Kombe la Kagame: TFF ya Jamal Malinzi yanukia rushwa ya siasa

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,250
15,116
Mnamo tar 18/07/2015 Jumamosi, wapenzi wa tasnia ya mpira wa miguu wanapata nafasi nyingine ya kushuhudia mashindano makuu ya Afrika Mashariki.

Ili kupamba ufunguzi huo, shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) liliamua kufanya Maamuzi ambayo tunaweza kuyaita ya "Kipuuzi".

Kitendo cha kumleta mgeni rasmi wa michuano hiyo ambaye ni mmoja wa wanao wania urais kupitia ccm si cha kiungwana kabisa. Tunajua kwamba TFF wanadai kuwa wamemleta kwa kofia ya uwaziri..! na wanajua wazi kwamba wapenzi wa soka hapa nchini ni wenye itikadi "mbalimbali za kisiasa ".

Kwa taarifa zinazosikika sasa hivi ni kwamba "sherikaly" imeamua kutumia michuano hii ili kumpatia mgombea huyo recognition ya ziada.
Inadaiwa kuwa Kufanikisha hilo tukio, [TI°EF°EF] ilipokea kiasi fulani cha "$$$$DOLLARI$$$$" .. ili kuruhusu ujinga huo kufanyika...

Bila kuzingatia misingi ya mchezo wakaruhusu hili suala lifanikiwe.
Binafsi kama mdau mkubwa sana wa mchezo wa mpira wa miguu sikupendezwa na "Upenyezo wa siasa kwenye tasnia yetu" kabisa.

Huyu jamaa anaye jiita Jamal Malinzi... sioni kama anamalengo marefu na mpira wa tanzania. Rai yangu kwake ni kwamba ajiangalie sana, yeye ni kiongozi na yampasa asimame imara katika kiti chake.
Anapo fanya kinyume na hapo basi anapeleka mchezo huu kusiko kulikana.

#KataaRushwa JM.
 
Nilihisi tu.

Huyu mtia nia sijui mgombea hajawahi kabisa kuwa na shobo na Soka, iweje leo aalikwe. Ujinga kama huu dawa yake ni kususia tu...
 
Mphamvu

Lengo Kuu ni kutumia kadamnasi ya CECAFA Kagame cup kutimiza malengo yao ya Kisiasa.

Huyu Jamali Malinzi ni bogaz kwelikweli yaani linapenda pesa sana, wakati vitu kama hivi ndio vina tenganisha wapenzi wa soka kabisa.
 
Last edited by a moderator:
nliwaambia ninyi kuwa JAMAL MALINZI Ni JANGA LINGINE KWENYE SOKA LETU... wengi hamkutaka kufungua macho. mimi ni CCM lakini siungi mkono uhuni huu wanaofanya watu ambao wamekabidhiwa majukumu ya Kitaifa wao kuyafanya ya ki chama au kisiasa. Wananchi wasusie mashindano hayo.
 
Kila kitu Tz ni siasa tu whether you like or dislike it
 
Nadhani TFF, sasa wanataka kuharibu taswira ya mpira wa miguu nchini, na huyu MALINZI, nadhani anataka kutumia hii tff kama jukwaa la kujinadi kisiasa, kwani kuna kipindi alikwenda kujitambulisha ofisini kwa LOWASA!! ili kesho na keshokutwa anaweza kupata ubunge. Lakini si sawa
 
Back
Top Bottom