Kocha Mexime: Nimepandisha ‘CV’ kuifunga Yanga ya Maximo

Kocha Mexime: Nimepandisha ‘CV’ kuifunga Yanga ya Maximo

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713

maxime-maximo.jpg

​


KOCHA Mkuu wa timu ya Mtibwa Sugar ya Manungu, Morogoro, Mecky Mexime amewashukuru wachezaji wake kwa kuifunga Yanga na hivyo kumfanya apandishe wasifu (CV) wake mbele ya mwalimu wake mkuu katika soka.

Yanga kwa sasa inanolewa na Marcio Maximo, raia wa Brazil ambaye kwa miaka minne aliwahi kuifundisha timu ya Taifa, Taifa Stars wakati Mexime akiwa beki na nahodha wake.
Mexime alisema hayo baada ya kumalizika kwa mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga uliofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Jamhuri hapa ambao Mtibwa Sugar iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Hivyo alisema amefurahi kupata ushindi huo na zaidi ni kupata ushindi dhidi ya kocha wake mkuu wa zamani wa Taifa Stars, Maximo ambaye pia alimshauri asomee kazi ya ukocha.
"Napenda kuwashukuru wachezaji wangu kwa ushindi huu, sasa wameipandisha juu CV (wasifu) yangu kwani timu tulioifunga inafundishwa na kocha Maximo ambaye mimi nilikuwa ni mwanafunzi wake Taifa Stars," alisema Mexime.

"Ushindi huu si wangu pekee, ni wa wachezaji na timu kwa ujumla kwa maana mimi ni kocha sichezi uwanjani, mchango wangu ni kuwafundisha na kutoa maelekezo ambayo yakitekelezwa kwa vitendo yanazaa matunda."

Kwa mujibu wa kocha huyo, kabla ya kustaafu soka akiwa katika timu ya Taifa, Maximo ndiye aliyemshauri akiacha soka, ajifunze kazi ya ukocha na baada ya kustaafu, alitekeleza na sasa anainoa timu yake ya Mtibwa Sugar.

"Siku zote mashabiki wa soka wanapoona timu isiyokuwa na jina kubwa inapocheza na yenye jina kubwa haipewi nafasi ya kushinda kama ilivyo kwa mchezo huu wakiipa Yanga nafasi kubwa ya kushinda," alisema Mexime.

Kocha huyo hakupenda kubashiri makubwa zaidi katika michezo inayofuata, akisema Ligi Kuu ndio imeanza na safari ni ndefu na ushindi huo pia umeleta hamasa kwa wachezaji, viongozi na wapenzi wa timu hiyo kuiona ikiendelea kufanya vizuri michezo ijayo.

CHANZO: Habari Leo
 
Magazeti yetu yamempuuza, bado Jaja ni gumzo la jiji.
Kanuni ya Dhahabu: wafanyie wengine upendalo kufanyiwa wewe.
Kama kumsifu Jaja kwa kufunga magoli matano ndani ya mechi sita ni kosa, ni kosa pia kumsifu Maxime kwa kushinda mechi moja ya Ligi.
 
Kanuni ya Dhahabu: wafanyie wengine upendalo kufanyiwa wewe.
Kama kumsifu Jaja kwa kufunga magoli matano ndani ya mechi sita ni kosa, ni kosa pia kumsifu Maxime kwa kushinda mechi moja ya Ligi.

Mkuu baada ya "homa ya jiji" Jaja kuonesha kandanda safi, naskia amewachanganya kabisa Yanga mpaka wameighairi kumshitaki Okwi FIFA.
 
Kanuni ya Dhahabu: wafanyie wengine upendalo kufanyiwa wewe.
Kama kumsifu Jaja kwa kufunga magoli matano ndani ya mechi sita ni kosa, ni kosa pia kumsifu Maxime kwa kushinda mechi moja ya Ligi.

Jaja na wengine walisifiwa hata kabla ya kucheza mechi hata moja ya mashindano. News Room huwa wanapika habari kulingana na mihemko ya washabiki mkuu, wanajua ukiandika cha Mexime hakiuzi kwa hiyo watatafuta hata ushuzi wa Jaja au Okwi wauandike.
 
Huyu jamaa huwa n kizibo anaifunga yanga afu anakuja fungwa goal nying tu na Ndanda
 
Jaja na wengine walisifiwa hata kabla ya kucheza mechi hata moja ya mashindano. News Room huwa wanapika habari kulingana na mihemko ya washabiki mkuu, wanajua ukiandika cha Mexime hakiuzi kwa hiyo watatafuta hata ushuzi wa Jaja au Okwi wauandike.
Kanuni ya Dhahabu: kasoro mbili hazitengenezi sahihi moja.
Kama kumsifia Jaja kabla hajacheza lilikuwa kosa, kumsifia Mexime kwa mechi moja ni kosa pia.
 
Kanuni ya Dhahabu: kasoro mbili hazitengenezi sahihi moja.
Kama kumsifia Jaja kabla hajacheza lilikuwa kosa, kumsifia Mexime kwa mechi moja ni kosa pia.

Kusifia mtu kwa mechi moja sio kosa, kwani anastahili. Kosa ni kusifia pasi na ukweli, kwa mihemko na sio uhalisia... Wafanyiwavyo Jaja na wenzake.
 
Kusifia mtu kwa mechi moja sio kosa, kwani anastahili. Kosa ni kusifia pasi na ukweli, kwa mihemko na sio uhalisia... Wafanyiwavyo Jaja na wenzake.
Ni swala la mtizamo (perception). Kama unavyohisi Maxime amefanya vizuri (na ungemsifia laiti ungekuwa mwanahabari), na wanaomsifia huyo mwengine wanahisi amefanya vizuri. Tusilazimishe maoni yetu yawe ndiyo ya wengine wote, ingawa nakubaliana mno na wanaolaani unazi wa kiandishi. Nimekuwa nikiusema sana humu mtandaoni. Inashangaza kwamba kasoro hiyo imeanza kuwaudhi baadhi yetu kwa sababu tu amesifiwa Jaja!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom