Muda wa Kocha Dylan Kerr kuinoa Simba umefikia mwisho baada ya uongozi kwa pamoja kukubaliana kuachana naye rasmi.
Ni yale yale miaka inakwenda na kurudi, sioni jipya kabisa, hizi club bila kutolewa kwa wanachama na kuuzwa ili ziendeshwe kibiashara zaid hakuna jipya,
Muda wa Kocha Dylan Kerr kuinoa Simba umefikia mwisho baada ya uongozi kwa pamoja kukubaliana kuachana naye rasmi.
Uongozi wa Simba umefikia uamuzi wa kuachana na Kerr baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa kikosi hicho katika Ligi Kuu Bara na baadaye Kombe la Mapinduzi lililomalizika hivi karibuni mjini Zanzibar.
Pamoja na kutokuwa na matokeo mazuri lakini inaonekana uongozi haujaridhishwa na uchezaji wa kikosi cha timu hiyo na mambo yalikuwa mabaya zaidi katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar.
“Kweli kamati ya utendaji imefanya kikao cha muda cha dharura na kukubaliana na hilo,” kilieleza chanzo kutoka Zanzibar.
“Taarifa tulizonazo ni kwamba kocha Kerr ameitwa Dar es Salaam ambako ataondoka kesho Jumanne akiwa Dar es Salaam ataelezwa kuhusiana na uamuzi huo wa uongozi kumtupia virago na nafasi yake atapewa Kocha Majanja ambaye juzi aliingia mkataba kama kocha msaidizi.”
Chanzo kilipoulizwa kama uongozi hauwezi kubadili uamuzi hiyo kesho, kilieleza:
"Tunaamini hakuna nafasi hiyo, hata Kerr mwenyewe ameishashitukia, atakuwa anajua kwamba mambo yatakuwa hivyo. Usiku huu ameamua kutoka kwenda kuiaga Zanzibar (kicheko)."
Taarifa nyingine zimeeleza kwamba Kerr raia wa Uingereza ameponzwa na ubishi na uongozi umekuwa ukimlaumu kutofanya kazi kwa kujituma.
Wakati fulani, Rais wa Simba, Evans Aveva aliwahi kujitokeza mazoezini kimyakimya wakati Simba ikijifua kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), hali iliyoonyesha wazi uongozi hauridhiki na utendaji wa Mwingereza huyo aliyechukua nafasi ya Goran Kopunovic aliyeondoka baada ya kutaka dau la Sh milioni 100 ili aongeze mkataba mpya Simba.
Kerr anaondoka na kuiacha Simba katika nafasi ya tatu baada ya mechi 13 na imekusanya pointi 27 nyuma ya Yanga yenye 33 na Azam FC kileleni ikiwa na 35.
Mwingereza huyo anaiacha Simba ikiwa imeshinda mechi 8, sare 3 na kupoteza mbili, imefunga mabao 20 ikishika nafasi ya tatu kwa ufungaji baada ya Yanga yenye 30 na Azam FC yenye 27 huku ikiwa imeruhusu mabao 9, ikiwa safu bora ya ulinzi katika nafasi ya nne baada ya Azam iliyoruhusu mabao 8, Mtibwa Sugar mabao 7 na Yanga yenye safu ngumu zaidi imefungwa mabao matano tu.
hasira sana mkuuHao Simba Wasitufanye Sisi Wajinga Na ACHA LEO NITEME NYONGO YANGU KWANI NIMECHOKA NA UPUUZI WA AINA HII. Kocha Kerr Haachwi Labda Kwakuwa Hana UWEZO Bali Anaachwa Kwa VITENDO VYA KIPUUZI VYA Makamu Wa Rais Wa Simba Gofrey Nyange Kaburu Ambaye Mara Kwa Mara Amekuwa AKIKWARUZANA Nae Kwa Kuwa Alikuwa Anapenda KUMPANGIA Kikosi Na Kaburu Alipoona Kerr Ana MSIMAMO Akaendelea Kufanya UMAFIA Wake Uliozoeleka Simba Wa Kuwahonga WACHEZAJI Wale MAHIRI Na TEGEMEZI Wa Simba Ili Kuhujumu Na Hapo Baadae Mkitaka Niwatajieni Hao WACHEZAJI Nipo Tayari. Sababu Ya Pili Ya Kuondolewa Kwa Kerr Ni Baadhi Ya WAJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI Ya Simba Sports Club Wakiongozwa Na Said Tully Na Aliyewahi Kuwa Mmoja Wa Wajumbe Huko Nyuma Mtangazi Wa Michezo Wa E FM Ibrahim Masoud " Maestro " Ambao Wote Kwa Pamoja HAWAKUPENDEZWA NA KITENDO CHA Kocha Kerr KUSABABISHA " Mshikaji " Na " Mshirika " Wao Seleman Matola Aliyekuwa Kocha Msaidizi Kuondoka Simba Hivyo Walichokifanya Hawa Watu Ni Kufanya Kila Namna Kuihujumu Timu Kwa Namna Yoyote Ile Ili Afukuzwe Kitu Ambacho WAMEFANIKIWA Kwani Muda Si Mrefu Dylan Kerr ANAFUKUZWA Simba Pamoja Na Kipa Wa Makipa Mkenya Abdul Salim. Rais Wa Simba ANAMPENDA Na ANAMKUBALI Mno Na Sana Kocha Kerr Ila Anazidiwa Nguvu Ya Kimaamuzi Na Matajiri Waliopo Simba Sports Club Na Kujikuta Ni " JOKA LA KIBISA ".
SIRI GANI IPO NYUMA YA HAYA YOTE NA KWANINI KILA MARA SIMBA INAFUKUZA TU MAKOCHA WAKE?
Nimesema Kuwa Leo NATEMA NYONGO Na Naitema KWELI Bila UWOGA Na AIBU. Kwa Wanasimba Wenzangu Tambueni Kuwa 95% Ya VIONGOZI WA UTENDAJI WA SIMBA Wanakula Kupitia Migongo Ya WACHEZAJI. Kila MJUMBE WA SIMBA ANA MCHEZAJI WAKE Na Anafanya Kila Liwezekanalo Tu Ili Apangwe ( Acheze ) Ili Ktk Kila Posho au Mshahara Wa Huyo Mchezaji Basi Kuna 10% Ya Huyo Mjumbe Na Endapo Itatokea Mchezaji Baadae Akaja Kumgeuka Huyo Mjumbe Basi ATATENGENEZEWA ZENGWE Na Kujikuta HAPANGWI Na Hata KUFUKUZWA Klabuni. Kuna Wachezaji Wa Kigeni Ambao KABURU KAWALETA Lakini Kerr HAWAKUBALI Na Huwa Mgumu Kuwapanga Na Kuna Wachezaji Wengine Wa Kigeni KABURU Aliwaleta Lakini Kerr AKAWAKATAA Na Wakaondoka Zao. Hao WACHEZAJI WA KIGENI ANAPOWALETA Kaburu Huwa ANAPANDISHA DAU LAO Kisha ANAJILIPA Zaidi. Nina Mengi Zaidi Ya Haya Ila Kinachoisumbua Simba Sports Club Siyo MAKOCHA Hawa Wanaokuja Bali Ni:
Kwa Asubuhi Hii Naomba Niishie Hapa ILA Nitakuja Na Mengine Zaidi Baadae Kwani Yapo Mengi Yanayotia UCHUNGU Na HASIRA Ila Wana Simba Sports Club WENZANGU Tutaendelea Tu KULIA Na KUTESEKA Kwani Kuna Viongozi WAWILI Mmoja Ni Mkuu Ambaye Ni Godfrey Nyange Kaburu Na Mjumbe Wa Kamati Ya Utendaji Said Tully Hawa LEO NAPENDA KUTOA SIRI ZAO KUWA NI MASHABIKI WA KUTUKUKA WA KLABU YA YANGA FOOTBALL CLUB Na Mtakaonibishia Ktk HILI KUNA SIKU MTAKUJA KUNIKUMBUKA. Binafsi Tully Nimekua Nae Tokea Akiwa Anishi Hapo Kwao FIRE Kariakoo Ktk Hizo Kota Za NHC Na Nyumba Yao Ikiwa Jirani Na Aliyokuwa Anakaa Kocha MKWASA Na Pia Nimesoma Nae Miaka Miwili SHIGHATINI SECONDARY SCHOOL Kule Usangi Ni MSHABIKI Na MPENZI Tena Wa KUFA Wa YANGA FOOTBALL CLUB Na Nilishangaa Mno Na Kujiuliza Amejiingizaje Ndani Ya Simba Sports Club.
- Maelewano Mabaya Ya Rais Na Makamu Wake Japo Wanaonyesha Ushirikiano Wa KINDUMILAKUWILI.
- Uongozi Wa KIFISADI Na Kaeni Mkijua Kuwa Wachezaji Wanadai MISHAHARA Ya Miezi Miwili Sasa Ila Wanaogopa KUFUNGUKA.
- 10%.
- UNAFIKI ULIOTUKUKA.
- Kamati Ya USAJILI Ambayo Haina UELEDI Na Iliyojaa LONGOLONGO Tupu.
- UMOJA Hafifu Baina Ya MATAWI Huku Tawi Moja Tu Ndiyo Likipewa KIPAUMBELE Lile La Mzee DALALI La Pale Mikumi.
- Kuamini Mno USHIRIKINA Kuliko UFUNDI Ambapo MGANGA Hupewa Kipaumbele Kuliko MCHEZAJI Wa Timu.