Kodi ya tra na bandari kwajumla

Kodi ya tra na bandari kwajumla

amate

Senior Member
Joined
Feb 23, 2017
Posts
157
Reaction score
378
Habari za Jioni WanaJF,

Napenda kuwashukuru wanaJF kwaajiri ya michango yenu mbalimbali hapa kwenye forum ya kitanzania na East Africa kwa ujumla, pia Napenda kuiambia jamii ya kitanzania kuwa kuna elim kubwa inatolewa kila sku hapa na mafunzo yasiyohitaji kwenda darasani.

My Sincere Point, Nahitaji maelezo kuhusu procedures, Mda ambao kontena linakaa, Malipo ya kodi na kiasi cha malipo wakati umefikisha kontena la bidhaa kutoka nje ya nchi. Aina ya bidhaa ikiwa kama spare parts za pikipiki kutoka china au Dubai.

Nahitaji msaada wenu ili nipate kujua, pia iwe elim kwangu juu ya nchi yangu.
Asanteni sana, Mungu awabariki
 
Ili ufanye clearance ya mzigo wako unahitaji documents kama Bill of Lading, Commercial Invoices na Packing List. Hapa usisahahu pia documents kama Permits na CoC kwa bidhaa ambazo ziko regulated na TBS.

Ukileta container lako unapewa muda wa siku saba (7) bila kulipia storage charges, zikizidi hizo utaanza kulipia storage charges kwa kila siku kutegemea na ukubwa wa container lako au CBM ya mzigo wako. Lakini hii haiondoi charges kama wharfage ambayo inachajiwa kwa 1.6% ya gharama ya mzigo wako (CIF) pamoja na Port Handling charges na Corridor Levy.

Kuhusu kodi inategemea na aina ya bidhaa unayoingiza na gharama zake (CIF). Charges nyingine ni kama Delivered Order charges ambayo inatozwa na shipping line, Container Deposit ambazo hizi zote zinategemea ukubwa wa kontena. Lakini pia ongeza gharama za usafiri wa kontena mpaka ofisini/godown kwako pamoja na gharama za kumlipa wakala wa forodha (clearing agent) ambaye atakutolea mzigo wake.

Kwa maelezo zaidi niandikie trinitytanzania@gmail.com ili tufanye biashara.
 
Back
Top Bottom