Jana katika hali ya kushangaza watumishi wa Halmashauri wa Ilemela wakiongozwa na Mkurugenzi wao Ndugu Wanga waliwafungia wafanyabiashara wa Vibanda vya Stendi ya Buzuruga kisa kwa kutolipa Tshs.200,000 kwa mwezi.
Kwa mtu mwenye akili timamu kodi ya Tshs.200,000 kwa mwezi haiwezekani hata kidogo. Pale Stendi ya Buzuruga wengi wa wafanyabiashara wanaganga tuu njaa hawana mapato ya kulipa Tshs.200,000 kwa mwezi. Waliwaomba walipe Tshs.40,000 kwa mwezi Halmashauri ikagoma. Wafanyabiashara wanalipa kodi nyingi sana kama Leseni Tshs.150,000 kwa mwaka, Tshs.400,000 kodi ya mapato kwa mwaka, usafi,mabango etc.
Halmashauri isilete chuki baina yake na wananchi na hii itapelekea Serikali ya CCM kuchukiwa na wananchi na kuja kukosa kura 2020. Nashauri walipe angalau Tshs.40,000 kwa mwezi. Mhe. Mbunge hao ni wapiga kura wako nakushauri ufuatilie hili jambo usije ukakosa kura bado tunakuhitaji.