Kodi ya ACACIA yapungua asilimia 45

Kodi ya ACACIA yapungua asilimia 45

Una akili za kuambiwa na wewe umejiongezea za kwako. Mimi sijawahi kuhofia rioting ya Tume. Hao ACACIA ingekuwa Ike taarifa Prof. Mruma ni ya uongo wangelazimisha Tume huru kupima tena hayo makinikia lakini hawana haja ya kupima tena maana wanaogopa itawaumbua zaidi.
Wahenga walisema, ukiwa muongo usiwe msahaulifu.

Hawa ACACIA wanatuambia uongo halafu wanasahau kama walisema uongo.

Wanadai makanikia hayana mapato mengi halafu hapo hapo wanadai wamepoteza zaidi ya asilimia 45 ya mapato kwa sababu ya kutouza makanikia.

Kwa mantiki hii, mapato ya makanikia ni nusu ya mapato yote ya dhahabu wanazouza.
 
Huyo Mkurugenzi atulie maana mzigo upo pale Bulyanhulu haujaondoka,makubaliano yatakapofikiwa watapata hiyo pesa ya ushuru wanaoudai.
 
tangu wamelipwa hao watu wa halmahsauri wamefanya maendeleo gani hasaa??......watulie waache mwenye nchi afanye maendeleo
 
Uyu mkurugenzi anafaa kutumbuliwa maana uwezo wake wa kufikiria umefika kikomo. Yaani baada ya kutafuta vyanzo mbadala anangangana na chanzo kimoja tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaelewa maana ya kodi ya huduma?

Hiyo ni 0.3% ya production. Ulitaka watoe kiasi gani baada ya kulipa 30% corporate tax na 4% on production royalty?

Watanzania wengi ni hopeless kabisa. Wanaenda shule kujifunza kutengeneza sentensi za kiingereza lakini siyo kukuza analytical thinking.
Iam not stupid, najua ninachokiandika!Huyo DED ana complain indirectly kukosa mapato ya kodi ya huduma, anasahau picha kubwa kama nchi!Wao kupoteza kiasi hicho kwa miezi isiyozidi 5 wanajua serikali kuu inapoteza kiasi gani???Stupidity to the highest degree, you cant sacrifice a little for bigger achievements??
 
Kabla ya kulaumu ni vizuri ungejiuliza hiyo pesa ndio total amount of money to the government au hiyo ni sehemu tu ya pesa itolewayo kwa halmashauri? Na je formula pia ikoje? NI wao wanaamua cha kutoa au ipo kanuni maalumu ya kutolea and again kama ipo kanuni maalumu, je hi kanuni imeanza lini na kwanini? Vinginevyo kama umeuelewa vizuri uzi is like huo uongozi wa halmashauri (mkuu wa wilaya na huyo mwingine) ni kama wana laumu indirect hatua ya serikali kwa hatua zilizo chukuliwa dhidi ya huo mchanga. Soma tena utaona hapo.
Nimeelewa vivyo hivyo mkuu, yaani DED analamika kupoteza tujimilioni wakati nchi inapoteza mabilioni na bado JPM amekomaa tu!aina hii ya viongozi ndio huuza nchi wakati wa njaa
 
Miradi gani wakati hamna maji wala barabara? Hata mirai ya rea hakuna
 
Kwa hiyo makanikia yana mapato zaidi ya asilimia 45?

Kama tukikubali kuwa makanikia yana mapato zaidi ya asilimia 45 ya kodi ya huduma, kwa nini tukatae figure za tume ya Rais ambazo zinatoa mwelekeo wa mapato kama yanavyobainishwa.

Madai yanayotolewa na ACACIA yanafanya waonekane wana makosa (incriminate) kwa kusema viwango kidogo halafu hapo hapo wanadai mapato yao yamepungua kwa zaidi ya asilimia 45 kwa sababu ya kuzuiwa kuuza makanikia.
Tatizo kila mtanzania anajifanya mjuaji na kutaka kujibu kila hoja hata zile wasizo na elimu nazo!!!
Wew kaa kimya kuliko kuandika huu upuuzi!
Hujui hata ulichokiandika,jisome vizuri kama hutatambua ujinga wako then wewe ni kilaza sana!
 
Unaelewa maana ya kodi ya huduma?

Hiyo ni 0.3% ya production. Ulitaka watoe kiasi gani baada ya kulipa 30% corporate tax na 4% on production royalty?

Watanzania wengi ni hopeless kabisa. Wanaenda shule kujifunza kutengeneza sentensi za kiingereza lakini siyo kukuza analytical thinking.

Tena royalty sasa ni 6% na clearing Fee 1% hivyo ni 7%. na hivyo ya halmashauri 0.3% na tena 30% ya faida.
 
Kodi ya huduma inayotolewa na Mgodi wa Dhahabu wa ACACIA Bulyanhulu kwa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita imepungua kwa zaidi ya asilimia 45 kutokana na Serikali kuzuia usafirishaji wa mchanga (makinikia) kwenda nje ya nchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Carlos, Gwamagobe amesema kupungua kwa mapato yatolewayo na ACACIA itaathiri bajeti kwasababu wanategemea mwaka wa fedha 2017/18 kukusanya zaidi ya Sh800 milioni kama kodi ya huduma kutoka katika mgodi huo.

“Kushuka kwa mapato haya yataathiri bajeti yetu kwakuwa kuna miradi haitatekelezwa mwaka jana tulizielekeza kwenye sekta ya elimu sasa inabidi juhudi za makusudi zifanyike fedha hizi zilikua zikitusaidia sana kwenye miradi ya maendeleo na miradi ya kijamii,”amesema Gwamagobe.

Amesema halmashauri hiyo imefanikiwa kujenga madarasa 12 ya shule ya msingi, manane ya shule za sekondari na kujenga hosteli ya Shule ya Sekondari Kakola pamoja na kujenga ghala la kuhifadhia chakula.

Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale, Hamimu Buyama amesema kodi ya huduma inayotolewa na ACACIA imesadia kusukuma maendeleo ya halmashauri hiyo na kusema katika maendeleo lazima ziwepo changamoto kama zilivyowakuta ACACIA sasa.

Amesema suala la makinikia limekua kikwazo kwa kampuni lakini pia kwa halmashauri zinazotegemea kodi ya huduma kutokana na mapato kushuka na kusema anaimani suala hilo litafika mwisho mwema na wao kuendelea kufanya kazi kama ilivyokuwa awali.

Akikabidhi hundi kwa uongozi wa Wilaya ya Nyang’wale Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa ACACIA Bulyanhulu, Grahama Crew amesema kwa kipindi cha miezi sita iliyopita kodi ya ushuru wa huduma ni zaidi ya Sh687 milion ambazo zimegawanya katika Halmashauri ya Msalala iliyopata asilimia 67 na Nyang’wale iliyopata asilimia 33.

Amesema kuanzia mwaka 2000 hadi sasa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu umelipa zaidi ya Sh10.2 bilioni kama kodi ya huduma katika maeneo wanayofanya kazi ambapo amesema ni matarajio yao kuendelea kuimarisha sekta ya viwanda kwenye uchimbaji wa madini katika Wilaya ya Nyang’wale.

Akizungumza katika makabidhiano hayo mbunge wa Nyang’wale, Hussein Nassoro amesema wananchi wa Nyang’wale wanauhusiano mzuri na kampuni, lakini bado wanamahitaji makubwa.

Amesema wilaya hiyo bado iko nyuma katika sekta ya elimu, afya na miundombinu ya barabara na kuiomba kampuni hiyo kuendelea kuisaidia huduma za kijamii kwa wananchi ili waweze kuona faida ya uwekezaji katika maeneo yao.

Chanzo: Mwananchi
Huyu naona anajifungulia mlango wa kutokea.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndizo gharama zenyewe hizo za kukurupuka
 
10.2 billion Tzs. Ni sawa na $5m kwa miaka 16 hii ni peanuts tu.

Sent from my iPhone 8 using JamiiForums mobile app
 
tangu wamelipwa hao watu wa halmahsauri wamefanya maendeleo gani hasaa??......watulie waache mwenye nchi afanye maendeleo
Kweli kabisa tena yafukuzwe kabisa.
Kwanza kama zinawatosha wangewaambia wawajengee nyumba za makazi wafanyakazi wote kwa gharama nafuu kabisa
 
Kwa hiyo makanikia yana mapato zaidi ya asilimia 45?

Kama tukikubali kuwa makanikia yana mapato zaidi ya asilimia 45 ya kodi ya huduma, kwa nini tukatae figure za tume ya Rais ambazo zinatoa mwelekeo wa mapato kama yanavyobainishwa.

Madai yanayotolewa na ACACIA yanafanya waonekane wana makosa (incriminate) kwa kusema viwango kidogo halafu hapo hapo wanadai mapato yao yamepungua kwa zaidi ya asilimia 45 kwa sababu ya kuzuiwa kuuza makanikia.
Mkuu ACACIA walisema mapato yao nusu(50%) inatoka kwenye makinikia na 50% kwenye matofali ya dhahabu muda mwingi sana.. sana linapokuja swala la malipo watu wakisikia kodi imepungua wanaanza kushangaa
 
Miaka yte hyo ndio wamejenga madarasa 12 mbona kna hlimashauri hazipati hla kutka kwenye migodi na zna fnya vzuri hao viongizi wa hyo halimashauri itakuwa ni wez hao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo makanikia yana mapato zaidi ya asilimia 45?

Kama tukikubali kuwa makanikia yana mapato zaidi ya asilimia 45 ya kodi ya huduma, kwa nini tukatae figure za tume ya Rais ambazo zinatoa mwelekeo wa mapato kama yanavyobainishwa.

Madai yanayotolewa na ACACIA yanafanya waonekane wana makosa (incriminate) kwa kusema viwango kidogo halafu hapo hapo wanadai mapato yao yamepungua kwa zaidi ya asilimia 45 kwa sababu ya kuzuiwa kuuza makanikia.
Nadhani una upungufu mkubwa katika kuelewa mahesabu ya kitaalam.

Uweli ni kuwa kama una uelewa wa kitaalam wa mining industry, Acacia wapo sahihi. Viwango vya dhahabu hupimwa kwa ppm (parts per million) yaani grams per ton. Kwa kawaida huelezei kwa percentage. Ukipeleka kwenye percentage utaona kama ni kiwango kidogo sana. Viwango vya almasi huelezwa kwa carat, kwa sababu hutegemea kupata viwango vya kusomeka katika asilimia.

Bulyanhulu gold mine, average grade ni 13 ppm (13 grams per ton of ore material) ambayo ni sawa na 0.0013% Au. Acacia wameripoti kuwa ndani ya makinikia average grade ni 0.03% Au, hii ni sawa na 300ppm Au au 300g/t Au. Hiki ni kiwango cha juu sana, na huwezi kukipata katika hali ya uhalisia wa kawaida. Imefikia kiasi hicho baada ya kufanya concentration.

Tatizo kubwa ni kwamba watanzania wengi hawaelewi kabisa sekta hii lakini wanataka waonekane wanaelewa kwa hisia. Hesabu za Mruma zinaonesha kuwa kuna 3000g/t Au kwenye makinikia. Kwa anayejua, taarifa hiyo ni ya kipuuzi kabisa, nadhani ipo kwaajili ya wajinga maana haijawahi kupatikana concentration ya namna hiyo katika Dunia hii, labda mwezini ambako hakuna binadamu ambaye amewahi kufika.

Mruma's is special for the fools.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom