KKKT kwalipuka

KKKT kwalipuka

bucho

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2010
Posts
5,172
Reaction score
3,265
meandikwa tarehe 20 Desemba 2012 By John Mhala, Arusha Imesomwa mara: 725


Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati, Thomas Laizer




MGOGORO umeibuka kati ya baadhi ya waumini na viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati, baada ya kuweka mali za kanisa rehani na kuchukua mkopo ambao sasa unahatarisha mali hizo kunadiwa.


Hali hiyo imesababisha baadhi ya waumini wa dayosisi hiyo kuwatupia lawama viongozi wakuu wa kanisa hilo akiwemo Askofu Mkuu Thomas Laizer na Katibu Mkuu wake, Israel Karyongi na kuwataka wajiuzulu.


Viongozi hao wanadaiwa kuwa ndio chanzo cha kufikia hali hiyo na kwamba wamekuwa wakitumia miradi ya kanisa hilo kwa manufaa yao binafsi na kusababisha mali hizo kuwa hatarini kunadiwa na benki.


Habari za kutoka ndani ya Dayosisi hiyo, zinadai kuwa miradi inayodaiwa kuwa fedha zake zimetumika vibaya ni Hoteli ya Corridor Springs na Hospitali ya Rufaa ya Selian, ambayo kwa pamoja iligharimu Sh bilioni 11 kutoka katika michango ya waumini na misaada kutoka kwa wafadhili.


Hata hivyo, wakati ikidaiwa kuwa fedha hizo zimetokana na michango ya waumini na wafadhili, kuna madai mengine kuwa zilikopwa katika moja ya benki nchini kwa ajili ya uanzishwaji wa miradi hiyo.


Kutokana na hatari ya kunadiwa kwa miradi hiyo, waumini zaidi ya 600,000 wa Dayosisi hiyo wiki moja iliyopita wametakiwa kuchangia Sh 20,000 kila mmoja ili kuokoa jahazi. Kama waumini wote hao wakitoa mchango wao kama ilivyotarajiwa, zitapatikana Sh bilioni 12.


Waumini wanena


Wakizungumza na gazeti hili baada ya ibada Jumapili iliyopita, baadhi ya waumini walionesha wazi kutilia shaka hatua ya viongozi hao kuwachangisha michango wakati awali waliambiwa kuwa miradi hiyo ilidhaminiwa kwa asilimia 100 na Shirika la Peace House la Marekani.


“Tuliambiwa awali kuwa miradi hii ambayo iligharimu Dola za Marekani milioni 7 sawa na Sh bilioni 11 za Tanzania, ilidhaminiwa na Shirika la Peace House la Marekani, leo wanatuambia walikopa fedha benki (anaitaja). “Haikubaliki hapa kuna ufisadi umefanyika, tunataka Mzee Laizer (Askofu) na Katibu Israel Karyongi wakae pembeni,” alisema mtoa habari wetu.


Chanzo cha kukopa fedha hizo benki inadaiwa wakati miradi hiyo ikiwa katika hatua zake za kukamilika, wafadhili wa miradi hiyo walibaini hujuma iliyokuwa ikifanywa na viongozi wa Kanisa, wakajitoa kufadhili kulitaka Kanisa kurejesha fedha zao.


“Wafadhili walipojitoa, wazee hawa wakaenda benki kukopa fedha ili kuwarejeshea wazungu hao fedha zao lakini kwa sharti kuwa miradi hiyo iwe dhamana ya mkopo hadi watakapomaliza kulipa. “Lakini cha kushangaza wakati wanakopa hawajashirikisha washarika mpaka hapo walipokiuka mkataba na benki kugundua kuwa hawana uwezo wa kulipa mkopo kwa wakati ndipo wanatuambia sasa… tunashangaa ndio maana tuna wasiwasi,” aliongeza muumini mwingine ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.


Kutokana na hali hiyo ya kukiuka masharti ya mkopo, mtoa habari huyo alidai benki hiyo iliandika barua kwa Dayosisi hiyo, kuelezea kusudio la kuzikamata mali hizo za washarika kabla ya Januari mosi mwakani.


“Bila aibu wanakuja na kuwatangazia washarika kuwa tunadaiwa na ikifika Desemba 31 kama hatujalipa deni hilo, hoteli itauzwa kwa mnada. Hii haikubaliki lazima hatua zichukuliwe haraka na watakaobainika kuhusika wafikishwe mahakamani,” alidai muumini ambaye ni mzee wa Kanisa katika Kanisa la Mjini Kati.


Washarika hao wamemtaka Askofu Laizer kumfukuza kwanza kazi Karyongi, ambaye ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya Hoteli ya Corridor Springs ndipo na yeye atafakari nafasi yake.


“Huu ni uzembe wa hali ya juu katika kusimamia mali zetu na hapa kuna mgongano wa kiuongozi kati ya Askofu na Katibu, ambaye pia ni msimamizi wa mali zetu,” alidai msharika huyo.


Alituhumu uongozi wa Kanisa kwa kukiuka mkataba na benki iliyotoa mkopo ambao katika kipengele kimojawapo, unailazimisha kanisa kutumia benki hiyo peke yake katika kurejesha fedha zake, lakini viongozi wamefungua akaunti katika benki moja ya biashara ya nchi jirani yenye matawi yake nchini.


Deni linapotoshwa


Akijibu tuhuma hizo, Karyongi alisema hakuna tishio la kukamatwa kwa mali za kanisa, lakini alikiri kanisa linadaiwa na benki Sh bilioni moja na si Sh bilioni 11 kama inavyodaiwa na deni hilo ni malimbikizo ya nyuma. Aliwatupia lawama baadhi ya waumini, akidai ndio wanaotaka kutumia mwanya huo kulivuruga kanisa hilo.


Kuna watu huko mitaani wanataka kutumia waraka wa Askofu wa kuwachangisha washarika kuleta vurugu katika Dayosisi,” alisema na kuongeza: “Lugha iliyotumika katika waraka tuliowasomea washarika imetafsiriwa vibaya, ni kweli tunadaiwa na benki ila tuliwahadharisha washarika ndio maana tulisema huenda vitu tulivyoweka dhamana vikakamatwa.”


Katibu huyo aliongeza kuwa deni pekee ambalo imelazimu kuomba michango ya waumini ni la hoteli na haihusiani na hospitali. Pia alisema kukamatwa kwa mali za kanisa kwa sasa si jambo kubwa linaloweza kusababisha mgogoro katika dayosisi kama inavyodhaniwa na watu. Kuhusu tishio la waumini kugoma kuchangia kulipa deni hilo, Karyongi alisema hakuna jambo kama hilo.


“Hizi ni mali zao, watagomaje? Mimi sina taarifa hizo na wakuu wa majimbo wako hapa hakuna anayejua kuhusu kugoma kwa waumini,” alisema.


Haiwezekani kujiuzulu


Kuhusu kutakiwa kuachia nafasi zao ili kupisha uchunguzi, Karyongi alisema ni jambo lisilowezekana. “Askofu atatoa huduma mpaka mwaka 2016 na bado ana uwezo wa kufanya kazi zake kwa mujibu wa katiba yetu, hata mimi hakuna sababu, kwa nini nijiuzulu katika nafasi yangu?” alihoji katibu huyo.


Wakati katibu huyo akijinasibu, taarifa zinadai kuwa huenda akachukuliwa hatua katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Dayosisi kilichotarajiwa kukutana jana jijini hapa.


Kwa mujibu wa chanzo chetu ndani ya kikao hicho pamoja na mambo mengine, uamuzi wa kuwachangisha washarika utajadiliwa na kama italazimika baadhi ya wakuu wa dayosisi watachukuliwa hatua.


“Tunasubiri kwa hamu kubwa taarifa ya Katibu na kuijadili kwa kina, endapo tutaona inafaa atalazimishwa kukaa kando,” alidai mtoa habari wetu.
 
Hali bado tete KKKT

Imeandikwa tarehe 21 Desemba 2012 By John Mhala, Arusha


HALI ni tete ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati, baada ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Dayosisi kilichoitishwa kujadili madeni makubwa yanayoikabili Dayosisi hiyo, kusambaratika juzi.


Kuvunjika kwa kikao hicho kilichoitishwa kwa dharura, kulitokana na wajumbe wa kikao hicho kugawanyika pande mbili kutokana na tofauti za misimamo ya wajumbe.


Mgawanyiko huo umetokana na upande mmoja kutaka Bodi ya Hoteli ya Corridor Springs chini ya Uenyekiti wa Katibu wa Dayosisi, Israel ole Karyongi kuwajibika huku upande mwingine ukipinga hoja hiyo.


Hoteli hiyo inayomilikiwa na Dayosisi hiyo iko hatarini kupigwa mnada baada ya kushindwa kulipa marejesho ya mkopo uliochukuliwa kutoka benki moja ya biashara ili kuijenga mwaka 2006.


Habari kutoka ndani ya kikao hicho kilichofanyika katika hoteli hiyo, zinasema kulitokea mabishano miongoni mwa wajumbe na mwishowe kikao kilimalizika bila kufuata utaratibu wa kawaida wa mikutano unaohusisha sala ya kufungia.


"Mwandishi hali ni mbaya, kulikuwa na mabishano makali upande mmoja ukitaka Bodi ya Hoteli iwajibishwe wakiwa na hoja na wengine wakipinga bila hoja…kila mjumbe aliamua kuondoka ukumbini bila kuaga wala kufikia msimamo wowote," alisema mtoa habari wetu ambaye ni mjumbe wa kikao hicho.


*Wasusa chakula


Alisema mabishano na malumbano hayo, yalisababisha chakula kilichoandaliwa kwa ajili ya wajumbe hao kisuswe huku baadhi ya wajumbe wakiamua kununiana.


"Imefikia mahali wajumbe hata kusalimiana hawataki kutokana na tofauti zao, lakini inabidi kusali sana kuiombea Dayosisi yetu isisambaratike kwani watu wanatetea ufisadi wakati wengine wanataka viongozi wa kanisa hilo wawajibike kwa uzembe huo," aliongeza mjumbe mwingine ambaye hakutaka jina lake kutajwa gazetini.


Karyongi alipopigiwa simu jana alikataa kata kata kuzungumzia yaliyojiri katika kikao hicho akidai kuwa yupo safarini na atafuwe Jumatatu ijayo ili kutoa ufafanuzi kama ikibidi.


Chanzo cha mgogoro


Hali ya sintofahamu katika Dayosisi hiyo imetokea baada ya waumini wake kutakiwa kuchangia Sh 20,000 kila mmoja, ili kulipa deni la benki hiyo ya biashara kabla ya Desemba 31, mwaka huu ili kunusuru mali za Dayosisi hiyo ikiwamo Hoteli ya Corridor Springs na Hospitali ya Rufaa ya Selian zisipigwe mnada.


Chanzo cha mgogoro huo ni maagizo mawili tofauti ya kuwataka waumini hao wachangie kunusuru mali za Dayosisi hiyo yaliyotolewa ndani ya mwezi mmoja uliopita.


Katika maagizo ya kwanza yaliyotolewa kwa wakuu wa majimbo wa Dayosisi katika kikao kilichoketi Novemba 27, mwaka huu, ilielezwa kuwa deni lilikuwa Sh milioni 680.


Habari za uhakika zilisema kuwa kikao hicho kiliamua kila jimbo lichangie fedha kwa kadiri ya uwezo wa waumini wake na kila moja lilipangiwa kiasi wanachotakiwa kuchanga ili kuokoa mali za Dayosisi.


Kwa mfano moja tu katika makadirio hayo, Jimbo la Arusha Magharibi lilitakiwa kuchangia Sh milioni 300 kabla ya mwishoni mwa Machi mwakani.


Vyanzo vya habari vilisema kuwa maagizo hayo yalitolewa kwa wakuu wa majimbo sita yanayounda Dayosisi hiyo ya Kaskazini Kati. Hata hivyo, wakati maagizo hayo yakitekelezwa, Desemba 9, mwaka huu Makao Makuu ya Dayosisi ilitoa waraka wa kutaka kila muumini kuchangia Sh 20,000 kama kiwango cha chini kabla ya Desemba 31, mwaka huu.


Hatua hiyo ilidaiwa kuwa na lengo la kunusuru mali za Dayosisi hiyo hasa Hoteli ya Corridor Springs inayodaiwa na benki kiasi kinachofikia Sh bilioni 11 kutokana na malimbikizo ya mkopo.


Hata hivyo, Karyongi hivi karibuni alilieleza gazeti hili kuwa deni hilo si Sh bilioni 11 kama inavyodaiwa bali ni Sh bilioni moja ingawa kwa waraka wa kuwataka waumini zaidi ya 600,000 kuchangia Sh 20,000 kila mmoja, wangepata Sh bilioni 12.


Aidha, taarifa zilizolifikia gazeti hili zilibainisha kuwa Askofu Mkuu wa KKKT, Dk Alex Malasusa amewasili jijini Arusha, na inaelezwa kuwa mgogoro huo ni mojawapo ya sababu ya kuwapo hapa.
 
Acheni ku exaggerate, mambo ni tofauti kabisa na yanavyo ripotiwa


wewe unajua nini ? acha kuficha uchafu wa askofu na karyongi. hawafai hata kidogo . usitake tuongee mambo mazito hapa.
 
KKKT siku si nyingi litakuja kuwa kanisa la Anglican..
 
Tatizo ni Askofu Laizer amekaa madarakani muda mrefu sana almost more than 35 years !.
 
tunamstahi kidogo paka atoke ICU alikolazwa ila ni mchafu sana hafai hata kuwa mzee wa usharika licha ya kuwa askofu.
 
tunamstahi kidogo paka atoke ICU alikolazwa ila ni mchafu sana hafai hata kuwa mzee wa usharika licha ya kuwa askofu.

Hii ndio namna ya kutatua matatizo ya kanisa lenu?

Maelekezo haya mmeyapata kwenye Bible yenu au ni akili zile zile za kina Ponda walioko gerezani?

Yawezekana ukapata sifa na ujiko toka kwa watu ambao hata hamfahamiani, lakini umeshajiuliza nafasi yako mbele ya Mungu wako?
 
tunamstahi kidogo paka atoke ICU alikolazwa ila ni mchafu sana hafai hata kuwa mzee wa usharika licha ya kuwa askofu.

Madai haya sidhani kama yanaukweli kwani mfumo wa KKKT wa Miradi na utunzaji wa fedha ni makini sana, kutokana na ukweli kuwa wapo wahasibu na kamati mbalimbali ambayo huhusika kwenye usimamizi wa fedha na miradi mbalimbali na hakuna malipo ambayo yanafanyika bila kamati ya fedha kuelewa kinachoendelea, nitashangaa sana kama askofu ana uwezo wakuchota fedha au kutapanya atakavyo. Pia kudaiwa au kushindwa kulipa marejesho ya mkopo kwa Taasis yeyoyete ni jambo la kawaida na sio kitu cha ajabu, wakristo ni watu wanaothubutu kufanya maendeleo hivyo kama mkopo umeshindwa kurudisha faida ni sahihi waumini wakachangia na kazi kuendelea. Kutoa tuhuma zisizo na ushahidi wa vielelezo ni hatari na ni laana kwani kumkebehi au kumvunjia heshima mpakwa mafuta wa Bwana ni laana.

mimi sio msharika wa Dayosisi tajwa ila mengi makubwa yamefanyika na sidhani kuwa kuna dayosisi yeyote chini ya KKKT ambayo inamiradi mingi kushinda Dayosisi ys Arusha, hivyo tuwatie moyo na kuwashauri badala ya kuchochea chuki za kuwavunja moyo washarika.
 
Tatizo ni Askofu Laizer amekaa madarakani muda mrefu sana almost more than 35 years !.
Ngongo, heshima kwako......off point.....zawadi wa xmas umeiona pale mahakama ya rufaa jijini DSM??!!??
 
Last edited by a moderator:
Habari hii ni kweli kabisa,halafu hawa viongozi wetu hawatoi ripoti ya mapato na matumizi ya hii miradi kitu ambacho kinatusikitisha tulio wengi;ngoja nitoe mfano mdogo hapa,seliani ni hospitali yetu lakini kufungua tu file pale ni 20,000;nauliza mkristo wa kawaida anaeuza mboga mboga ataweza kupata matibabu katika hosp.hii? Je imejengwa kwa faida ya nani?manufaa yake kwa msharika mdogo ni upi? Kwa kweli hawa watu nadhubutu kusema hawastahili kuwepo kwenye nafac zao tena.mimi nadhani wakristo wenye kipato kidogo wangepewa kipaumbele ktk hosp.hii.
Ushauri wangu kwa hawa waheshimiwa ni kwamba watu wamesoma na ni waelewa kwa hiyo taratibu zote za uendeshaji ni vyema zikafuatwa.
Jambo lingine tetesi zilizopo ni kwamba manager wa corridor spring ni mwenyeji wa nchi jirani.je?arusha amekosekana mtu mwenye hiyo taaluma? Au amekosekana mkristo wa dhehebu hilo mwenye taaluma kama hiyo? Ok.inawezekana amekosekana je arusha/tanzania hakuna mwenye taaluma kama hiyo? Huo ni mradi wao na mimi kwa dhati nawapongeza wakristo kwa msimamo wao wa kuchangia kidogo/kutokuchangia kabisa.
 
... Ni kawaida ya SHETANI kukaa karibu na wacha Mungu. Kuweni makini wanaKKKT, mnakaribishwa kwenye himaya ya Lucife Satanic, the fallen Angel.
 
Habari hii ni kweli kabisa,halafu hawa viongozi wetu hawatoi ripoti ya mapato na matumizi ya hii miradi kitu ambacho kinatusikitisha tulio wengi;ngoja nitoe mfano mdogo hapa,seliani ni hospitali yetu lakini kufungua tu file pale ni 20,000;nauliza mkristo wa kawaida anaeuza mboga mboga ataweza kupata matibabu katika hosp.hii? Je imejengwa kwa faida ya nani?manufaa yake kwa msharika mdogo ni upi? Kwa kweli hawa watu nadhubutu kusema hawastahili kuwepo kwenye nafac zao tena.mimi nadhani wakristo wenye kipato kidogo wangepewa kipaumbele ktk hosp.hii.
Ushauri wangu kwa hawa waheshimiwa ni kwamba watu wamesoma na ni waelewa kwa hiyo taratibu zote za uendeshaji ni vyema zikafuatwa.
Jambo lingine tetesi zilizopo ni kwamba manager wa corridor spring ni mwenyeji wa nchi jirani.je?arusha amekosekana mtu mwenye hiyo taaluma? Au amekosekana mkristo wa dhehebu hilo mwenye taaluma kama hiyo? Ok.inawezekana amekosekana je arusha/tanzania hakuna mwenye taaluma kama hiyo? Huo ni mradi wao na mimi kwa dhati nawapongeza wakristo kwa msimamo wao wa kuchangia kidogo/kutokuchangia kabisa.

Jamani tumuogope Mungu, mbona mimi inaniwia vigumu kuamini hili! Kufungua file 20,000? Au ulimaanisha 2,000 mkuu?

Kwa hili la Meneja wa Corridor Spring kuwa mgeni tuache fikra mgando. Kama Corridor Spring ni kitega uchumi na kinaendeshwa kibiashara basi misingi ya biashara lazima iheshimike. Hili suala la Mtanzania Mtanzania halina tija. Wote tunafahamu uwezo na tabia zetu linapokuja suala la uwajibikaji.

Sea Cliff Hotel ilikuwa na Mkurugenzi Muingereza, na mameneja kadhaa Makaburu, hii yote ni suala la taaluma na kuchukua uzoefu wa huyo aliyetolewa mbali. Hata Taifa Starz ina kocha mgeni
 
Nilidhani pesa zililiwa, kumbe zilileta maendeleo.
Mbona hawaini msaada unaoletwa na hospitali ya seliani?
Hizi ni dalili za uchu wa masaraka kwa baadhi ya watu sio na mapenzi mema na kanisa
 
Back
Top Bottom