mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,771
- 7,138
Wana JF,
Akiwa kwenye mpambano mkali kwenye uwanja wa vita, Mabwenyenye wamejaribu makombora mengi kupitia kwa vibaraka wao , lakini safari hii wameonekana kuchoka kwani mbinu wanazozitumia kwa kumwaga pesa kila sehemu ili watumie mamluki kupunguza nguvu za komando John lakini wamekutana na vikwazo lukuki kwani hawakubaliki tena, hii vita ya kukomboa fikra za wana CCM ambao ni mateka watiifu wa mabwanyenye ambao walitekwa baada ya kifo cha Jemedari Mwl Mkuu wa taifa hili ambaye alikuwa akiwaponda kichwa kila walipokuwa wakionekana kunyemelea vitu vizuri vya wanyonge.
Mabwanyenye wameteka mabasi UDA, wameteka shehena za vyakula, na njia zote za usafiri ili kudhoofisha Komando John lakini kwa sasa watarudisha majeshi nyuma na kusurrender kwa makombora ya kisasa.
Tanzania tunahitaji sana njia alizozitumia Rais wa Russia Puttin kushinda vita hii ya mwabwanyenye maana ilikuwa sio ya kitoto. Baadhi washaamisha pesa zao nje ili wakimbie.
Vita ya mabwanyenye ni mbaya kuliko ya wauza sembe, kwa sababu watumia sembe wanaweza kugoma kutumia baada ya kufundishwa madhara yake lakini ya hawa mabwanyenye wameteka kila kitu, kunahitaji njia mbadala kuwamaliza nguvu na kuheshimu taratibu za nchi, hawa ukiwahita kwenye unyonyaji wamo, ukiwahita kwenye dhuluma wamo, ukiwaita kwenye kukwepa kodi wamo, hawa ambao hawazidi kumi, inabidi kumwombea commando John asimame kidete kushinda vita hii.