Kocha yupi ni bora kwa sasa Duniani?

Najua umekubaliana na Mimi mkuu kuwa varverde hana kikosi kizuri kama cha Madrid na anafanya mambo makubwa imagine angekuwa na ukuta kama wa atletico Madrid angefungwa hata goal 1?
Kinachoibeba barce messi tu,ndiye anaevuruga plan za timu pinzani..ukimtoa messi barce wanamchapa usiku na mchana..
 
Ningejua sifa za kuwa KOCHA BORA, ningeweza kutaja angalau majina matatu, ila mpaka sasa, Man City na Real Madrid wameonesha kabumbu la burudani na ushindani mkubwa ndani ya UEFA.
man city na what !!? u cnt be serious aiseeee haaaaha
 
Kocha bora kwa sasa ni kocha anaeifundisha team ambayo haijapoteza mechi hata moja kwenye league mpaka sasa. Namzungumzia Ernesto Valverde wa Barcelona!

Ameifikisha team fainali copa del rey, anaongoza league kwa gap kubwa, na ameivusha team kuingia robo fainali ya UEFA!

Tactically, ameibadili Barcelona kua team yenye defense imara kuliko wakati mwingine niliopata kushuhudia.

Team imefungwa magoli machache sana kuliko misimu mingine!

Mpinzani wake ni Pep Guardiola. Hakuna asieona transformation aliyoifanya pale etihad!

Pia anaongoza league, yupo robo fainali UEFA, pia nusu fainali emirates cup!

Huwezi kumuweka Zidane kwenye hii list wakati team yake haiko hata nafasi ya pili kwenye league. Pia ametolewa Copa del rey.

Pia Mourinho team yake haina achievement yoyote ya maana msimu huu, huwezi kumuita kocha bora kwa sasa!

Ubora unapimwa kwa mafanikio. Namkubali sana Diego Simeone, ila team yake haina mafanikio ya kutosha kuthibitisha ubora wake!

Hatuwezi kukuita kocha bora wakati team haishindi vikombe.

Budget kubwa ya usajili sio tatizo. Mourinho katumia budget kubwa sana, ila sasa hivi anapambana kubaki top four badala ya kupambania ubingwa!

Christian Ronaldo amekua mchezaji bora wa mwaka kwa kushinda UCL na EURO, pamoja na idadi kubwa ya magoli.

Kwahiyo hata kocha bora itabidi tuangalie makombe anayoshinda na mafanikio ya team kwa ujumla!

Adiós amigos!
 
Back
Top Bottom