bakundande jr
JF-Expert Member
- Oct 22, 2021
- 507
- 670
Real betis ni miongoni mwa klabu kongwr zinazoshiriki ligi kuu nchini Spain maarufu kama La liga.
Kwa njia ya kipekee kabisa ili kuleta mabadiliko katika historia ya klabu hio hususani katika suala la uwanja wao wa mpira, klabu hii ilamaua kuanzisha shindano lililohusisha watu wengi duniani.
Lengo la shindano hili ni kupata ubunifu wa uwanja wa mpira ambao utakuwa bora zaidi na wa kisasa zaidi kuliko uwanja wa sasa wa Real Betis. Uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuchukua idadi kubwa ya mashabiki, na utakuwa na vifaa vya kisasa zaidi vya teknolojia.
Pia klabu hiyo ilitangaza ya kuwa washindi wa shindano hilo watapata zawadi ya pesa pamoja na fursa ya kufanya kazi na Real betis.
Klabu hiyo ilitangaza kuwa tarehe 31 desemba 2020 kuwa ndio mwisho wa kupokea michoro kutoka kwa wabunifu.
Baada ya michoro mingi kupita bodi ya watendaji wa klabu hiyo ilikaa na kupitia mchoro mmoja baada ya mwingine na hatimae kuchagua mchoro ulionekqna kuvutia zaidi. Katika mchoro huo unaoneshq ya kuwa uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuingiza watazamaji 60379 ikiwa ni karibu mara nne zaidi ya uwanja wao wa awali unaoingiza watazamaji 15000+.
Cha muhimu kutoka katika shindano na hadithi hii ni kuwa klabu zetu kuongwe na penda hapa nchi, nazungumzia mapacha toka kariakoo yaani wekundu wa msimbazi (simba) na ndugu zao wananchi (yanga) zinaweza kujifunza kitu sio tu kuazisha program za kuchangia pesa hata katika maswala ya ubunifu zinaweza kushirikisha mashabiki na wanachama wake.
Hii inaweza kuongeza mapato na mapenzi kwa vilabu hivi.
Pichani hapo chini ni mchoro wa uwanja uliochaguliwa kutoka katika shindano hilo.
Na bakundande jr
Naomba kuwasilisha