Kombani & Makamba VS Bomani, Manento, Warioba, Ramadhani, Shivji, & Tendwa

Tasia I

JF-Expert Member
Apr 21, 2010
1,223
193
Wandugu. kama vugu vugu la kudai katiba mpya linavyozidi kuchukua kasi mpya kila siku, huku wananchi, taasisi za umma na binafsi, pamoja na wasomi wakizidi kutoa maoni yao(wengi wakitaka katiba mpya) juu ya haja ya kuundwa katiba mpya, mimi binafsi nilisikitishwa sana na mtizamo wa waziri wa katiba (Kombani), na katibu wa CCM (Makamba) walioonesha kutoona haja ya kuwepo katiba mpya.

Hivi katika hali ya kawaidatu, kitu kinachoungwa mkono na wanchi (karibu wote), na pia wasomi na watu wenye influence ktk jamii kinaweza kua potofu kweli?? je hii haitoshi kuthibitisha sana kua kombani hana nia njema na nchi??

Naulizatu nipate kujua zaidi!
 
Kombani anachojali ni mkono wake unaenda kinywani. kwake yeye wanaodai katiba mpya should go to hell! Makamba is an outdated human remnant. Hawezi kuwa na jipya na sijui kwa nini chama kama ccm wanaweza kuvumilia kuwa na katibu mhafidhina kama yule katika ulimwengu wa kisasa. aibu!!!!
 
Ukweli ubaki kuwa ukweli tu, kinachojitokeza na kujidhihirisha hapo ni UBINAFSI uliokithiri hasa wa viongozi wetu kukosa utashi wa kuangalia maridhio ya wanyonge, kwa sababu haijengi wala kuleta taswira katika misimamo ya viongozi kutotaka KATIBA inayolingana na mahitaji ya WATANZANIA ili kukabiliana na UMASIKINI, UJINGA, MARADHI NA UHURU USIO NA USAWA.

Wale wanaong'ang'ania katiba isibadirishwe wanayo ajenda yao ya kibinafsi na inayotaka UHURU USIO NA USAWA uendelee kuitesa jamii yetu ya kitanzania, zaidi wanajilinda waendelee kututawala kama staili ya wakoloni ya kutaka kukaa madarakani milele kitu ambacho ni UKIUKWAJI MKUBWA WA HAKI ZA BINADAMU,
Kikubwa wasisahau ila wanaweza kujiuliza kwa nini wanaotoa miongozo mizuri ya KATIBA wanaungwa mkono na wanazuoni na wasomi wengi zaidi,

NAOMBA SANA KAMA VIONGOZI WA TANZANIA WAJIFIKIRIE MARA MBILI LAKINI WAWAFIKIRIE ZAIDI WANANCHI WANYONGE NA WENGINE WANAOTAKA HAKI NA UTU ILI KULIJENGA TAIFA LETU KATIKA MISINGI YA HAKI, UWAJIBIKAJI, NA USAWA KUEPUKA MIGONGANO MBELE YA SAFARI.
 
Back
Top Bottom