Kodi iliyolipwa MwanaHalisi nani kawajibishwa? Je, Mawio wakishinda?

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,680
8,868
Naomba kuuliza tumeona Mwana Halisi lilifungiwa na Serikali na mwisho wa Siku akashinda kesi na serikali kuamliwa na Mahakama kulipia gharama za kesi pamoja na hasara iliyopatikana kutokana na usimamishaji wa uzalishaji!

Kimsingi hii pesa ni ya walipa kodi! Sasa pesa ya umma inapotumika bila usimamizi je ni nani anatakiwa kuwajibishwa?

Je, wahusika walioitia hasara serikali wamewajibishwa?

Leo Wizara ile ile inarudia kulifungia Gazeti la Mawio. Je, Gazeti la Mawio leo likishinda nani atalipia gharama za kusimamisha uzalishaji? Je, watawajibishwa maana pesa ni za walipa kodi, mlipa kodi ni wewe ni Mimi.

Je, sisi tunawawajibisha vipi?

Nawasilisha.
 
Mi sio mwanasheria na sijasomea sheria kabisaaaa,ila mazingira yalotumika kulifungia Mwanahalisi ndio hayohayo yamelikumba MAWIO.

Kwa maana hiyo kuna.kila dalili Mawio wakashinda kesi,na pia sijui (hili nahisi)jamaa waliyaandika waloyaandika wakiamini ipo siku wahusika wataingia mtegoni kuwafungia,maana leo nimeona picha kwenye Mwananchi wakienda Kituo cha polisi KATI.

Najiuliza kama mtoa mada je wakishinda itakuwajeeee,Mwanahalisi alipigwa ban kwa miaka mitatu mwisho ikaonekana alionewa,kwa sababu Waziri au serikal itapaswa kuithibitishia mahakama kwa kuwapa USHAHIDI ili kuitia hatian Mawio pasipo kutia shaka,je serikali inao huo ushahidi?.
 
Naomba kuuliza tumeona Mwana Halisi lilifungiwa na Serikali na mwisho wa Siku akashinda kesi na serikali kuamliwa na Mahakama kulipia gharama za kesi pamoja na hasara iliyopatikana kutokana na usimamishaji wa uzalishaji! Kimsingi hii pesa ni ya walipa kodi! sasa pesa ya umma inapotumika bila usimamizi je ni nani anatakiwa kuwajibishwa??Je wahusika waliyo itia hasara serikali je wamewajibishwa???Leo Wizara ile ile inarudia kulifungia Gazeti la Mawio. Je Gazeti la Mawio leo likishinda nani atalipia gharama za kusimamisha uzalishaji je watawajibishwa??maana pesa Hi ni za walipa kodi mlipa kodi ni wewe ni Mimi je sisi tunawawajibisha vipi?.Nawasilisha.
HAKUNA FEDHA YOYOTE MWANAHALISI IMELIPWA KWA KUSHINDA KESI,WANGEPEWA KAMA TU MWANAHALISI WANGEFUNGUA KESI YA KUDAI FIDIA JAMBO AMBALO HAWAKULIFANYA.ELEWENI BAVICHA
 
HAKUNA FEDHA YOYOTE MWANAHALISI IMELIPWA KWA KUSHINDA KESI,WANGEPEWA KAMA TU MWANAHALISI WANGEFUNGUA KESI YA KUDAI FIDIA JAMBO AMBALO HAWAKULIFANYA.ELEWENI BAVICHA
Kwani kesi iliyofunguliwa ilikuwa ni ya nini??au na wewe mwana Lumumba ni mganga njaa ujui hata kesi ilihusu nini??Sasa washinde kesi na walizuiliwa uzalishaji wasidai hivi unamuona wakili wa Mwana Halisi kama wa Uhuru Publication?kwe wewe Lumumba Buku 7
 
Back
Top Bottom