Klabu ya Yanga yamtimua kocha wake mkuu Romain Folz baada ya kichapo kutoka kwa Silver Strickers

Klabu ya Yanga yamtimua kocha wake mkuu Romain Folz baada ya kichapo kutoka kwa Silver Strickers

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Klabu ya Young Africans ya Tanzania imetangaza kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza, Romain Folz.

Katika taarifa yake ya leo Oktoba 18, 2025, mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, wametangaza kuachana na Folz huku nafasi yake ikichukuliwa na kocha msaidizi Patrick Mabedi.

Uamuzi huo unakuja saa chache baada ya Young Africans kufungwa bao 1-0 na Silver Strikers ya Malawi katika mchezo wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, uliofanyika leo Oktoba 18 katika uwanja wa Bingu jijini Lilongwe.

1760812342483.png
Soma Pia: FT: Silver Strikers 1-0 Yanga SC | CAF CL | Second preliminary round Leg 1 of 2 | Bingu National Stadium| 18.10.2025 | Saa 10:00 Jioni
 
Klabu ya yanga sc imefikia makubaliano ya kuachana na kocha wake Roman Folz kufutia mfululizo wa mwenendo mbaya wa timu hiyo yangu alipoanza kuifundisha,

Uamuzi huo unakuja mara baada ya timu ya hiyo kupoteza mghezo wake wa mzunguko wa kwanza wa ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Silver strikers ya nchini malawi
Screenshot_20251018-213231.png
 
Uto bwana uvumilivu hawana yaan wao wanadhani ndo wamezaliwa kufunga tu ...washamba sana mtafukuza mpaka vibwengo ....
 
Tayari Jangwani kumewaka
 
Uchizi Vunga.Bao la chizi anayevunga limesababisha bikira itoke na mfuniko.
 
UONGOZI wa Young Africans Sports Club unapenda kuutaarifu umma kuwa, umevunja mkataba wa Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza, Romain Folz.

Uongozi wa Young Africans SC unamshukuru kocha Romain Folz kwa mchango wake ndani ya Klabu yetu na unamtakia kila la kheri katika majukumu yake yanayofata.

Katika kipindi hiki kikosi chetu kitakuwa chini ya Kocha Msaidizi Patrick Mabedi huku mchakato wa kutafuta Kocha Mkuu ukiendelea.

Imetolewa na
Idara ya Habari na Mawasiliano
YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB
Soma Pia>>
I told them
 
Back
Top Bottom