapigwa na kugonga mwamba na Mo kumalizia

Simba SC 2-2 Mashujaa FC

85' Kwasi anakosa bao la wazi..ilikuwa hatari sana lango la Mashujaa FC

90+7' kuelekea kumalizika kwa mpambano uwanja wa Taifa ASFC

Gooo goooaal..Makosa ya golikipa Munishi kushindwa kuudaka mpira wa kimo cha kuku inaipatia Mashujaa FC bao

Simba SC 2-3 Mashujaa FC

Naaaaaaaam mpira umekwisha uwanja wa Taifa ni michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports ambapo Mashujaa FC wameibuka na ushindi

Simba SC 2-3 Mashujaa FC

Asanteni....Ghazwat....
 

Attachments

  • IMG_20181226_143714_741.jpeg
    IMG_20181226_143714_741.jpeg
    36.4 KB · Views: 53
Back
Top Bottom