Klabu ya Everton imemtimua kocha Martinez

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Ikiwa msimu wa ligi kuu soka nchini Uingereza unakaribia kufikia tamati leo klabu ya Everton iliyopo katika jiji la Liverpool imemfukuza kazi kocha mkuu, Roberto Martinez baada ya kuitumikia timu hiyo kwa muda wa miaka mitatu.

=================
150212132248_roberto_martinez_640x360_afp_nocredit.jpg


Roberto Martinez
Klabu ya Everton imempiga kalamu mkufunzi wake Roberto Martinez baada ya kuifunza klabu hiyo kwa miaka mitatu.

Kilabu hiyo ya Martinez ilio katika nafasi ya 12 katika jedwali li ligi ya Uingereza ilishindwa 3-1 na mabingwa wa ligi Leicester siku ya Jumamosi na kupoteza 3-0 dhidi ya Sunderland siku ya Jumatano.

Everton ilipoteza katika nusu fainali ya kombe la FA na lile la Carling msimu huu.

Timu hiyo imeshinda mechi tano pekee nyumbani msimu wote na inatarajiwa kumaliza msimu huu ikiwa na pointi za chini zaidi tangu uzinduzi wa pointi tatu kwa ushindi wowote mnamo mwaka 1981.

Klabu hiyo inatarajiwa kuthibitisha rasmi hatua yao.Kumekuwa na ongezeko la maandamano dhidi ya kocha huyo raia wa Uhispania kutoka kwa mashabiki katika mechi zilizochezwa nyumbani.

Chanzo: BBC
 
Ni mida muafaka wa kufukuza kocha kwa sasa, sio unafukuza kocha kati na kati ya msimu, wapo makocha wengine wanaohitaji kufukuzwa akiwemo mzee wenger
 
Back
Top Bottom