Kodi ya ACACIA yapungua asilimia 45

Kodi ya ACACIA yapungua asilimia 45

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,247
Reaction score
25,191
Kodi ya huduma inayotolewa na Mgodi wa Dhahabu wa ACACIA Bulyanhulu kwa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita imepungua kwa zaidi ya asilimia 45 kutokana na Serikali kuzuia usafirishaji wa mchanga (makinikia) kwenda nje ya nchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Carlos, Gwamagobe amesema kupungua kwa mapato yatolewayo na ACACIA itaathiri bajeti kwasababu wanategemea mwaka wa fedha 2017/18 kukusanya zaidi ya Sh800 milioni kama kodi ya huduma kutoka katika mgodi huo.

“Kushuka kwa mapato haya yataathiri bajeti yetu kwakuwa kuna miradi haitatekelezwa mwaka jana tulizielekeza kwenye sekta ya elimu sasa inabidi juhudi za makusudi zifanyike fedha hizi zilikua zikitusaidia sana kwenye miradi ya maendeleo na miradi ya kijamii,”amesema Gwamagobe.

Amesema halmashauri hiyo imefanikiwa kujenga madarasa 12 ya shule ya msingi, manane ya shule za sekondari na kujenga hosteli ya Shule ya Sekondari Kakola pamoja na kujenga ghala la kuhifadhia chakula.

Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale, Hamimu Buyama amesema kodi ya huduma inayotolewa na ACACIA imesadia kusukuma maendeleo ya halmashauri hiyo na kusema katika maendeleo lazima ziwepo changamoto kama zilivyowakuta ACACIA sasa.

Amesema suala la makinikia limekua kikwazo kwa kampuni lakini pia kwa halmashauri zinazotegemea kodi ya huduma kutokana na mapato kushuka na kusema anaimani suala hilo litafika mwisho mwema na wao kuendelea kufanya kazi kama ilivyokuwa awali.

Akikabidhi hundi kwa uongozi wa Wilaya ya Nyang’wale Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa ACACIA Bulyanhulu, Grahama Crew amesema kwa kipindi cha miezi sita iliyopita kodi ya ushuru wa huduma ni zaidi ya Sh687 milion ambazo zimegawanya katika Halmashauri ya Msalala iliyopata asilimia 67 na Nyang’wale iliyopata asilimia 33.

Amesema kuanzia mwaka 2000 hadi sasa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu umelipa zaidi ya Sh10.2 bilioni kama kodi ya huduma katika maeneo wanayofanya kazi ambapo amesema ni matarajio yao kuendelea kuimarisha sekta ya viwanda kwenye uchimbaji wa madini katika Wilaya ya Nyang’wale.

Akizungumza katika makabidhiano hayo mbunge wa Nyang’wale, Hussein Nassoro amesema wananchi wa Nyang’wale wanauhusiano mzuri na kampuni, lakini bado wanamahitaji makubwa.

Amesema wilaya hiyo bado iko nyuma katika sekta ya elimu, afya na miundombinu ya barabara na kuiomba kampuni hiyo kuendelea kuisaidia huduma za kijamii kwa wananchi ili waweze kuona faida ya uwekezaji katika maeneo yao.

Chanzo: Mwananchi
 
Miaka 17 bil 10, what a waste...
Unaelewa maana ya kodi ya huduma?

Hiyo ni 0.3% ya production. Ulitaka watoe kiasi gani baada ya kulipa 30% corporate tax na 4% on production royalty?

Watanzania wengi ni hopeless kabisa. Wanaenda shule kujifunza kutengeneza sentensi za kiingereza lakini siyo kukuza analytical thinking.
 
Miaka 17 bil 10, what a waste...
Kabla ya kulaumu ni vizuri ungejiuliza hiyo pesa ndio total amount of money to the government au hiyo ni sehemu tu ya pesa itolewayo kwa halmashauri? Na je formula pia ikoje? NI wao wanaamua cha kutoa au ipo kanuni maalumu ya kutolea and again kama ipo kanuni maalumu, je hi kanuni imeanza lini na kwanini? Vinginevyo kama umeuelewa vizuri uzi is like huo uongozi wa halmashauri (mkuu wa wilaya na huyo mwingine) ni kama wana laumu indirect hatua ya serikali kwa hatua zilizo chukuliwa dhidi ya huo mchanga. Soma tena utaona hapo.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Carlos, Gwamagobe amesema kupungua kwa mapato yatolewayo na ACACIA itaathiri bajeti kwasababu wanategemea mwaka wa fedha 2017/18 kukusanya zaidi ya Sh800 milioni kama kodi ya huduma kutoka katika mgodi huo.

“Kushuka kwa mapato haya yataathiri bajeti yetu kwakuwa kuna miradi haitatekelezwa mwaka jana tulizielekeza kwenye sekta ya elimu sasa inabidi juhudi za makusudi zifanyike fedha hizi zilikua zikitusaidia sana kwenye miradi ya maendeleo na miradi ya kijamii,”amesema Gwamagobe.

Huyu anatafuta kutumbuliwa. Watu wanadai trilioni 425, yeye anazungumzia kodi ya sh. milioni mia nane?!
 
Kodi ya huduma inayotolewa na Mgodi wa Dhahabu wa ACACIA Bulyanhulu kwa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita imepungua kwa zaidi ya asilimia 45 kutokana na Serikali kuzuia usafirishaji wa mchanga (makinikia) kwenda nje ya nchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Carlos, Gwamagobe amesema kupungua kwa mapato yatolewayo na ACACIA itaathiri bajeti kwasababu wanategemea mwaka wa fedha 2017/18 kukusanya zaidi ya Sh800 milioni kama kodi ya huduma kutoka katika mgodi huo.

“Kushuka kwa mapato haya yataathiri bajeti yetu kwakuwa kuna miradi haitatekelezwa mwaka jana tulizielekeza kwenye sekta ya elimu sasa inabidi juhudi za makusudi zifanyike fedha hizi zilikua zikitusaidia sana kwenye miradi ya maendeleo na miradi ya kijamii,”amesema Gwamagobe.

Amesema halmashauri hiyo imefanikiwa kujenga madarasa 12 ya shule ya msingi, manane ya shule za sekondari na kujenga hosteli ya Shule ya Sekondari Kakola pamoja na kujenga ghala la kuhifadhia chakula.

Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale, Hamimu Buyama amesema kodi ya huduma inayotolewa na ACACIA imesadia kusukuma maendeleo ya halmashauri hiyo na kusema katika maendeleo lazima ziwepo changamoto kama zilivyowakuta ACACIA sasa.

Amesema suala la makinikia limekua kikwazo kwa kampuni lakini pia kwa halmashauri zinazotegemea kodi ya huduma kutokana na mapato kushuka na kusema anaimani suala hilo litafika mwisho mwema na wao kuendelea kufanya kazi kama ilivyokuwa awali.

Akikabidhi hundi kwa uongozi wa Wilaya ya Nyang’wale Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa ACACIA Bulyanhulu, Grahama Crew amesema kwa kipindi cha miezi sita iliyopita kodi ya ushuru wa huduma ni zaidi ya Sh687 milion ambazo zimegawanya katika Halmashauri ya Msalala iliyopata asilimia 67 na Nyang’wale iliyopata asilimia 33.

Amesema kuanzia mwaka 2000 hadi sasa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu umelipa zaidi ya Sh10.2 bilioni kama kodi ya huduma katika maeneo wanayofanya kazi ambapo amesema ni matarajio yao kuendelea kuimarisha sekta ya viwanda kwenye uchimbaji wa madini katika Wilaya ya Nyang’wale.

Akizungumza katika makabidhiano hayo mbunge wa Nyang’wale, Hussein Nassoro amesema wananchi wa Nyang’wale wanauhusiano mzuri na kampuni, lakini bado wanamahitaji makubwa.

Amesema wilaya hiyo bado iko nyuma katika sekta ya elimu, afya na miundombinu ya barabara na kuiomba kampuni hiyo kuendelea kuisaidia huduma za kijamii kwa wananchi ili waweze kuona faida ya uwekezaji katika maeneo yao.

Chanzo: Mwananchi
Waache kuingilia Mjadala unaoendelea kwa hiyo Kama siyo hiyo Migoni hizo Halmashauri haziwezi kubuni vyanzo vingine vya Kupata hizo hela... WEaache kupotosha Umma kwa kutumiwa na Uongozi wa hiyo Migodi
 
Unajua watu wanaangalia tu asilimia inayotolewa kwenye mrabaha na kusahau kwamba migodi pia inalipa kodi na tozo mbali mbali zaidi ya mrabaha. lakini pia migodi inatumia malighafi mbali mbali ili kuendesha migodi hiyo.

Watu sasa mawazo yamezama kwenye mitambo ya kuchenjulia bila ya kuangalia maslahi ambayo na wafanyakazi wanatakiwa kupewa.
 
Kwa hiyo makanikia yana mapato zaidi ya asilimia 45?

Kama tukikubali kuwa makanikia yana mapato zaidi ya asilimia 45 ya kodi ya huduma, kwa nini tukatae figure za tume ya Rais ambazo zinatoa mwelekeo wa mapato kama yanavyobainishwa.

Madai yanayotolewa na ACACIA yanafanya waonekane wana makosa (incriminate) kwa kusema viwango kidogo halafu hapo hapo wanadai mapato yao yamepungua kwa zaidi ya asilimia 45 kwa sababu ya kuzuiwa kuuza makanikia.
 
Waambie watulie watu tuzoe pesa !hiyo halamashauri haitaki noah?
Sisi tunafukuzia mifwezwa nyie mnalialia na vipunje vya hela !wapige kimya wakati palamagamba anafanya abracadabra zake huko!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua watu wanaangalia tu asilimia inayotolewa kwenye mrabaha na kusahau kwamba migodi pia inalipa kodi na tozo mbali mbali zaidi ya mrabaha. lakini pia migodi inatumia malighafi mbali mbali ili kuendesha migodi hiyo.

Watu sasa mawazo yamezama kwenye mitambo ya kuchenjulia bila ya kuangalia maslahi ambayo na wafanyakazi wanatakiwa kupewa.
Mkuu naomba Ututajie Mali Ghafi ambazo zinanunuliwa kweny Mikoa ambayo Migodi ipo ..Local Raw Material.. Naomba unitajie Mkuu
 
Siku hizi kuna majina ya ajabu ya wilaya!

May Allah bless Me and You
 
Mkuu naomba Ututajie Mali Ghafi ambazo zinanunuliwa kweny Mikoa ambayo Migodi ipo ..Local Raw Material.. Naomba unitajie Mkuu
Unapotaka kusema malighafi kwenye uzalishaji wa kisasa unazungumzia vitu vingi. Kwa mfano kwa Acacia dhahabu ni zao (Product) lakini wa watengeneza vito dhahabu ni malghafi (Raw Material). Sijasema kwamba Malighafi za uzalishaji zinanunuliwa mikoa ilipo migodi lakini naamini bila shaka kuna makampuni ya Kitanzania yana zabuni za kupeleka malighafi mbalimbali ili dhahabu iwe dhahabu inayofaa kuuzwa.
 
Kwa hiyo makanikia yana mapato zaidi ya asilimia 45?

Kama tukikubali kuwa makanikia yana mapato zaidi ya asilimia 45 ya kodi ya huduma, kwa nini tukatae figure za tume ya Rais ambazo zinatoa mwelekeo wa mapato kama yanavyobainishwa.

Madai yanayotolewa na ACACIA yanafanya waonekane wana makosa (incriminate) kwa kusema viwango kidogo halafu hapo hapo wanadai mapato yao yamepungua kwa zaidi ya asilimia 45 kwa sababu ya kuzuiwa kuuza makanikia.
Una akili za kuambiwa na wewe umejiongezea za kwako. Mimi sijawahi kuhofia rioting ya Tume. Hao ACACIA ingekuwa Ike taarifa Prof. Mruma ni ya uongo wangelazimisha Tume huru kupima tena hayo makinikia lakini hawana haja ya kupima tena maana wanaogopa itawaumbua zaidi.
 
Kupungua mapato kwa asilimia zote hizo kisa makinikia!

Makinikia si ni nyongeza tu!!!?
Mfano ukinunua kopo la mkaa anakupa na chenga kidogo!

Kwel tumepigwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kodi ya huduma inayotolewa na Mgodi wa Dhahabu wa ACACIA Bulyanhulu kwa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita imepungua kwa zaidi ya asilimia 45 kutokana na Serikali kuzuia usafirishaji wa mchanga (makinikia) kwenda nje ya nchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Carlos, Gwamagobe amesema kupungua kwa mapato yatolewayo na ACACIA itaathiri bajeti kwasababu wanategemea mwaka wa fedha 2017/18 kukusanya zaidi ya Sh800 milioni kama kodi ya huduma kutoka katika mgodi huo.

“Kushuka kwa mapato haya yataathiri bajeti yetu kwakuwa kuna miradi haitatekelezwa mwaka jana tulizielekeza kwenye sekta ya elimu sasa inabidi juhudi za makusudi zifanyike fedha hizi zilikua zikitusaidia sana kwenye miradi ya maendeleo na miradi ya kijamii,”amesema Gwamagobe.

Amesema halmashauri hiyo imefanikiwa kujenga madarasa 12 ya shule ya msingi, manane ya shule za sekondari na kujenga hosteli ya Shule ya Sekondari Kakola pamoja na kujenga ghala la kuhifadhia chakula.

Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale, Hamimu Buyama amesema kodi ya huduma inayotolewa na ACACIA imesadia kusukuma maendeleo ya halmashauri hiyo na kusema katika maendeleo lazima ziwepo changamoto kama zilivyowakuta ACACIA sasa.

Amesema suala la makinikia limekua kikwazo kwa kampuni lakini pia kwa halmashauri zinazotegemea kodi ya huduma kutokana na mapato kushuka na kusema anaimani suala hilo litafika mwisho mwema na wao kuendelea kufanya kazi kama ilivyokuwa awali.

Akikabidhi hundi kwa uongozi wa Wilaya ya Nyang’wale Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa ACACIA Bulyanhulu, Grahama Crew amesema kwa kipindi cha miezi sita iliyopita kodi ya ushuru wa huduma ni zaidi ya Sh687 milion ambazo zimegawanya katika Halmashauri ya Msalala iliyopata asilimia 67 na Nyang’wale iliyopata asilimia 33.

Amesema kuanzia mwaka 2000 hadi sasa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu umelipa zaidi ya Sh10.2 bilioni kama kodi ya huduma katika maeneo wanayofanya kazi ambapo amesema ni matarajio yao kuendelea kuimarisha sekta ya viwanda kwenye uchimbaji wa madini katika Wilaya ya Nyang’wale.

Akizungumza katika makabidhiano hayo mbunge wa Nyang’wale, Hussein Nassoro amesema wananchi wa Nyang’wale wanauhusiano mzuri na kampuni, lakini bado wanamahitaji makubwa.

Amesema wilaya hiyo bado iko nyuma katika sekta ya elimu, afya na miundombinu ya barabara na kuiomba kampuni hiyo kuendelea kuisaidia huduma za kijamii kwa wananchi ili waweze kuona faida ya uwekezaji katika maeneo yao.

Chanzo: Mwananchi

Gazeti la Rostam naona mnakazana sana na hii issue ya Acacia.
 
Back
Top Bottom