Rugby Union
JF-Expert Member
- Nov 21, 2012
- 402
- 257
MABINGWA wa soka wa Zanzibar, KMKM leo wanatupa karata muhimu katika Kombe la Kagame.
Timu hiyo inahitaji ushindi ili kujiweka kufuzu kwa robo fainali, vinginevyo kipigo au sare kitakuwa kimewapa tiketi ya kurudi Unguja kabla ya michuano kumalizika.
Kikosi hicho cha Ali Bushiri kina pointi mbili kutokana na michezo mitatu ya Kundi A, baada ya kuanza kwa sare ya bao 1-1 na Atlabara ya Sudan Kusini na kisha kuchapwa mabao 4-0 na Azam FC na juzi kulazimisha sare ya bao 1-1 na Adama City ya Ethiopia.
Kwa matokeo hayo, inahitaji ushindi leo ili kusonga mbele au kutokubali kufungwa ili angalau iwe katika nafasi nzuri ya kupata nafasi ya tatu bora.
Katika Kundi A, timu tatu zi tasonga mbele kucheza robo fainali sawa na Kundi B wakati Kundi C litatoa timu mbili katika hatua hiyo itakayoanza Jumanne ijayo. Kutakuwa na nafasi moja ya timu ya tatu yenye matokeo mazuri miongoni mwa makundi hayo.
Kwa msingi huo, KMKM inayohitimisha hatua ya makundi leo, ina kibarua kigumu cha kuhakikisha kinasonga mbele kwani inakutana na moja ya timu wenyeji katika michuano hiyo, Rayon Sport.
Rayon Sport ni ya pili katika kundi hilo la A ikiwa na pointi nne, moja nyuma ya Azam FC yenye pointi tano.
Mechi nyingine leo ni kati ya Adama City dhidi ya Atlabara ambazo nazo zina nafasi ya kusonga mbele katika robo fainali, kwani Adama ina pointi moja baada ya mechi mbili, wakati Atlabara wana pointi mbili kwa mechi mbili, wakibaki na mechi mbili.
Hivyo, timu zote hizi zitaingia uwanjani kusaka pointi tatu zikifahamu zina nafasi kubwa ya kucheza robo fainali kama zitachanga karata zao vizuri. Pambano jingine litaikutanisha Polisi ya Rwanda na Banadir ya Djibouti katika mechi ya Kundi C inayotarajiwa kuwa na upinzani mkali.</p>
Chanzo: HabariLeo